9 Aug 2011Kwa mujibu wa tovuti  ya Tanzagiza

Maandamano Kumpinga “Baba Ridhiwani” Jijini Washington DC, USA 
Wa Tanzagiza wanaoishi USA waandaa maandamano kumpinga “Baba Ridhiwani”, Hii ni sehemu ya maandalizi hayo kama yalivyoandikwa na ELIAKIM MALLYA.Kutokana na kuchoka na hali ngumu inayoendelea hapa Tanzania, ndugu zatu wanaoishi USA wameandaa maandamano ambayo yatakuwa ya amani kupinga utawala mbovu wa “Baba Ridhiwani” hasa baada ya kushindwa kuwachukulia hatua mafisadi hapa nchi. 
Tunaandaa maandamano ya amani jijini Washington DC Rais Kikwete “Baba Ridhiwani” atakapowasili kwenye kikao cha DICOTA 2011. Tayari watu 150 wamekubali kushiriki kwenye maandamano hayo. Tunataka watu wengi zaidi kujitokeza. Hii ni kumshinikiza huyu fisadi papa na mzururaji kushugulikia matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida. Maandamano yetu yatahitimishwa na kupokelewa na viongozikutoka United States Department. Tayari tumetuma maombi kupinga misaada marekani inayopa Tanzania, kwani hayasaidii Jamii bali Kikwete na genge lake la majambazi. 
Wote mnakaribishwa karibishwa. Maandamano ya Amani yanaruhusiwa marekani ilimradi mtu hajavunja sheria nchini. Ukiwa na makaratasi yako, njoo tulikomboe taifa letu. Ukombozi wa TANZANIA upo mikononi mwetu. Mabango yanachapishwa tarehe 24, Tunaomba mawazo tofauti kuhusu ujumbe tutakaobeba kwenye mabango yetu. Tumechoka na Kikwete, dawa nikuanza maandamano.Tupo tayari kufa sasa. Tunisia iliokolewa na watu tu kama sisi, tukifa bahati mbaya vizazi vijavyo vitafaidi. Tafadhali sambaza ujumbe. Tutatoa tamko rasmi ya maandalizi tarehe 20 mwezi huu. Ukitaka kushiriki tuma barua pepe [email protected] 
Raia wa kawaida anayo haki ya kumfanya Kikwete Anyimwe VISA. Kwa Kupinga Ujio wa Kikwete, au yeye kunyimwa VISA tumeni emails nyingi iwezekanavyo kwenda East African Affairs Bureau. Email Adress [email protected]

Hatua kama hizi zinaweza kusaidia kumfanya Rais Kikwete apunguze kuzurura kutoka nchi moja hadi nyingine kana kwamba hana kazi ya kufanya nchini kwake.Rais gani ambaye takriban kila mwezi lazima asafiri nje ya nchi?Ameshazuru Marekani mara kadhaa lakini bado hajatosheka.

Pengine unaweza kumtetea kwa kusema "kwani safari zake zina ubaya gani?".Kila msafara wa Rais nje ya nchi unagharimu mamilioni ya shilingi kwa ajili ya gharama za usafiri,malazi,posho na vikorombwezo vingine.

Visingizio vingine vya Kikwete kuzurura nje ya nchi havina mashiko hata chembe.Kwani Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe akimwakilisha Kikwete kwenye shughuli hiyo ya DACOTA kitapungua nini?Actually,Balozi wetu nchini Marekani anaweza kabisa kuwa mgeni rasmi na shughuli hiyo ikafana pasipo matatizo.Kwa mantiki hii,nawasihi ndugu zetu wa DACOTA kufikiria upya uamuzi wao wa kumwalika Kikwete.Tangulizeni maslahi ya nchi (kwa kuokoa gharama zitakasosababishwa na ziara nyingine ya Kikwete nchini Marekani) in front of maslahi ya jumuiya yenu.

KULIKONI UGHAIBUNI inaunga kwa dhati harakati hizi za kizalendo za kudai kilicho bora kwa nchi yetu.Kila Mtanzania mwenye uchungu anapaswa kuunga mkono harakati hizi kwa matarajio kuwa hatimaye Kikwete atapatwa na aibu ya kuzurura kila kukicha.

3 comments:

 1. Nashauri watanzania wote tujitokeze kwa wingi kwenye maandamano yetu ya amani, hiki ni haki yetu katika kupinga utawala huu usiyejali wananchi; kama una rafiki, ndugu, co-workers wenye mapenzi mema na TZ pia tunawaalika kuja kutuunga mkono. Ni lazima tuonyeshe kwa vitendo sasa tumechoka, nafikiri tumeshapoteza miaka karibia sita bila kupiga hatua yeyote chini ya JK, we have to do something now!!!

  ReplyDelete
 2. naona dalili za kukomaa kwa udini.

  Mi naanzisha kikundi kitakacho andamana kupinga maandamano haya ya kusingizia.

  ReplyDelete
 3. kweli huyu mtu ni zonto.nchi yetu haina dira tena lakini kwake dira inamdirect kuzurura na kulala angani kama popo.Mgomo ni lazima,hasituwe States huyu zonto/popo.

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube