7 Jan 2011

PICHA KWA HISANI YA VYANZO MBALIMBALI MTANDAONI.
INTELIJENSIA YA KUBASHIRI KUWA MAANDAMANO YA AMANI YATAISHIA KUVUNJA AMANI-IPO.INTELIJENSIA YA KUMJUA MMILIKI WA KAGODA HAIPO.INTELIJENSIA YA KUMTAMBULISHA MMILIKI WA DOWANS HAIPO!

BINAFSI NACHUKULIA AMRI YA KIKWETE ILIYOPELEKEA MAUAJI YA WATANZANIA WASIO NA HATIA ILITOKANA NA HASIRA YA YEYE KUTAJWA KUWA NI MMILIKI WA KAMPUNI YA KIJAMBAZI YA DOWANS.

LAKINI KWA VILE KIKWETE-NA DOLA YAKE ANAYOJIVUNIA KUWADHIBITI WANAOMTAKA AWAJIBIKE- AMEINGILIA JUKUMU LA MWENYEZI MUNGU KWA KUKATISHA UHAI WA WATANZANIA WASIO NA HATIA HUKO ARUSHA (HATUWEZI KUJUA KWA HAKIKA NI WANGAPI WAMEUAWA KWA VILE WATOA TAARIFA NI POLISI HAOHAO WALIOUA) BASI AMIN NAWAAMBIA MUNGU MTOA HAKI YA KWELI ATATENDA HAKI.HAKUNA MAHAKAMA YA TANZANIA INAYOWEZA KUMHUKUMU KIKWETE AU SAID MWEMA LAKINI TAYARI MAHAKAMA YA UMMA (COURT OF PUBLIC OPINION) IMESHATOA HUKUMU,NA TUNACHUSUBIRI NI HUKUMU KUBWA ZAIDI KUTOKA KWA MUUMBA WETU (MAANA KIKWETE KALEWA MADARAKA MPAKA KUINGILIA KAZI ZA MUNGU ALIYEMUUMBA).

KWA WAZALENDO WALIOUAWA-"KOSA" LAO LIKIWA KUTUMIA HAKI YAO YA KIKATIBA KUANDAMANA KWA AMANI-DAMU YENU HAIJAMWAGIKA BURE.KIKWETE NA WAPAMBE WAKE WATAJITAHIDI KUWAPACHIKA KILA MAJINA ILI KUHALALISHA KUWA MLISTAHILI KUUAWA.HATUWEZI KUMZUWIA KWA SASA.LAKINI KAMA DOLA ZA KIKOMUNISTI ZA ULAYA YA MASHARIKI ZILISAMBARATIKA LICHA YA MATUMIZI MAKUBWA YA NGUVU ZA DOLA,BASI IPO SIKU UBABE,UNYAMA,UUAJI NA USHENZI WA CCM UTAFIKA KIKOMO.

TUNAKUOMBA MUNGU MWENYE HURUMA NA UPENDO UZIREHEMU ROHO ZA MASHUJAA WETU WALIONYANG'ANYWA UHAI NA SERIKALI YA KIKWETE,NA TUNAKUOMBA UTOE ADHABU KALI KWA WAHUSIKA,HUSUSAN RAIS JAKAYA KIKWETE NA VYOMBO VYAKE VYA DOLA.KWA MUNGU YOTE YANAWEZEKANA. 

10 comments:

 1. Inauma sana kwa Watanzania wote. Hili ni janga na inaonesha wazi makucha yaliyofichama ndani ya CCM, Raisi wa nchi hajasikitika hata kidogo, hata salam za rambirambi hajatoa, Watanzania tujifunze kutokana na makosa tunayofanya wakati wa uchaguzi.

  ReplyDelete
 2. Naungana mkono nawe, nguvu kama hizi zingetumika kurudisha mabilioni yanayochukuliwa kila siku sio kuua raia wasio na hatia. Hivi kweli Mwema na Kikwete watu kukusanyika bila kibali wanapewa hukumu ya kifo??

  ReplyDelete
 3. sijui kama kweli ila nimesikia mkutano uliruhusiwa ila maandamano yalikatazwa siku moja kabla, sasa kama waliruhusu mkutano tuu unategemea kitu gani kwa sababu kwenye mkutano kuna ambatana na mabango,kushereheka, na mkusanyiko wa watu, je walitegemea watu watoke mmoja mmoja tena kibubu bubu hadi kwenye mkutano? tena hiyo nayo ingetakiwa kueleza watu kuwa jamani mje kimya tena mmoja mmoja. na ingeletea tena polisi kusema kuna intelligensia watu wanapanga mambo mabaya, inaelekea polisi walivyoona ni maandamano ya amani wakaamua kuanzisha fujo kwa kuwakamata viongozi wakijua watu watakwenda kuwakomboa na ndio mambo yalipoanza, mbona polisi hawajawakamata wabunge wa ccm waliokusanyika sehemu mbali mbali na wananchi ili kupongezwa kwa ushindi wao. binafsi siichukii ccm ila nachukia mfumo wa rushwa kila mahali hadi hospitali, uwanja wa ndege unaposafiri, unyanyasaji wa wanafunzi kupanda daladala, barabara mbovu, huduma maofisini duni,elimu bora kwa matajiri, n.k watu wakilalamika unaambiwa mpinzani tukimbilie wapi wanyonge???

  ReplyDelete
 4. Very sad. Nimemshangaa Makamba badala ya kusikitishwa na vifo yeye anasikitishwa na mali za CCM zilizoharibiwa. Nafikiri kwa mtu mwenye akili ya kawaida tu anaweza kujua jinsi Makamba na JK wanavyojali mali kuliko uhai wa binadamu. That being said wamekusudia kulinda ufisadi at any cost even by shedding blood.

  ReplyDelete
 5. taarifa zinasema polisi wamesema hawajakosea eti kuzuia maandamano wanadai eti wasingezuia watu wengi zaidi wangekufa, wanasahau kuwa chadema wameshawai fanya maandamano makubwa zaidi wakati wa kampeni na hakuna hata paka aliyekufa, je washitakiwe wapi waliotoa amri ya silaha za moto kutumika kwenye maandamano ya amani hata kama hakukuwa na kibali, kibali wasingetoa hata hivyo, walaaniwe kwa kufanya familia ziwe yatima arusha

  ReplyDelete
 6. ewe ulieshika bastola,rungu ,jiwe au chochote ulichotumia kumwaga damu na kuua raia wema,damu zao na ziwe kaa la moto kwako siku zote za maisha yako.

  ReplyDelete
 7. hiyo picha nyingine polisi kama watano wamenyanyua virungu kumpiga mtu mmoja mbona inatisha, imekaa kama majambazi waliovaa sare za polisi, polisi watano mnashindwa kumkamata mtu mmoja kistaarabu hadi wote mmpige virungu, shame on you mtakufa vifo vya ajabu

  ReplyDelete
 8. Jamani hakuna watu wa kujitoa mhanga tukaondokana na hiki kilaza akili mgando na tuanze upya!!!!!

  Tunawaombea mashujaa Mwenyezi Mungu awapokee katika ufalme wake na siku itafika tutakapoinua mnara wa kuwakumbuka - Amen

  ReplyDelete
 9. Kwanza ni kitu cha ajabu kuwaruhusu watu waandamane ila masaa machache kabla ya siku kufika polisi wanakataza maandamano, wangewaarifu saangapi wanachama, na hata kama wangearifiwa wanachama gafla kuwa hakuna maandamano je wangepitia wapi ili wafike uwanjani walikoandalia maandamano,wangepaa juu au ilikuwa halali kwao kupitia bara barani hadi sehemu yao ya mkutano? Haki ukowapi Tanzania? kilamahali pametawaliwa na dhuluma tu,utashitaki wapi wakati secta zote zipo chini ya mtoa tamko la mwisho? Inauma, inauma inauma.Sasa hivi kila kitu bei juu hapa Dar, bado machungu ya hali ngumu ya maisha haijapoa,tumepata tumaini labda Januari hii mambo yangekuwa mazuri wapi; Jamani wenzetu mlioko nje ya nchi hongereni maana Tanzania ya leo ni kilio tupu.Tunatamani kuhamia porini tukaishi na wanyama labda itakuwa nafuu.

  ReplyDelete
 10. JAMANI WAKATI WA KUJITOA MHANGA UMEFIKA, TUSIPOMALIZA HAYA KUTATAWALIWA NA HAWA WAUWAJI MPAKA VITUKUU VYETU WATAKUBWA NA UFISADI, KAMA ALIVYOSEMA MDAU, TUTANYANYUA MNARA KWA WANAMAPINDUZI WALIOPOTEZA UHAI WAO. SASA KASI IPAMBE MOTO JAMA, MUDA WA KULALA UMEKWISHA, TUSAMBAZE HABARI ZIONGELEWE KWENYE MABUNGE YOTE DUNIANI, TUWAUMBUE TUWATOE HADHARANI, NI MAKUPE HAYA, BILA HATA AIBU MNAWATUMA WATOTO WENU "ETI WANALAANI MAANAMANO YA CHADEMA!! HEBU TOKENI HAPO KABISA, MWISHO WENU UKO KARIBU. WANANCHI WAMEFIKA MWISHO.

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube