15 Apr 2011


Ndugu wa Bwana Lilah Hussein ambaye anadaiwa kuchomwa moto na walinzi na Meneja/Mmiliki wa Hotel ya South Beach wameomba wapatiwe mwanga wa kisheria jinsi ya kudai haki kwa ndugu yao aliyechomwa moto.

Akiongea nami mmoja wa jamaa wa Lilah amesema kuwa mpaka sasa wako gizani hawajui pakuanzia kutokana na kutojua mambo ya kisheria.

Labda kwa anayeweza kutoa msaada au muongozo wowote wa kisheria anaweza kuwasiliana na mmoja wa ndugu hao kupitia 0655362785

Kwa sasa Lilah bado amelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

2 comments:

  1. Mkuu,inabidi utoe ilani kwa watizamaji wako, wengine wanaweza kuwa na moyo mdogo kuitizama hii picha. Binafsi nimeshindwa kabisa kuitizama.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli mkuu hapo nilipitiwa.Kwa hakika inatisha

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.