5 Sept 2010

Pasipo kutarajia,CCM inaweza kulazimika kuuambia umma kwanini mafisadi waliotajwa kwenye List Of Shame (orodha ya mafisadi sugu iliyowekwa wazi na Chadema viwanja vya Mwembeyanga) hawajachukuliwa hatua hadi leo.Kama ambavyo chama hicho tawala kilivyokosa umakini katika kuongoza nchi ndivyo walivyokurupuka na kuwasilisha malalamiko yao NEC wakidai "wametukanwa kwa kuitwa mafisadi".Sijui ni ulevi wa madaraka au ubabaishaji tu kiasi kwamba walisahau kuwa wote waliotajwa katika List of Shame hawajathubutu kwenda mahakamani kama walivyotishia kwa kuogopa "kuwekwa uchi zaidi".Sasa wamejipeleka mahakamani wenyewe kwa kudai tuhuma hizo ni kashfa.Utamu wa stori hii uko kwenye ukweli kwamba ukidai nimekukashifu basi unawajibika kuthibitisha tuhuma nilizotoa dhidi yako sio za kweli.Kibaya zaidi kwa mafisadi waliotajwa,CHADEMA wana ushahidi mzito dhidi ya watajwa.Patamu hapo!

Hebu soma habari husika

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewasilisha ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) majibu ya utetezi wake kuhusu malalamiko ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa kimeikashifu viongozi wake waandamizi wakati wa uzinduzi wa kampeni huku kikitoa orodha ya mafisadi kama moja ushahidi kwake.
Katika majibu hayo imo orodha ya majina 12 ya watuhumiwa wa ufisadi ambayo iliwahi kutangazwa na Chadema mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembeyenga.
Naibu katibu wa Chadema John Mnyika jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa wamechukua hatua hiyo ili kuthibitisha kauli zao walizozitoa kwenye uzinduzi wa kampeni zao wiki moja iliyopita katika viwanja vya Jangwani.
“Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chadema inaeleza wazi kuwa viongozi wote ambao walishabainisha kuhusika na tuhuma za ufiasadi na ubadhilifu wa mali ya umma ambao serikali imeshindwa kuwafikisha mahakamani, watafiishwa mahakamani ndani ya siku 180, iwapo tutaingia madarakani,” alisema Mnyika.
Alisema watuhumiwa hao wakiwamo marais wastaafu ambao wataondolewa kinga yao na Bunge ili wafikishwe mahakamani.
Mnyika alifafanua kuwa hatua hiyo imelenga katika kujenga uongozi bora na kuimarisha utawala wa sheria hapa nchini.
Kuhusu kutaja orodha ya majina ya mafiasadi kwenye mkutanio huo chama hicho kilisema huo si ukiukaji wa maadili ya uchaguzi kwakuwa tuhuma hizo zipo na wahusika hadi sasa hawajachukuliwa hatua na baadhi yao wanagombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Alisema madai yote waliyoyatoa kwenye viwanja hivyo wana ushahidi nayo na mengi ni yale ambayo tayari waliwahi kuyaweka wazi siku za nyuma.
Kwa sababu hiyo, Chadema iliitaka Nec kutupilia mbali malalmiko ya CCM kwa sababu waliwasilisha bila kusoma sheria za maadili.
CHANZO: Mwananchi

Hatimaye watajwa kwenye List of Shame wanaweza kulazimika kuuthibitishia umma kwanini wasiwe jela muda huu wanaopita huku na kule kuomba wachaguliwe tena.


Patamu hapo!!!

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.