6 Sept 2011


Kama unafuatilia blogu hii kwa kina basi utakuwa unatambua kuwa licha ya kuelemea zaidi kwenye masuala ya siasa,ninapenda pia muziki hasa katika kusaidia kuwatangaza Watanzania wenzetu wenye vipaji.

Na kama wewe ni mfuatiliaji mzuri wa matangazo ya ujio wa wasanii wetu kuja huku nje kuwa mara kadhaa matangazo hayo yameishia kuwa matangazo tu pasipo shoo zinazoahidiwa ku-materialise.Juzi juzi kulikuwa na matangazo ya shoo flani lakini ikayeyuka.

Ili kupata undani wa suala hili,nilizungumza na rafiki yangu ambaye ni msanii maarufu kabisa huko nyumbani,Hamis Mwinjuma au maarufu kama MwanaFA.Nilianza kwa kumuuliza mtizamo wake kuhusu utendaji kazi wa mapromota wa huko nyumbani na hawa walio nje (naomba ieleweke kuwa napozungumzia mapromota walio nje ninamaanisha Watanzania wanaojishughulisha na music promotion nje ya nchi yetu).


MwanaFA anaeleza kuwa kwa sasa utendaji kazi wa mapromota wengi wa huko nyumbani unaridhisha,a na anachangia improvement hiyo kwa jitihada za wasanii wenyewe kuwabana mapromota hao ili wasilete ubabaishaji.Anasema (namnukuu), "Kwa sasa mapromota nchini wamenyooka,wana nafuu sana,nadhani tume-deal nao kisawasawa wamenyooka,japokuwa lazima kutakuwa na mikasa ya hapa na pale."


Msanii huyo aliweka bayana kuwa mapromota wengi wa Kitanzania nje ya nchi bado wapo nyuma kidogo tofauti na ambavyo ingetarajiwa kwa vile wanaishi katika "dunia ya kwanza." MwanaFA anaeleza kuwa uwepo wa mapromota hao nje ya nchi unatarajiwa kuwafanya wawe na uelewa wa kutosha kuhusu music industry na suala la promotion za kimataifa.

"Angalau uki-deal na mapromota wa Kikenya ,wana respect (heshima) na wamenyooka already (tayari),wanajua kazi yao  na mazingira ya msanii anatakiwa kufanya kazi iende smooth," anasema MwanaFA katika mawasiliano yetu tuliyofanya kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Msanii huyo anadhani chanzo cha tatizo kinaweza kuwa kwenye hisia kuwa mara nyingi mapromota wa Kitanzania wanaojaribu kuandaa ziara za wasanii wa nyumbani ni watu 'local',sio mapromota wa kweli na ni wadogo mno, "kwahiyo mapindisho pindisho ni mengi pia."


Binafsi naafikiana na MwanaFA.Nadhani tatizo la mapromota wababaishaji linaweza kuchangiwa pia na maandalizi hafifu na ya muda mfupi.Wengi wao wanategemea mapato ya mlangoni aidha kuwalipa wasanii walioalikwa au kufidia gharama walizoingia kuwaleta na/au kuwalipa wasanii husika.Tatizo linakuja pale maandalizi duni yanapopelekea watu wachache kujitkeza kwenye shoo husika.

Mapromota wengi wanaojua kazi yao huanza maandalizi ya ziara ya msanii miezi kadhaa kabla ya shoo.Maandalizi ya muda mrefu yanawezesha matangazo kuhusu ziara ya msanii husika kuwafikia watu wengi zaidi,hasa kwa vile maisha ya wengihapa pia yanahitaji mipango ya muda mrefu.Prmota anapotangaza ujio ya msanii wiki mbili kabla ya tukio anaweza kupelekea watu wengi kukosa nafasi ya kuhudhuria shoo husika.

Lakini wasanii wetu wa huko nyumbani wanaweza kukabiliana na mapromota wababaishaji kwa kuandaa shoo hizo wao wenyewe kwa kushirikiana na wadau mbalimbali waliopo nje ya nchi.Kwa lugha nyingine,wasanii wanakuwa kama wanaajiri watu wa kufanikisha shoo hizo ambao malipo yao yatategemea ufanisi wa shoo husika.Lakini kubwa zaidi ni kwa wasanii wetu kujenga mahusiano na makampuni ya promsheni badala ya watu binafsi ambao wanaganga njaa kwa migongo ya wenye vipaji.Katika hili,wasanii wanaweza kuwatumia wadau mbalimbali kuwasaidia kufanya research ya makampuni yenye uwezo wa kufanikisha ziara ya msanii.


Blogu hii inamshukuru MwanaFA kwa mchango wake wa mawazo.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube