20 Aug 2016

Baadhi ya vyombo vya habari viliripoti jana kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akieleza kuwa Watanzania wanaruhusiwa kwenda jijini Dar es Salaam lakini LAZIMA WAWE NA SIFA MAALUM...na japo wanaruhusiwa kutembelea ndugu zao LAKINI WASIKAE SANA.

Hivi huyu mtu kalewa madaraka ama? Yeye ni nani hasa wa kuingilia HAKI YA WATANZANIA ILIYOWEKWA WAZI KWENYE IBARA YA 17 CHA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA inayotamka bayana Sasa huyu Makonda ni nani hasa kiasi cha kujiona yupo juu ya Katiba na kuingilia haki na uhuru wa Watanzania? 

Huyu bwana amekuwa mtu wa kukurupuka tu na amri, nyingi zikiwa zisizo na kichwa wala miguu kwa maana ya ugumu wa kutekelezeka kwake. 

Ninatumaini kuwa Rais Dkt John Magufuli hatoruhusu uhuni wa madaraka wa aina hii ambao kimsingi utapelekea hisia za 'Magufuli ni dikteta' kupata nguvu zaidi.

Tupo mwaka 2016 halafu anakurupuka mtu kuwarejesha Watanzania kwenye zama za ukoloni ambapo serikali ya mkoloni ilidhibiti uhuru wa wazawa kwenda watakako kama mbinu ya kudumisha ukoloni na kudhibiti upinzani dhidi ya mkoloni.

Mbinu hiyo ya kidhalimu ilitumika pia wakati wa utawala wa kinyama wa Makaburu huko Afrika Kusini ambapo Weusi walipaswa kuwa na ruhusa maalumu kutoka nje ya maeneo yao.

Huyu Bwana Makonda aendelee kufuatilia hao mashoga, ombaomba, wavuta shisha, nk ambao ni dhahiri wamemzidi akili na wanaendelea na maisha yao kama kawaida.

Wito wangu kwa Bwana Makonda ni kwamba yawezekana kabisa kuwa kiongozi mzuri bila kukurupuka na amri zisizo na mwelekeo. Ni muhimu kwa RC huyo kutofautisha maigizo na uongozi, na akitaka maigizo aende bongo movie.

Hizi ni jitihada za makusudi za kumkosanisha Rais Magufuli na Watanzania.0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube