28 Aug 2014

Kabla ya kukuletea 'darasa' hili ni vema nikakufahamisha kitu kimoja: 'tabia' iliyozoeleka miongoni mwa Wamarekani wengi kudhani kuwa 'dunia' inaishia kwenye mipaka ya nchi hiyo tu. Kuna idadi kubwa tu ya Wamarekani wasio na habari na 'dunia nje ya Marekani,' na pengine ndo maana si ajabu kukutana na 'Kombe la Dunia' la mchezo flani nchi humo linalohusisha timu za Marekani pekee...kwa vile kwa mtizamo wa wengi, Marekani ndio dunia.

Twende kwenye mada husika. Pengine kutokana na mtizamo huo fyongo, baadhi ya watengenezaji apps za simu 'hujisahau' na kudhani wamiliki pekee wa simu wapo Marekani hivyo apps zao zikiwekwa Google Play, kwa mfano, zinaweza kutumika nchini humo tu. Na hii ni moja ya sababu za kukutana na ujumbe "This app is not available in your country."

Lakini next time ukikutana na ujumbe huo usipaniki, kwani darasa lifuatalo linakueleza kiufasaha jinsi unavyoweza 'kuizunguka amri hiyo,' na kufanikiwa ku-download app yoyote ile katika simu yako, alimradi iwe 'compatible.'

Fuatilia video ifuatayo, lakini kama utakwama mahali flani basi usisite kuwasiliana nami kwa ufafanuzi zaidi.Kwa habari zaidi za teknolojia, endelea kutembelea blogu hii, na rahisisha zoezi hilo kwa kubonyeza menu ya TEKNOLOJIA hapo juu. Karibuni sana.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube