4 May 2010

Wiki moja baada ya kusherehekea mwaka wake wa 115 tangu azaliwe,binadamu mwenye umri mkubwa zaidi duniani amefariki katika kisiwa cha kaskazini mwa Japan cha Okinawa.Kama Chinen alizaliwa tarehe 10 ya mwezi Mei mwaka 1895 na kubahatika kushuhudia karne tatu tofauti,kwa mujibu wa wa taasisi ya utafiti wa vipengele (aspects) vya kijamii,saikolojia na baiolojia vya ukuaji wa binadamu (Gerontology Research Group)


Kikongwe huyo alifariki Jumapili iliyopita kwenye nyumba ya kutunza wazee/wagonjwa (care home)japokuwa taarifa za kifo chake hazijatolewa kwa nduguze ambao wamekuwa wakilinda faragha ya bibi hiyo kwa makini.

Kisiwa cha Okinawa kina sifa ya kuwa na wakazi wenye maisha marefu hali inayohusishwa na mlo wa asili wa mchaichai (green tea),supu ya 'miso',mbogamboga,wali na samaki.

Kama ameshikilia rekodi ya umri mkubwa duniani tangu mwezi Sptemba mwaka jana,baada ya kikongwe Gertrude Baines kufariki akiwa na umri wa miaka 115 huko Los Angeles nchini Marekani.Baada ya kifo cha Kama,rekodi yake sasa inabaki kwa bibi wa Kifaransa,Eugenie Blanchard,aliyezaliwa mwezi Februari mwaka 1896.Mwingereza Florence Emily Baldwin,wa Leeds,anashikilia nafasi ya pili akiwa na umri wa miaka 114 pia.Japo bibi huyo anasema kuwa kula sandiwichi ya mayai (egg sandwich)ndio siri ya kuishi kwake miaka yote hiyo,wataalam wanahisi maisha yasiyohusisha uvutaji sigara,unywaji pombe na kufanya kazi kwa bidii kumechangia zaidi.

Imetafsiriwa kutoka kituo cha runinga cha Sky


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.