1 Jan 2011



Heri ya Mwaka Mpya.Well,so far hakuna jipya katika mwaka huu ukiondoa mabadiliko kwenye tarakimu 2010,ambapo sasa inasomeka 2011.Kitu pekee kitakachofanya upya wa mwaka huu (na pengine hapo baadaye) ni mabadiliko.Iwe ya mtu binafsi au ya jamii.Na baraka za Mungu,ofkozi

Nimesoma hotuba ya Rais Jakaya Kikwete kuaga mwaka jana na kukaribisha mwaka huu "mpya".Naomba niwe mkweli.Hotuba hiyo imethibitisha kwa mara ya elfu kidogo kuwa Kikwete is out of touch.Najua hadi hapa msomaji mpendwa unaweza kusema "ah ee bwanaee,kweli wewe unamchukia JK.Yani hata alivyoahidi Katiba mpya bado unamlaumu?".Well,simchukii huyu Mkwere bali siridhishwi na udhaifu wake kiuongozi.

Hotuba ya Kikwete jana inatoa picha wa kiongozi wa nchi ya kufikirika.Badala ya kuwa mkweli kwa anawaowaongoza,anarejea usanii wake wa kwenye kampeni za uchaguzi ambapo yayumkinika kusema aliweka historia kwa kutoa rundo la ahadi,ilhali nyingi ya zile alizotoa mwanzo zikiwa hazijatekelezwa.

Kuna bloga mmoja ameandika makala ya kumpongeza JK kwa kuanzisha mchakato wa Katiba mpya.Tatizo la ndugu yangu huyu ni kuweka busara zake kando kila linapokuja suala linalomhusu JK.Anasahau kuwa umuhimu wa Katiba mpya sio matakwa ya Rais,na hasa ikizingatiwa bayana kuwa Katiba mpya si miongoni mwa vipaumbele vyake (if he has any at all).Lakini pia anapuuza ukweli kuwa tamko la jana ni matokeo ya moto unaowaka kwenye jamii kushinikiza jambo hilo muhimu.Sasa hata kiongozi anapofanya kile anachopaswa kufanya-yaani kusikiza matakwa ya jamii- ni sababu ya kiongozi huyo kuingizwa kwenye vitabu vya historia?This is way too low hata kwa magwiji wa kujipendekeza.

Lakini ili uelewe vema mantiki ya post hii,jaribu kusikia baadhi ya kauli za viongozi wa mataifa yenye hali njema zaidi ya Tanzania,Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron,kwa mfano wa karibu na ulio mwafaka.Katika salamu zake za mwaka mpya,Cameron amekuwa mkweli kwa Waingereza na kuwaambia licha ya jitihada za serikali yake ya mseto (wa vyama vya Conservative na Liberal Democrats),mwaka 2011 utakuwa mgumu,hususan kutokana na utekelezaji wa hatua za kubana matumizi.Waziri Mkuu huyo alibainisha kuwa hakuna njia ya mkato ya kukabili mwenendo tete wa uchumi wa Uingereza ( sambamba na kuyumba kwa uchumi wa dunia) bali kufanya kinachostahili sasa ili kuepusha madhara makubwa mbeleni.Pia,Cameron,aliwafahamisha Waingereza kuwa tishio la ugaidi bado lipo juu,na akawaomba Waislam wa nchini hapa kusaidia katika mapambano dhidi ya msimamo mkali wa kidini.

Tofauti na Kikwete ambaye sehemu kubwa ya hotuba yake ilikuwa inatoa picha kuwa Tanzania iko shwari kabisa-kisiasa,kiuchumi,kijamii,nk,mwenzie Cameron hakuumauma maneno bali alifanya kile kinachopaswa kufanywa na kiongozi anayejali ncbi na watu wake.Wafadhili wetu wanakuwa wakweli kwa walipakodi wao,sie wafadhiliwa tunavishana vilemba vya ukoka kuwa mambo si mabaya.

Ukisikia namna Kikwete anavyozungumzia uchumi wa Tanzania,unaweza kudhani nchi yetu iko kwenye ngazi ya developed nations,hatutegemei fadhila za wahisani kutosheleza bajeti yetu na tunamudu kwa ufanisi huduma muhimu kwa umma.Uchumi pekee unaoleta maana kwa Mtanzania wa kawaida sio takwimu,kwa vile baba hawezi kuilisha familia yake kwa takwimu.Hakuna mwenye nyumba atakayemwelewa mpangaji wake kwa takwimu,au muuza duka atakayekuuzia bidhaa kwa takwimu badala ya fedha.Umasikini unazidi kuongezeka miongoni mwa Watanzania lakini hilo halimsumbui Kikwete kwa vile takwimu zinaridhisha.

Hebu angalia alivyozungumzia ishu ya umeme!Ahadi juu ya ahadi kama ilivyokuwa wakati wa kampeni.Lakini kingine cha msingi ni ni ahadi kuwa tatizo la umeme linatarajiwa kumalizwa within miezi 36 kutoka sasa.I wish iwe hivyo,lakini itawezekanaje kuwa hivyo katika hali tuliyonayo sasa ambapo sekta ya nishati ni kitegauchumi cha kuaminika zaidi kwa mafisadi?Je dhamira hiyo ya Kikwete ina baraka kutoka kwa akina Rostam?Je wamemwahidi kuwa hakutakuwa na Richmond na Dowans nyingine mara baada ya kulipwa shilingi bilioni 185 kama zawadi ya kutufisadi?Halafu yule bloga wa kujipendekeza anasema JK atakumbukwa kwa historia njema (kuhusu Katiba)!!!

Na wakati ameweza kutetea ongezeko la bei ya umeme,JK alijifanya hajasikia kuwa kampuni ambayo hadi leo hatujui mmiliki wake-Dowans- italipwa shs bilioni 185 licha ya utapeli na ujambazi waliotufanyia.JK alijifanya hakumbuki kauli ya Mwanasheria wake Mkuu,"Mura" Jaji Werema ( pumzika kwa aibu huko Ukuryani,bosi wako JK kakuumbua),kwamba suala la kuilipa Dowans halina mjadala.Kikwete ameshindwa kuwaambia ukweli Watanzania kuwa bei ya umeme inabidi iongezeke ili kupata fedha za kuwalipa wanaharamu wa Dowans.

Kuna wanaoweza kudai JK asingeweza kuongelea ishu ya kuilipa Dowans kwa vile ni suala la kisheria.Je alipozungumzia uwezekano wa serikali yake kukata rufaa dhidi ya hukumu ya Zombe haikuwa jambo la kisheria?

Ndio maana kichwa cha habari cha post hii kinahoji JK amejulia wapi kuwa Watanzania wanahitaji Katiba mpya ilhali yeye anaonekana kuishi nchi tofauti na wanayoishi walalahoi?Amejuaje kuhusu Katiba lakini ameshindwa kujua kuhusu Dowans?Jibu ni rahisi.He is completely out of touch with reality.Anazungumzia kubana matumizi wakati serikali yake inaendeleza matumizi ya anasa na akina Mkulo wanakodi ndege kwa shs milioni tano kuhudhuria mahafali huku shangingi lake likipelekwa "tupu".Au anajigamba kuhusu kubana matumizi kwa vile the so-called "Mtoto wa Mkulima",Waziri Mkuu,Mizengo Pinda alikataa shangingi (lakini akashindwa kuzuwia shangingi hilo kukabidhiwa mtu mwingine!)

Sijawahi kuongelea suala la Katiba mpya,na leo sintoongelea hilo.Ila kwa wanaoanza kudai kuwa yaani kwa KUAHIDI tu mchakato wa Katiba basi JK ataingia kwenye vitabu vya historia,ni vema wakatambua kuwa JK ni GWIJI LA AHADI.Pia wanapaswa watambue kuwa hii top-bottom model of constutitional reforms inaweza kutuletea kilekile tunacholalamikia kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi: vitu vinavyofanywa kiujanja ujanja kuendeleza maslahi ya makundi flani.Kinachohitajika sio tume ya mchakato wa mabadiliko ya katiba bali tume HURU ya kushughulikia mchakato huo.

4 comments:

  1. Kwa mtazamao wangu mimi nafikiri Kikwete is good at that thing of "tell people what they want to hear" Hii ni kwasababu toka alipoingia madarakani ni mtu wakusema mambo mazuri tu lakini utekelezaji zero. Sasa na hili la katiba naona amesema tu lakini hakumaanisha alilosema: ukizingatia watendaji wake wa sheria walishatoa misimamo tofauti.Kwa kifupi everything kwenye ile hotuba ni uendelezaji wa usanii kama kawaida. Sitashangaa kusikia hotuba zake anasoma tu kile alichoandikiwa na hajafanya proof reading au mchango wowote kwenye kile kilichoandikwa. Maana hilo la umeme kwakweli mmh! lina fanya u-question his thinking capacity.

    ReplyDelete
  2. Huyu ni mzee wa Tume, Hebu tuangalie success level ya tume zote alizowahi kupendekeza ziundwe chini ya utawala wake. Kama hamna success je nini kinatufanya tuamini hii nyingine itakayoundwa?? Hili ni changa la macho tu amkeni mliolala.

    ReplyDelete
  3. KWA KWELI NIMESOMA HIYO HOTUBA, INAKUFANYA UNACHUKIA SANA, KWANINI KIONGOZI WA NCHI ANAKUWA MUONGO HIVI!! KWANINI MTU HATAKI AKUMBUKWE KWA MAZURI? TOKA IKULU WANANCHI WAKO WAKULILIE. HOTUBA IMEJAA UONGO MTAKATIFU. ALIVYO RELAX MWENZETU UTAFIKIRI KILA KITU SORTED HUKO MASHULENI,MAHOSPITALINI, WATOTO OMBAOMBA KILA SEHEMU, MATATIZO YA UMEME, AJIRA,UBABE WA KULIPA LAKI 7 KWA DAMU ILIYOMWAGIKA KIJINGA, UFISADI NA UONGO MKUBWA WA DOWANS... YAANI ANALETA USANII WA KITOTO SANA, INASIKITISHA MNO, KWANINI KIONGOZI KAMA JK AMBAYE AMEISHI NCHI ZA NJE KWA SANA TU ASIWE NA UCHUNGU WA KULETA MAENDELEO HAPA BONGO! NI UMASIKINI KWAMBA NIMEINGIA SASA NILE!! USHAMBA SANA, SHAME ON YOU NA HOTUBA YAKO, IMEKAA KAMA UNAONGEA NA WATOTO WA CHEKECHEA, ULIVYOKUJA JUZI ULISEMA UTATULETEA PIPI, HUJAJANAZO ALAFU UNATUAMBIA TENA NITAKUJA NA PIPI KESHO..TOA UONGO WAKO HAPO NA MUOGOPE MUUMBA WAKO, UNAONGOZA NCHI WEWE ALAFU UNALETA USANII!! NI HATARI, UNAWEZA SABABISHA VITA, WATU WAMECHOSHWA NA MAISHA YA AHADI ZA UONGO, WAKO KWENYE UMASIKINI WA KUTUPWA. INGEKUWA WEWE UNGEKUBALI KUDANGANYWA KAMA KITOTO CHA CHEKECHEA?! NI BORA HATA ASINGEKUWA ANAONGEA KITU, MAANA INAKUFANYA UONE UNA AKILI KULIKO RAISI WAKO, NI KUJISHUSHA SANA. WANANCHI WANATAKA MABADILIKO SIO POROJO POROJO TU. NAJUA KAKA UTATOA HII COMMENT KWANI WEWE NI MZALENDO WA KWELI, LAKINI NASHANGAA GLOB FLANI UNATOA COMMENT HAZITOLEWI! SASA SIJUI MWENZETU ANASHEA NA JK! UJINGA TU, ATATOKA HAPO IKULU UTAACHWA NA MATATIZO YAKO NA KIBLOG CHAKO UNAENDELEA KUTOA AJALI, FOLENI NA MATATIZO YA WATANZANIA, BADALA YA KUACHA WANANCHI WATOE MACHUNGU YAO, NA HUYO JK AONE SISI SIO WAJINGA WA KUDANGANYWA KITOTO HIVYO. TUMECHOKA JAMA

    ReplyDelete
  4. Heri ya mwaka mpya Bwana Chahali!!

    Hivi karibuni nilitembelea mtandaoni kwenye hii link, http://www.youtube.com/watch?v=bixs3LAFM2w&feature=fvw, Nimepata maneno mazuri sana yanamfaha mtu kama JK na viongozi wengine wa Afrika na pia yanakupongeza Juhudi zako Bwana Chahali kutoka kwa mwanamuziki wa Reggae kwa jina Sean Paul kwenye yake ya Trinity...Nanukuu" He doesn't want to look that he is talking about only dirty things happening in the third world countries but Good things never come out from the dirty". Nimemaliza kunukuu.

    Kimsingi Huyu JK anatamka kwamba yeye ataunda kamati kutoka wapi.!!!! kwa hao watu wake ili hawahadae watanzania kwa kuunda kamati yenye mtazamo ule ule wa chama kimoja na tena kuwatengenezea mafisadi nafasi ya kulindwa zaidi.

    Nilitegemea kama anatambua kuwa Tanzania kama nchi siyo mali yake binafsi, atamke kuwa suala hili litapelekwa kwa wananchi ili jamii ya kitanzania hifanye maamuzi ya namna gani ifanyike ili tutengeneze katiba. JK kumbuka katiba ya nchi siyo sawa na barua ya kumposa mke. Katiba ni roho na muhimili wa nchi na wananchi hivyo lazima iwe makini na kushirikisha jamii yote kwa vitendo siyo kwa maneno ya jukwaani tena maneno na ahadi bla bla...!!!!

    Bwana Chahali kamwe haufanyi makosa kumkosoa huyu mbabaishaji wetu. Naona pengine ametumwa na mafisadi kuongelea ili suala la katiba, hivi sasa na kuichukua hii mada ya wapenda maendeleo. Halafu imwone kama mtu anayetaka kweli kutoa ushirikiano kwenye mabadiliko ya katiba.

    Angalia kauli za mawaziri wake na mwanasheria mkuu wa serikali. Hiyo ni ishara tosha kwamba hata hii kauli yake haina ukweli.

    Mimi mtazamo wangu naona JK ametamka hayo ili kupunguza msukumo uliyojitokeza kutoka kwenye jamii hivi karibuni madai ya katiba mpya na siyo kubandika viraka kwenye katiba iliyopo. Kubwa zaidi ni tishio la maandamano na matoke yake.

    Kuhusu huyo mtu anayesifia kila kitu cha JK bila kuwa muwazi hii yote inatokana na njaa na ukosefu wa ubunifu mbinu halali za kupambana maisha kujipatia kipato halali, na pia kushindwa kutambua na kuelewa maana halisi binadamu huru na nchi huru.

    Kifupi huyo Bwana ni mnafiki haujui kuwa JK siyo mkubwa kuliko nchi ya Tanzania.!!!!

    God bless all nationalist such a Mr Chahali.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.