1 Mar 2012

Wazee wa iliyokuwa Jumuia ya Afrika Mashariki wakiwa wamekaaa katikati ya jiji la Dar es Salaam wakijadili malipo yao yaliyocheleweshwa na serikali hadi leo.…

Nimekutana na picha hiyo hapo juu kwenye mtandao wa Global Publishers.Kwa kweli imenisikitisha sana kuona wazee wetu waliotumikia taifa letu kwa uadilifu wakihangaishwa miaka nenda miaka rudi kupewa mafao yao ya utumishi katika iliyokuwa Jumuiya ya Nchi za Afrika Mashariki.

Hazipiti wiki kadhaa kabla ya kusikia Rais wetu yuko kiguu na njie kwenda nje ya nchi huku akiambatana na msururu wa watu kwenye msafara.Watendaji wengine wa serikali wanatumia magari ya thamani kubwa huku ofisi zao zikisheheni samani kutoka ng'ambo.Matumizi ya viongozi wetu hayaendani kabisa na umasikini wetu.Mabilioni yalitapanywa mwezi Disemba mwaka jana katika maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.Hivi fedha hizi zisingeweza kumaliza adha inayowakabili wazee wetu hawa?

Jamii inayopuuza wanyonge (kwa mfano wazee hawa) ni kama inasaka ugomvi usio wa lazima na Muumba.Kosa la wazee hawa ni lipi hadi wahangaishwe kiasi hiki?Chonde chonde viongozi wetu-hususan Rais Kikwete-waoneeni huruma wazee wetu hawa.Wanachodai sio posho za vikao kama za wabunge bali ni jasho lao halali.Wenzao wa Uganda na Kenya walishalipwa stahili zao zote.Kama wao waliweza kwanini sie tushindwe?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube