JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALI
ASILI NA UTALII

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI – (PRESS RELEASE) ILIYOTOLEWA
NA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII, MHE. BALOZI KHAMIS .S. KAGASHEKI LIWALE
TAREHE 8/8/2012
NDUGU
WAANDISHI WA VYOMBO VYA HABARI:
1.0 SALAMU
ZA JUMLA:
NACHUKUA NAFASI HII KUWAKARIBISHA NA KUWAPONGEZA KWA JINSI MNAVYOSHIRIKIANA
NA WIZARA HII KUPIGA VITA UHALIFU / UJANGILI WA RASILIMALI ZA TAIFA. AIDHA
NATAMBUA JINSI MLIVYOTENGA MUDA WENU NA
KUFIKA HAPA ILI TUPEANE TAARIFA ZA KIUTENDAJI HUSUSANI OPERESHENI INAYOENDELEA
KATIKA WILAYA YA LIWALE MKOA WA LINDI.
NDUGU WANAHABARI:
2.0
UTEKELEZAJI WA OPERESHENI:
KUMEKUWA
NA ONGEZEKO LA VITENDO / WIMBI LA UHALIFU / UJANGILI WA NYARA ZA SERIKALI AMBAO
UNAATHIRI RASILIMALI ZA TAIFA HUSUSANI WANYAPORI TEMBO, VIBOKO, SIMBA, MAMBA, TWIGA, NYATI NA WANYAMA WENGINE PAMOJA NA
UVUNAJI HARAMU WA MAZAO YA MISITU. KUTOKANA NA HALI HIYO, WIZARA YA MALI
ASILI NA UTALII ILIOMBA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI KUPITIA WIZARA YA MAMBO
NDANI YA NCHI KUANDAA OPERESHENI MAALUM WILAYANI LIWALE KUDHIBITI HALI HIYO.
JESHI LA POLISI LILIKIAGIZA KITENGO CHA KUPAMBANA NA UHALIFU MKUBWA NCHINI
(NATIONAL AND TRANSNATIONAL SERIOUS CRIME INVESTIGATION UNIT – NATIONAL TASK
FORCE) AMBACHO KINAVISHIRIKISHA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYA (POLISI, JWTZ,
TISS, MAGEREZA, UHAMIAJI NA OFISI YA DPP) KUTEKELEZA MAJUKUMU YA OPERESHENI
MAALUM KAMA ILIVYOELEKEZWA. OPERESHENI HII ILIANZA TAREHE 22/07/2012 NA NI ENDELEVU. KATIKA OPERESHENI HIYO MAOFISA WAKUU WAANDAMIZI, MAOFISA WA KATI,
WAKAGUZI NA ASKARI WA KAWAIDA KUTOKA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA TAJWA HAPO
JUU WANASHIRIKI UTEKELEZAJI WA OPERESHENI HIYO.
MATOKEO
YA AWALI YA UTEKELEZAJI WA OPERESHENI HII NI KAMA IFUATAVYO;
v WATUHUMIWA
101 NA KESI 101 ZIMEFUNGULIWA KITUO CHA POLISI LIWALE KATI YA HIZO:
i.
KESI
15 ZIMEFIKISHWA MAHAKAMANI NA MIONGONI MWAKE KESI MOJA (1) IMETOLEWA
HUKUMU NA ZILIZOBAKI ZIKO KWENYE HATUA MBALIMBALI MAHAKAMANI,
ii.
KESI 20 ZIMESIKILIZWA
NA KUPATA HUKUMU YA “BINDING OVER”, MIONGONI
MWAKE KESI 7 ZIMEPATA MAAMUZI NA 13 ZINASUBIRI MAAMUZI YA MAHAKAMA. MASHARTI YA
“BINDING OVER” YALIYOTOLEWA YAMETOLEWA DHIDI YA WATUHUMIWA;
a.
KUTOTOKA
NJE YA WILAYA YA LIWALE BILA KIBALI CHA HAKIMU MKAZI WA WILAYA
b.
KURIPOTI
KWA OC CID KITUO CHA POLISI LIWALE KILA
MWISHO WA MWEZI
c.
KUITWA
KUHOJIWA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA WAKATI WOWOTE KADRI
ITAKAVYOONA INAFAA
d.
KUTOFANYA KOSA LOLOTE NDANI YA MIAKA MIWILI YA MATAZAMIO
e.
KWA WALIOKUWA WAMILIKI WA SILAHA, SILAHA ZAO ZIMEHODHIWA
POLISI LIWALE KWA MUDA WA MIAKA MIWILI NA MMILIKI ATAWAJIBIKA KUANZA TARATIBU
ZA MAOMBI YA KUMILIKI SILAHA HIYO / HIZO UPYA PINDI UTEKELEZAJI WA HUKUMU HIYO
ITAKAPOMALIZIKA
f.
KUWEKA DHAMANA YA MALI ISIYOHAMISHIKA YENYE THAMANI YA
TSH. 5,000, 000.00 NA MALI HIZO ZIWE NDANI YA WILAYA YA LIWALE
II. KESI 66
ZINAENDELEA KUFANYIWA UCHUNGUZI ILI WAHUSIKA WAFIKISHWE MAHAKAMANI
v AIDHA
KATIKA OPERESHENI HII VIJIJI 27 VYA WILAYA YA LIWALE VINGI VIKIWA VIMEPAKANA NA
HIFADHI YA SELOUS VIMEHUSIKA. MATOKEO YAKE NI KUPATIKANA KWA SILAHA 80, RISASI 674
NA MAGANDA YA RISASI 289 KAMA IFUATAVYO;
v BUNDUKI
79 ZILIZOKAMATWA NI;
i.
SAR - 1,
ii.
RIFLE - 16
iii.
SHOT GUN
- 63
v JUMLA YA
RISASI 645 ZIMEKAMATWA NI;
i.
SAR - 20,
ii.
RIFLE - 8
iii.
SHOT GUN – 647
v MAGANDA
YA RISASI 289 YALIYOKAMATWA NI ;
i.
RIFLE - 99
ii.
SHOT GUN – 190
v NYARA ZA SERIKALI;
SN
|
AINA YA NYARA ZILIZOKAMATWA
|
KIASI
|
THAMANI TSH
|
1
|
MENO YA
KIBOKO,
|
80
|
18,892,500.00
|
3
|
MENO YA TEMBO
|
14
|
164,075,000.00
|
5
|
BANGILI MOJA YA USINGA WA MKIA WA TEMBO
|
1
|
23, 625, 000.00,
|
6
|
NGOZI ZA SIMBA,
|
2
|
15,435,000.00
|
7
|
NGOZI YA CHUI,
|
1
|
5,505,500.00
|
9
|
MIKIA MIWILI
YA NGEDERE
|
2
|
378,000.00
|
10
|
KICHWA CHA NYATI CHENYE PEMBE 2,
|
1
|
2,992,500.00
|
11
|
NYAMA YA NYATI ,
|
KG
|
2,988,700.00
|
12
|
KICHWA CHA POFU CHENYE PEMBE 2,
|
1
|
2,677,500.00
|
JUMLA KUU
|
212,944,700.00
|
v VIELELEZO VINGINEVYO
o GARI NDOGO AINA YA TOYOTA CORONA NO. T. 836 ADV
o PIKIPIKI
MBILI ZA SANLG T. 901 BXQ NA T. 772 BSD
o
MSUMENO WA MBAO NA MBAO 149
3.0 LENGO
LA OPERESHENI;
OPERESHENI
HII MAALUM INALENGA KUZUIA, KUDHIBITI NA KUPAMBANA NA UHALIFU / UJANGILI KATIKA
MAENEO MBALIMBALI NCHINI WILAYA YA LIWALE IKIWA KAMA ‘ROLE MODEL’.
4.0
MAFANIKIO;
I.
KWA KUWA OPERESHENI HII IMEPANGWA NA
KUENDESHWA KITAALAM NA KISAYANSI (INTELLIGENCE LED OPERATIONS), MAFANIKIO
YAFUATAYO YAMEJIDHIHIRISHA;
a.
IMEUNGWA MKONO NA KUSIFIWA NA RAIA NA
WANANCHI KWA UJUMLA KWA MAELEZO KUWA HAKUNA MTUHUMIWA ALIYEKAMATWA KWA KUONEWA.
b.
KUMEKUWEPO NA MAPOKEO CHANYA (POSITIVE IMPACT)
KUTOKANA NA WANANCHI KUTAMBUA KUWA MWENENDO WA OPERESHENI HII UNAIPA HESHIMA
KUBWA SERIKALI
c.
HAKUKUWA NA RAIA MWEMA
ALIYEBUGHUDHIWA AU KULALAMIKIA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA OPERESHENI HII
ii.
MTANDAO WA UHALIFU WA UJANGILI
UNAVUNJWA NA WAHUSIKA WOTE SASA WANAFAHAMIKA NA UCHUNGUZI MAKINI NA WA KINA
UNAENDELEA DHIDI YAO NA WATAFIKISHWA MBELE YA MAHAKAMA NA SHERIA ICHUKUE MKONDO
WAKE
iii.
BAADHI YA WAZEE WENYE UMRI MKUBWA NA
AMBAO AFYA ZAO ZILIONEKANA KUTOMUDU MASHARTI YA KUENDELEA KUMILIKI SILAHA
WALIZISALIMISHA WENYEWE NA KUOMBA ZIHIFADHIWE KATIKA KITUO CHA POLISI LIWALE
MPAKA MAAMUZI YATAKAPOTOLEWA NA MAHAKAMA DHIDI YA SILAHA HIZO.
iv.
WALE AMBAO MAHAKAMA ITAONA WAMEPOTEZA
SIFA ZA KUMILIKI SILAHA ZITAHODHIWA KITUO CHA POLISI KUSUBIRI UTEKELEZAJI WA
MAAMUZI YA MAHAKAMA
5.0
CHANGAMOTO:
i.
BAADHI YA WAMILIKI WA SILAHA SIO
WAAMINIFU KWA KUWA WANATUMIA SILAHA
ZAO KUFANYA UJANGILI AU KUZIAZIMISHA KWA MAJANGILI.
ii.
BAADHI YA WAMILIKI WA
SILAHA WAMEPOTEZA SIFA ZA UMILIKI KUTOKANA NA MATATIZO YA KIAFYA; MFANO
KUKABILIWA NA UPOFU, UGONJWA WA KIHARUSI N.K JAMBO AMBALO LINACHANGIA WAO
KUSHINDWA KUZINGATIA NA KUTEKELEZA TARATIBU ZA UMILIKI WA SILAHA
6.0
MUONO WA MBELE (WAY FORWARD);
i.
WIZARA
YA MALI ASILI NA UTALII ITAENDELEA KUTOA ELIMU KWA JAMII ZINAZOISHI KANDOKANDO
YA MAPORI YA AKIBA / HIFADHI KUHUSU
UMUHIMU WAO WA KUTOJIHUSISHA NA UJANGILI NA WAWE VYANZO VYA TAARIFA ZA
KIINTELIJENSIA KUFUATIA MKAKATI MADHUBUTI WA KUDHIBITI MTANDAO WA UJANGILI
NCHINI.
ii.
UTAKUWEPO
MWENDELEZO WA KUBORESHA NA KUIMARISHA DORIA, MISAKO NA HATUA NYINGINE ZA
KIOPERESHENI KWENYE MAPORI YA AKIBA NA HIFADHI ZA TAIFA MARA KWA MARA KUFUATIA
MUONGOZO WA TAARIFA ZA KIINTELIJENSIA KADRI ITAKAVYOONEKANA INAFAA KATIKA
KUFANYA OPERESHENI ZA PAMOJA (JOINT OPERATIONS INVESTIGATIONS & INTELIGENCE
–JOII) KWA KUTUMIA VYOMBO VYA ULINZI NA
USALAMA KUPITIA “TASK FORCE” YA KITAIFA .
7.0 MWISHO
NAWAPONGEZA MAOFISA
WAANDAMIZI, MAOFISA WA KATI, WAKAGUZI NA ASKARI WA VYEO MBALIMBALI WANAOSHIRIKI
UTEKELEZAJI WA OPERESHENI HII INAYOENDELEA. KWA UJUMLA NAMALIZIA KWA
KUWASHUKURU TENA NYINYI WANAHABARI MLIOFIKA HAPA KWA USHIRIKIANO MNAOUTOA
KATIKA KUPAMBANA NA UHALIFU HUU.
ASANTENI
SANA KWA KUNISIKILIZA
//////////////////////////////////////////MWISHO///////////////////////////////////////
IMETOLEWA TAREHE 08/08/2012 NA
MHE. BALOZI KHAMIS .S. KAGASHEKI
(MB)
WAZIRI
NAKALA KWA:
VYOMBO VYA HABARI
0 comments:
Post a Comment