14 Apr 2011Kwa mujibu wa mtandao wa Jamii Forums

Rostam, Bashe watangaza vita na JK, wamuita naye fisadi
Katika kile kinachoonekana kuwa sasa wanatangaza vita, gazeti la Mtanzania linalomilikiwa na Rostam Aziz na kusimamiwa na Hussein Bashe limemchimba JK kwa kuandika leo kwamba Kikwete naye fisadi wakinukuu List of Shame iliyotolewa na Chadema Mwembe Yanga, huku wakinukuu tuhuma zotte ambazo zilielekezwa kwa JK na huku wakijifanya kuwarushia mpira Nape na Chiligati kuwa walisema mafisadi wote CCM wajiuzulu akiwamo JK.

JK, Mukama, Chiligati na Nape walizungumza wakirejea vikao vya CCM na si LIST of Shame na kama walitambua hilo wangesema mapema si baada ya kufukuzwa.

Katika vikao vya CCM List of Shame ya Chadema haijajadiliwa bali walijadili Richmond, Dowans, Kagoda na Rada na waliwataja kwa majina Lowassa, Rostam na Chenge. Hii ni sawa na mwizi kukamatwa na kusema "tuliiba na mwenzangu mbona hakamatwi?" Maana yake anakiri kuwa ni mwizi.0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube