17 Jun 2011Leo imetimia miaka miwili kamili tokea ututoke mama yetu mpendwa, Magreth Mabula-Senga. Haupo nasi kimwili baada ya kukuzika kule makaburini Yombo, Dar es Salaam, lakini kiroho mama, upo nasi siku zote. 

Mama, tunakukumbuka kila saa, tunakumbuka upole wako, busara zako, uvumilivu wako, lakini zaidi upendo wako wa pekee ambao umefanya tuweze kufika hapa tulipofika. Mama ulitaka tuishi maisha ya mafanikio, maisha ya upendo kama uliokuwa nao, maisha ya kusaidiana. Tunakumbuka mama kuna kipindi ulilazimika hata kujinyima kwa ajili yetu sisi! Kuna kipindi mama ulitoa machozi ulipoona mambo kwa upande wetu hayaendi sawa. Kwa hakika mama ulitupenda sana sisi wanao.

Mama, tulipenda uendelee kuwepo. Ndio maana hata ulipopatwa na maradhi na kulazwa hospitali, tulikuwa na wewe karibu, tukihangaika na kukuombea Mungu akuponye na kuendelea kukupa pumzi. Lakini haikuwa hivyo, kwa mapenzi yake muumba, mama ulituacha kimwili. Ilikuwa ni pigo kubwa sana kwetu na hatukuwa na namna au uwezo wa kulizuia hili. Tulikubali na kuhuzunika sana.
Tunakuahidi mama yetu, tutazidi kuyaishi yale ambayo uliyapenda huku tukiomba kila wakati Mwenyezi Mungu azidi kutukarimu moyo kama uliokuwa nao. Tunazidi kukuombea mama yetu, roho yako istarehe kwa amani. Tunaomba na wewe utuombee, tuweze kupata baraka na mafanikio leo na siku zote zijazo. 


MAMA TUNAKUPENDA SANA. NI MIAKA MIWILI SASA LAKINI BADO UPO NASIPOLE SANA NDUGU YANGU MWANASOSHOLOJIA.SIE TULIMPENDA MAMA LAKINI BWANA ALIMPENDA ZAIDI,NA KWA VILE NI MWENYE UPENDO BASI ANAMPATIA PUMZIKO NA MWANGA WA MILELE.NAUNGANA NA WEWE BINAFSI NA FAMILIA YAKO KATIKA MAOMBOLEZO HAYA.

2 comments:

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube