6 Aug 2011


Nimekutana nayo huko Jamii Forums.Habari hii imenikumbusha mbinu iliyotumiwa na utawala wa mkoloni kuendeleza utawala wake dhalimu.Wakoloni walitugawanya kwa misingi mbalimbali,hususan rangi,na kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kuchelewesha jithada za ukombozi wetu.Lakini kama zilivyo mbinu nyingine za ujanja ujanja,mbinu hiyo haikuweza kudumu milele.Kwa hakika hakuna mbinu yoyote inayoweza kuzuwia kiu ya mwanadamu kuleta mabadiliko bora kwake.

Kinachonisikitisha katika habari hii ni namna baadhi ya wanablogu wenzetu wanavyokubali kuuza utu wao (na kuwasaliti mamilioni ya walalahoi) kwa ajili tu ya maslahi binafsi.Wosia wangu kwao ni mwepesi tu: waangalie namna CCM ilivyowatumia wanahabari katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,na mara baada ya Wanamtandao kufanikiwa kumwingiza Kikwete Ikulu wakawatosa wengi wa wanahabari hao.Kuna wanahabari walibembelezwa kuacha vibarua vyao nje ya nchi,wakawatumikia wanamtandao na baada ya umuhimu wao kwisha,wakatoswa.Ni vema mabloga walioingia mkenge huu wakatambua kuwa nafasi yao walionayo ni mhimili wa nne wa dola.Lakini la muhimu zaidi,wakae wakielewa kuwa,ashakum si matusi watatumika kama kondomu: MUHIMU SANA KABLA NA WAKATI WA TENDO LA NDOA LAKINI HUONEKANA UCHAFU USIOVUMILIKA BAADA YA TENDO HILO.

You have been warned.

Soma habari husika hapa chini


CCM yaanzisha Mtandao wa Friendly Media to CCM

Wana Jf

Nimesoma habari ambayo imenistua na imenibidi niongee na Mhariri wa Gazeti la Mtanzani Ndg Jacton Manyerere na amenithibitishia kuwa habari aliyoandika ni ya uhakika.

Idara ya Uenezi na Itikadi ya CCM ambayo ipo Chini ya Ndg Nape imeanzisha Mtandao wa Vyombo vya Habari na wana Habari Rafiki na Bloggers na amekuwa akikutana nao Mara kwa Mara.

Kutokana Taarifa za Gazeti la Mtanzania (Media House ambao si Rafiki na CCM kwa Sasa), media ambazo hazitahudhuria ktk mkutano wa Tar 13 na 14 mwezi huu utakaofanyika Morogoro ni Mwananchi Communication, New Habari, Hali Halisi na Free Media. Vyombo hivi si Rafiki wa CCM.

Na Bwana Jacton ansema doc ya FCCM inaonyesha uwepo wa Mpango Mkakati wa Kuanzisha FORUM itakayoitwa KWETUFORUM na pia utaanzishwa mpango halisi wa kuimaliza Jamii Forums.

Pamoja na mpango huu awali walikua wakutane Dodoma wakati wa kamati kuu na mnamo mwezi wa Tano Nape alifanya kikao makao makuu ya CCM na akakutana Bloggers na kuwaahidi kuwasaidia lakini waisaidie CCM ktk Mkutano huo alikuwepo Blogger mmoja wa Jinsia ya Kike... kutokana na mahudhurio ya kikao hicho.

Kilichonishangaza ni baada ya kusoma Agenda za Mkutano ktk Gazeti la Mtanzania leo nimeshangaa katibu wa mpango huu ni dada ambaye sisi hapa Nipashe alikuwa haheshimiki na alisimamishwa kazi.

Binafsi hii ninailaani kwakua inaleta Taswira Mbaya na ninatarajia kuona Editors Forum wanalifanyia kazi kama CCM inatugawa wana Habari ktk Makundi ya Rafiki na Adui ni jambo baya kufanywa na chama kikongwe kama Hiki. Nadhani huyu dogo Nape amechanganyikiwa kabisa.

Nimeona niilete hapa Jamvini Tulijadili.

Story ipo ukurasa wa kwanza ktk Gazeti la Mtanzania na inaendelea ukurusa wa nane

CHANZO: Jamii Forums

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube