1 Feb 2012


Moja ya mambo ambayo ninajitahidi sana kuepukana nayo ni malumbano.Hata hivyo,kwa vile kila binadamu ana mtizamo wake na sote tuna uwezo wa akili unaotofautiana,kuna nyakati nalazimika kuingia kwenye malumbano hususan unapotokea upotoshaji wa makusudi dhidi yangu au kazi yangu.

Jana niliweka makala moja fupi yenye kichwa cha habari "EXCLUSIVE TO KULIKONI UGHAIBUNI: Rais Kikwete Azungumzia Kauli ya Pinda Kuhusu Posho za Wabunge." Katika makala hiyo niliambatanisha picha za mazungumzo (yasiyo rasmi) kati yangu na Rais Kikwete kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Sasa jamaa mmoja huko Twitter anayetumia 'handle' ya @majaliwa68 ameamua kushikia bangu makala hiyo,hususan matumizi ya neno 'Exclusive.' Alianza kwa kuandika 


Sasa sijui tatizo la ndugu yangu huyu lilikuwa nini hadi hapo.Lakini ukidhani kuwa aliishia hapo,subiri usome hukumu yake zaidi kuhusu makala hiyo,kama picha zifuatazo zinavyoonyesha (pamoja na majibu yangu)



Sijui kama muungwana huyu anajua lolote kuhusu uandishi,uwe ni wa makala au wa kuandika kwa minajili ya kujifurahisha tu.Ninaandika hivyo kwa sababu laiti angejihangaisha kutafuta maana ya habari ambayo ni 'Exclusive' angemaizi kuwa ni "habari ambayo awali imetolewa kwa chapisho moja tu." Ninaamini nilikuwa na kila sababu ya kuiita habari hiyo 'Exclusive' kwa sababu chanzo chake kilikuwa mazungumzo yangu (yasiyo rasmi na Rais kwenye Twitter.Lakini kwenye elimu ya maneno (Semantics), 'Exclusive' pia inamaanisha "kwa ajili ya mtu/kundi au kitu/vitu fulani tu,pasipo kuwa kimefanywa na watu mtu mwingine au kundi jingine/kitu kingine/vitu vingine."

Kwa upande mmoja,kama mwandishi niliona mazungumzo hayo yasiyo rasmi na Rais kuhusu jambo linalotawala akilini mwa Watanzania wengi (kauli ya Pinda kuwa Rais ameridhia ongezeko la posho za wabunge lakini Rais kupitia Ikulu amekanusha hilo) ni habari yenye umuhimu wa kipekee (na katika Semantics,upekee pia ni exclusive kwa Kiingereza).

Kwa upande mwingine,habari hiyo ilikuwa maalum kwa wasomaji wa blogu hii na ndio maana kichwa cha habari kilikuwa "EXCLUSIVE TO KULIKONI UGHAIBUNI..." Kwa kuwajali na kuwathamini wasomaji wa blogu hii niliona habari hiyo inaweza kuwa yenye interest kwao,hasa ikizingatiwa si kila aliyepo Twitter anadiriki kumuuliza Rais maswali mbalimbali (na si kila anayeuliza anajibiwa).Sasa sijui ndugu yangu @majaliwa68-ambaye ninaamini si mosmaji wa blogu hii-alikerwa na nini baada ya mie kufanya jitihada hizo za kuwapatia wasomaji wa blogu hii kile ambacho laiti kingekuwa kwenye vyombo vya habari 'conventional' kingeitwa SCOOP.

Ndio.Hiyo ni mithili ya Scoop kwani Rais kutolea ufafanuzi kukinzana kwa msimamo wake na Waziri Mkuu wake si jambo dogo.Na habari husika haikubeba 'tweets' zangu na Rais tu bali nilijaribu kuwasilisha 'background' ya tukio zima-kuanzia habari iliyochapishwa na gazeti la Mwananchi na tamko la Ikulu.

Kabla sijaendelea zaidi,naomba niwasilishe shutuma zaidi kutoka kwa Ndugu @majaliwa68


Sasa sijui kama 'EXCLUSIVE' maana yake ni "kuongea na mtu kwa kina" neno la Kiingereza 'INDEPTH' litakuwa na maana gani!Na sijui by "kuongea kwa kina" Ndugu @majaliwa68 alitaka niandike makala ndefu kama thesis ya PhD au alitamani iwe na maneno mengi kama makala zangu kwenye jarida la Raia Mwema!

Hakujihangaisha kutambua kuwa lengo la makala yangu halikuwa kutoa hukumu,kukosoa,kurekebisha au kuchangia 'tweets' za Rais.Nilichofanya ni kuwasilisha kauli zake kama zilivyo (na nilifanya hivyo kwa kutumia picha ili isionekane nimepandikiza maneno yangu mdomoni mwa kiongozi mkuu wa nchi.)

Bwana @majaliwa68 akaendelea na 'busara' zake kama ifuatavyo:

Well,ameshasema hapo juu kwamba kwa uelewa wake, 'EXCLUSIVE' ni 'kuongea kwa kina.' Ukimuuliza 'kina' ni urefu wa kiasi gani sidhani kama atakuwa na jibu la maana.

Akazidi kuchambua


Sijui amehesabu mara ngapi kuona kila 'tweet' ya Rais Kikwete imewekwa bloguni hapa kama 'EXCLUSIVE'!!!Halafu,ni upuuzi wa hali ya juu kudai "kila aliyejibiwa na Rais wakimbilie exclusiveness." Ni upuuzi kwa sababu,kwanza,si kila anayejibiwa na Rais ni mwandishi au bloga,na pili,suala la kuandika au kutoandika ni uamuzi wa mtu binafsi.Lakini pengine hoja ya msingi zaidi ni kwamba mtu ataandika vipi kama HWEZI KUANDIKA?Ninasema hivyo kwa sababu kuna wanaodhani uandishi ni suala la kukurupuka tu.Hii ni fani na ina utaalamu wake.Na licha ya kuwa fani yenye utaalamu wake,si kila anayeweza kuandika atamudu kuandika kitu cha msingi.Kwa lugha nyingine,uandishi ni kipaji kwani japo takriban kila anayejua A,B,C...Z  anaweza kuandika lakini kuandika makala yenye hoja za msingi ni kunahitaji zaidi ya uwezo wa kuandika tu.

Hakuishia hapo,akaendelea

Ndio maana nilisema huyu mtu si msomaji wa blogu hii na wala hana idea yoyote kuhusu uandishi.Kadhalika,nadhani Bwana @majaliwa68 bado ana mtizamo mithili ya ule wa Zama za Mawe (Stone Age) ambapo 'kuzungumza' lazima iwe 'mdomo kwa mdomo.' Yaani kwake,uki-tweet chat na mtu au ukiibua mjadala huko Facebook basi huko sio kuzungumza.Kwa faida yake ninapenda kumfundisha kuwa chanzo cha habari kinaweza kuwa chochote kile alimradi kinaaminika na habari husika ni ya kweli.Sasa sijui mtu huyu alitaka mpaka Rais aongee nami kwa simu au ana kwa ana ndipo niwe na haki ya kuandika "Rais amezungumza..." Jamani fani nyingine si zenu na ni vema kuwaachia wanaojaribu kuzimudu au wanaozimudu kabisa.

Kwa leo amemalizia na 'tweet'  ifuatayo

 Mdau Kelvin Manaseh (@kmanaseh) akachangia hoja hii


Nami nimehitimisha mjadala kwa 'tweets zifuatazo




Kama nilivyotanabaisha hapo mwanzo,sipendelea malumbano lakini nimelazimika kukabiliana na upotoshaji wa Bwana @majaliwa68 ambao kimsingi ninaamini ni matokeo ya kukurupukia jambo asilolielewa.Hajui 'EXCLUSIVE TO...' inamaanisha nini,na kwa uelewa wake fyongo,mazungumzo yanayotokana na vyombo vipya vya mawasiliano kama Twitter hayana sifa ya kuitwa mazungumzo.

Hizi ni baadhi ya changamoto tunazokumbana nazo mabloga na wengineo tulioamua kutumia muda wetu kuuhudumia umma kwa njia ya uandishi.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.