Jeshi la polisi Zanzibar limetoa mchoro wa sura (E-FIT) ya aliyemuua Padre Evaristus Mushi. Mchoro huo umepatikana baada ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na Polisi Zanzibar kuwahoji watu walioshuhudia tukio hilo la mauaji. Wananchi wametakiwa kuripoti polisi pindi wakimwona mtu mwenye sura hiyo.