13 Feb 2013Pichani ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Philip Mangula,na Katibu Mkuu wa Chama hicho Abdulrahman Kinana  wakiwa na Juliana Shonzi na Mwampamba waliohama Chadema na kujiunga na chama tawala.

Umuhimu wa tukio hilo haupo kwenye picha hiyo wala uamuzi wa wanasiasa hao kujiunga na CCM,bali ukweli kwamba katika siku za hivi karibuni, wanasiasa hao wachanga walitokea kuwa chanzo cha sokomoko ndani ya Chadema hasa kwa kutumia mitandao ya kijamii.

Kama wasemavyo waswahili,Mungu hamfichi mnafiki. Wakati Shonzi na Mwampamba walipokuwa wakipita huko na kule kujaribu kuihujumu Chadema kutoka ndani, baadhi yetu tulifahamu kuwa wanasiasa hao walikuwa wakitumiwa na CCM,chama ambacho licha ya ukongwe wake kimekuwa mahiri katika uendeshaji wa hujuma dhidi ya vyama vya upinzani.

Japo uamuzi wa wanasiasa hao kuhama Chadema na kujiunga na CCM ni matumizi ya haki zao za kidemokrasia na kikatiba, lakini kwa kiwango kikubwa kitendo hicho kinasaidia kuipa nafuu Chadema,sio tu kwa maana ya 'kuvuja kwa pakacha ni nafuu ya mchukuzi' bali pia kuuthibitishia umma kuwa kelele za hapa na pale kutoka kwa baadhi wa viongozi wa chama hicho wanaodai kuhujumiwa kwa madai ya 'ukandamizwaji wa demokrasia ndani ya Chadema' ni matokeo ya harakati zisizoisha za CCM kukihujumu chama hicho na vyama vingine vya upinzani.

Wakati Shonzi na Mwampamba wameshapata 'dakika zao 15 za umaarufu' (15 minutes of fame) ni vema wakatambua kuwa kazi waliyotumwa na 'mwajiri' wao huko CCM haikufanikiwa hasa kwa vile jitihada zote walizotumia kuichafua Chadema zimesihia kupuuzwa na watu wengi makini.

Kadhalika, ni muhimu kwao kutambua kuwa licha ya CCM kutumia kila njia-huku nyingi zikiwa ni chafu- lakini kwa hakika chama hicho sio tu kimezeeka bali kina kansa kali ambayo inyeshe mvua liwake jua lazima kitang'oka madarakani.Kama si mwaka keshokutwa 2015 basi miaka michache ijayo.

CCM itakufa kwa sababu itafika mahala Watanzania walio wengi watafikia mwafaka kuwa kuendelea kukiacha chama hicho madarakani ni sawa na ku-fast track kifo cha taifa letu.Haihitaji uelewa wa siasa za huko nyumbani kutambua kuwa vurugu mbalimbali zinazoendela kujitkeza huko nyumbani ni matokeo ya siasa za kihuni za CCM,chama ambacho kipo tayari kufanya lolote hata kama lina madhara kwake au kwa taifa,ilimradi tu kiendelee kubaki madarakani: si kwa minajili ya kutumikia umma bali kuendeleza ujambazi wa mchana kweupe (daylight robbery) kufilisi nchi yetu.

Ni wazi kuwa kuodnoka kwa Shonza na Mwampamba ni good riddance kwa Chadema...watatumika kwa siku mbili tatu kuichafua Chadema na hususan Dkt Slaa lakini mwisho wake ni kama ilivyo kwa kondomu: muhimu kabla na wakati wa tendo la ndoa,lakini uchafu usiovumilika baada ya shughuli hiyo.0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube