20 Sept 2010

Image and video hosting by TinyPic
UBISHI TUUU: HUU UTITIRI WA MASHANGINGI SIO UTHIBITISHO WA MAISHA BORA?SASA HIYO NI AWAMU YA KWANZA.AWAMU IJAYO NI BAJAJ KWA WAJAWAZITO NCHI NZIMA


MAJI BWERERE

MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YAMEWEZEKANA

USHAHIDI WA MAISHA BORA UNAONEKANA HATA KWA WATOTO WADOGOYOU SEE, TATIZO LA MAJI MIJINI NA VIJIJINI LIMEPATIWA UFUMBUZI WA KUDUMU
TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI MIJINI LIMEMALIZWA.MNATAKA MAISHA BORA YAPI ZAIDI YA HAYA?

MNAONA?POLISI WENYE MAKAZI DUNI SASA WANA SWIMMING POOL HAPO MSIMBAZI POLICE FLATS.MAISHA BORA KWA POLISI YAMEPELEKEA WAACHE KUDAI RUSHWA NA KUBAMBIKIZA KESI KWA WALALAHOI
Image and video hosting by TinyPic
KURA ZA ALBINO ZIMEZAA MATUNDA.HUYO MGOMBEA WA CCM WANAYEDAI  NI MTUHUMIWA WA BIASHARA YA VIUNGO VYA ALBINO NI SIASA ZA MAJITAKA TU


Image and video hosting by TinyPic
HATA SUPAMODO NAOMI CAMPBELL ALIPOTEMBELEZA TANZANIA ALIRIDHISHWA NA HALI ALIYOKUTA WODI YA AKINAMAMA.NA AKATOA MACHOZI YA FURAHA 


BARABARA ZETU NI MARIDADI.TUMELETEWA MATREKTA MENGI MNO KWA  KILIMO KWANZA  HADI INABIDI YAFANYE KAZI YA KUVUTA MALORI.EBO!KWANI CHA AJABU NINI TREKTA KUVUTA LORI?NI FERI ZA NCHI KAVU HIZO

CHAGUA KIKWETE NA CCM KWA BARABARA BORA.NA 2010-2015 BARABARA KAMA HIYO HAPO JUU ZITAKUWA UPGRADED TO FLYOVER.

SERIKALI YA KIKWETE IMEWAJALI SANA WANAFUNZI NA KUWANUNULIA MADAWATI BORA MNO HADI YANAWACHOSHA KUYAKALIA NA KUAMUA KUKAA SAKAFUNI

HAPANA.KOSA LA MSOMI HUYO WA CHUO KIKUU ANAYEFUKUZWA NA FFU NI KUGOMA KUCHUKUA HELA ZA KUJIKIMU ZILIZOINGIZWA KWENYE AKAUNTI YAKE KABLA HAJAWASILI CHUONI.HAPO ASKARI WA FFU ANAMHAMASISHA MSOMI HUYO AENDE BENKI.CHAGUA KIKWETE USOME KWA RAHA MUSTAREHE

NDIO MAANA RAIS MPENDWA JAKAYA KIKWETE ALISEMA MIMBA ZA WANAFUNZI NI KIMBELEMBELE CHAO TU.ANGALIA MWENYEWE MAZINGIRA BORA KABISA YA NAMNA VIJANA WETU WANAVYOPATA ELIMU.KIKWETE OYEEE

BAADA YA MABILIONI YA KIKWETE,NA KAGODA KUREJESHA MABILIONI,SASA MAISHA BORA NI KWA MWENDO WA PIPI KWA KILA MTOTO.YAH,PIPI KWANZA KISHA LAPTOP KWA KILA MWANAFUNZI.HALAFU HUYO SLAA ANAPOSEMA ATATOA ELIMU YA BURE KWANI MIE NAUZA HIZI PIPI?

SAFARI MOJA HUANZISHA NYINGINE.KWANI MLIPONICHAGUA MLITAKA NIOTE MATENDE IKULU?

MFANO HAI WA AMANI NA UTULIVU

ZAPATERO ANAELEKEA KUSHANGAA: HIVI KAMA HUYO JAMAA ANA MAWAZO YA HALI YA JUU KIASI HIKI KWANINI BADO NCHI YAKE NI MASIKINI?NO,HAPO KIKWETE ANAHUBIRI KUHUSU CHANZO CHA UMASIKINI WA AFRIKA JAPO HAFAHAMU KWANINI TANZANIA NI MASIKINI

AKINAMAMA WAMEPEWA KIPAUMBELE CHA HALI YA JUU KATIKA MIPANGO YA SERIKALI YA KIKWETE.PICHA INAWAONYESHA KAMA WANA MAJONZI LAKINI UKWELI NI KUWA WAMESHIKWA NA BUTWAA KUTOKANA NA KAZI NZURI YA CHAGUO LA MUNGU KIKWETE


MMENG'ANG'ANIA TU SUALA LA EPA NA KAGODA NA KUSAHAU MINARA PACHA.BY THE WAY,FEDHA ZA EPA HAZIKUIBWA BALI ZILIAZIMWA TU,NDIO MAANA NILIWASIHI TULIOWAAZIMA WAZIREJESHE.WALIOAZIMWA WANAREJESHA IN KIND KWA KUCHANGIA KAMPENI ZA CCM

TEH TEH TEH,NICHEKE MIE.KIKWETE MTU BOMBA SANA.SIE TUMEKUJA NA KABRASHA TUPU LEO HII TUNA MABILIONI KWENYE AKAUNTI.ASANTE DOWANS KWA KUTURITHI,ASANTE KARAMAGI NA MSABAHA.ASANTE WATANZANIA KWA KUMWAMINI KIKWETE.SI MNAONA SASA TATIZO LA UMEME NI HISTORIA KAMA ALIVYOAHIDI CHAGUO LA MUNGU KIKWETE?
MWAKYEMBE NA TUME YAKE NI ROHO MBAYA TU.KAMA MUME WANGU LOWASSA ALIHUSIKA NA UFISADI WA RICHMOND MBONA KIKWETE AMEKUJA JIMBONI KUMPIGIA DEBE?
TATIZO LENU WATANZANIA MNA KUMBUKUMBU HAFIFU.MMESAHAU ENZI ZA Boyz II Men?MIE NA JAKAYA HATUJAFAHAMIANA MTAANI.MNABISHA?SI MMEONA JINSI MAJUZI ALIVYOMWAGIA SIFA JIMBONI MONDULI?

MNASEMA NASAFIRI SANA?KWANI MLIPONICHAGUA MLIKUWA HAMFAHAMU KUWA NILIPOKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NILIKUWA NASAFIRI SANA?ACHENI UZUSHI,SAFARI ZANGU ZITAILETEA TANZANIA SIFA YA KUVUNJA REKODI YA VASCO DA GAMA.

MTAJIJU....ACHE MIE NIBEMBEE 

JIJENGE HUKO UVCCM.SI UMEONA FAMILIA YA BUSH ILITOA MARAIS WAWILI KAMA YA KABILA HUKO DRC?BASI NA WEWE JIANDAE.MIE NAITWA CHAGUO LA MUNGU,WEWE UTAITWA CHAGUO LA BABA
WE KATUNI HUELEWI SOMO LIPI TENA?YANI UNAKUWA KAMAMIE NISIYEELEWA KWANINI TANZANIA NI MASIKINI!

PICHA YA JUU NA YA CHINI: CHAGUO LA MUNGU DANCING.BY THE WAY "Never Trust a Spiritual Leader who cannot Dance".-Mr Miyagi,The Next Karate Kid,1994

HUYU SLAA ANATAKA KUNIWEKEA MCHANGA BADALA YA UBWABWA KWENYE SAHANI HII.HIZI HABARI ZA MIE KUFUKUZWA UALIMU ZA NINI TENA MUDA HUU?
WANAKUJA NA USHAHIDI NINI?WANATOKEA HUKU AU KULE?ANYWAY,HAWAWEZI KUTHIBITISHA LOLOTE
MGOSI,UNAKUMBUKA SIKU ZILEEEE KATIKA SHULE ILEEE...BASI SLAA KAINYAKA HIYO ISHU.

29 comments:

 1. ha ha Gosh!I laughed to the extent that I can't define myself nomore.Kudos to the person who prepared this article..It absolutely touched me.Guys what are you waiting for?? Kikwete can't lead us and that's for sure.Too much smiling and pretending like Vasco Da Gama II will not help Tanzanian..So, Slaa all the way...

  ReplyDelete
 2. Kazi nzuri kaka tumeipenda endelea

  ReplyDelete
 3. Uchaguzi upite sie tupumue na haya mahadithi ya wanasiasa.
  Hongera kwa uchambuzi wa picha bwana chahali japo nahisi umeamua kuchagua baadhi tu ya picha. I dont believe kwamba Kikwete kafanya mabaya tu, atleast you should be fair to the guy despite all his mapungufus.

  ReplyDelete
 4. huyu si rais wa tanzania nathani, hii nchi haina hata kanuni zinazofatwa kila mmoja anafanya analotaka. tumeshapotezwa, tuanakazi kubwa sana kurudisha nchi kwenye uhai.

  ReplyDelete
 5. kazi safi sana kaka,we need changes

  ReplyDelete
 6. Kaka Nimeikubali kazi yako, Hongera kwa kutuamsha. Nchi yetu inaelekea kubaya kama tusipochukuwa hatua za kuwang'oa hawa wakoloni weusi. We need more blog like this. Kikwete ajue kuwa hatumtaki na ameshindwa kuliongoza Taifa letu, uroho wake wa madaraka na chama chake cha ufisadi ndio kinachotufanya watanzania kuwa na hali mbaya kama hii tulioiona kwenye hizi pics

  ReplyDelete
 7. Duh! hizi picha zaweza kuhamishiwa kwenye tv ya ITV au TBC jamani? Je twaweza kuzipata kwenye magazeti kama majira na mtanzania? Please hata jaribu kufanya bango pale Salander bridge wadau tutachangia yawe yanaonyesha at least for a day! Ikitoka hapo iende Mpanda, Ruvuma, Kigoma, Kagera na siyo mjini bali kulekule kwenyewe kwenye wapiga kura wengi. Itafaa.

  Shukrani mdau kwa hili.

  ReplyDelete
 8. well done for create this site tumechoka na michuzi ya ccm

  ReplyDelete
 9. kweli hizi picha zimetoa taswira nzuri sana ya jinsi mambo yalivyo. Nimefurahis sana kwa uchambuzi wa namna kama hii. watanzania tuamke, CCM imetuweka kwenye hali hiyo yunayoiona hapo juu, sisi bado ni maskini na cha kushangaza hatujui umaskini wetu utaisha lini. CCM hawana ufumbuzi wa tatizo letu hata moja, na kama hawawezi ni dhahiri kwamba wanatakiwa waondoke. Tanzania tuamke jamani, Dr Slaa ni mwanamapinduzi wa kweli. hii nchi sio ukoo, tumechoshwa na siasa za kale.

  ReplyDelete
 10. Mdau uliyeandaa nakupa Big Up, umetuamsha kweli, tufanyeje jamani ili huu ukweli uweze kufahamika kwa wapiga kura, ambao wengi wao wako mbali na mtandao huu. Ikiwezekana kila mdau unayesoma makala haya uprint copy, ili ukifika katika mtaa wako uwavutie kastori hii wenyeji wetu ambao hawana hili wala lile, na usisahau kufunga kastori kwa kuwaomba nao wahakikishe wanafanya uamuzi mzito kubadili hali hii, kwa kuitumia vizuri tarehe 31 Oct. 2010. aidha kila mmoja kwa nafasi yake, kama unaweza fupisha ujumbe huu bila kubadili maana uweke kwenye simu then foward kwa waana wa nchi hii. Ni kwa kukumbushana tunaweza kufanya badiliko. ASANTE SANA TUKO PAMOJA

  ReplyDelete
 11. mafisadi footballl kilabu 1. kikwete 2 lowassa 3.??? 4. Chenge 5. makamba? 6. Kalamaji 7. Hosea 8.....9......10...... 11.... wachezaji wa akiba

  1. saluma kk 2... Nimeshindwa kumalizia kwani inauma naomba wadau mnisaidie kumalizia orodha ili wadanganyika wajue watu wanao wapa ofisi

  ReplyDelete
 12. Lol great! this is fantastic i never thought all of this situations, now you have opened my eyes, cant imagine if CCM will win again i think poverty will be doubled....

  good author. Slaa take on your way! tired of this guy...

  ReplyDelete
 13. kazi ni kubwa

  ReplyDelete
 14. Inasikitisha lakini ndio ukweli tuamke kwa mabadiliko

  ReplyDelete
 15. woooow!! what a way to present!.. KAZI NZURI SANA MKUU. MWENYE MACHO NA AONE, MWENYE MASIKIO ASIKIE.

  chiggs, deslam

  ReplyDelete
 16. kaza buti, sisi tupo nyuma kuzuia kufungwa, shambulia tupate magoli mkuu, wakati wa mabadiliko ni sasa, safi sana... Mungu akuzidishie afya na akulinde na waovu..

  ReplyDelete
 17. Hii kumbukumbu ni hazina.

  ReplyDelete
 18. Sitasema KAZI NZURI maana hicho ndicho ninachoata kila niingiapo hapa
  ENDELEA KUIFUNZA JAMII KAKA.
  Siku ya siku TUTAAMKA

  ReplyDelete
 19. Dear my fellow Tanzanians, at least you have seen how the real situation is through these posters.

  Now let's all show that we're tired of these, lets vote for the right candidate, Mr. Slaa has shown and proved to be the right leader for prospering Tanzania. Think about our future, think about our children, think about our nation in the focus of 50years to come.

  Let's Start re-building our nation from where Nyerere ended. VOTE FOR DR. WILBROAD SLAA.

  ReplyDelete
 20. Mungu ameweka uwezo wa kila Mwanadamu kumiliki na Kutawala,lakini uwezo huo unatofautiana kulingana na mtu huyo anavyo mtegemea Mungu.Wengine wanaweza kuongoza familia zao tu na ukiwapa uongozi wa kutawala Mtaa au Kijiji inakuwa ni shida tupu.Mungu kwa sasa anawaangalia Vijana watanzania watafanya Maamuzi gani juu ya Uchaguzi 2010 Octoba.Vijana kumbukeni Mungu hana dini ni wazazi wenu tu wamewaingiza huko ukajikuta ni Mkristo au ni Mwislamu.Hawa wazazi wenu waliopo madarakani ndio wanaoipeleka nchi yenu mtakayorithi kwenye laana.Kama mnataka kurithi utajiri fanyeni maamuzi Magumu sasa na Mungu wenu nyote atawasimamia.Lakini kama mnataka kurithi laana basi acheni kufanya mabadiliko,maisha ni mabadiliko ya kuondoa kile kibovu ulichonacho kichwani na kuingiza kikubwa zaidi kichwani chenye ubora wa viwango.

  ReplyDelete
 21. Kikwete Vs Dr. Slaa ni kama dola ya Zimbabwe Vs dola ya Marekani. Big up kamamnda kwa kutupa kitu cha uhakika.
  Kila anayesoma ajielekeze katika kutuma ujumbe makini huo vijijini tunakotokea ili yu kuiong'oa CCM kabla hawajaiacha nchi taabani zaidi.
  Shime wazalendo wenzangu, tumeachwa na wakati tayari.

  ReplyDelete
 22. Great Great...tusambaze ujumbe kama huu kwa haraka zaidi kwani tupo nyuma ya wakati.

  ReplyDelete
 23. dah kweli hizi ndo harakati zinazoitajika katika nchi kama hikwani hadi kumkomboa mtanzania ambae ni mtumwa wa fikra si kitu kidogo big up kaka...

  ReplyDelete
 24. I love this site, and the guy who post all this i give him full respect!!, this is one of the reasons why most of young people run away from that country!!. but tha thing is most of them people in rural areas dont know anything!!.

  ReplyDelete
 25. Hii uliyofanya mwandishi wa makala haya ni kielelezo tu cha uandishi usiokuwa na usawa na uchambuzi wa kina, hivi unataka kutuonyesha katika miaka 5 iliyopita JK hakuna hata zuri alofanya?, yaana hakuna idadi ya madarasa, meza, viti vilivyoongezeka? hakuna barabara mpya za kiwango cha lami mpya? unatikiwa kama mwandishi makini uonyeshe pande zote mbili za shilingi, hata ccm wenyewe wamekiri kuna maeneo wamefanikiwa na kuna maeneo bado na kwenye ilani yao wameahidi kuyafanyia kazi kipindi kijacho kama watapata ridhaa ya kuongoza tena

  ReplyDelete
 26. Haya ndio maisha halisi ya watanzania wanatuhadaa na mabango yanayoonyesha picha hata za kuwatwisha wanawake ndoo za maji vichwani! Kiongozi bora asingenadiwa na bango kama lile maana linaonyesha uzalilishaji kwa kina mama na ndio hao hao wakipewa kanga na vilemba ndio wanajisahau kaabisa.

  Usanii ni mwingi sana na yote tuna yajua huu ndio wakati wetu wa kufanya mabadiliko ya kweli maana hakika wakati umefika na wakati huo ni sasa! Dawa ni kuwapiga chini na kuweka uongozi mpya na wao pia wakituletea mawenge tunawapga chini.

  Mtoi

  ReplyDelete
 27. Aisee nmenjoy tho inackitisha sana, ka raha 2 amekula ila trh 31 oct kazi ipo..!!!! mpaka kielewek!!!!!

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube