28 Feb 2020


Kabla hujanitolea jicho kwa kutanabaisha kuwa "hatuna uhaba wa viongozi wapumbavu," na kunituhumu kuwa nimekosa heshima kwa viongozi wetu, naomba tu kukukumbusha kauli maarufu ya Rais wetu John Magufuli 

Image


Sasa kama Mheshimiwa sana Magufuli anaweza kutumia neno hilo kwanini sie watawaliwa wake iwe dhambi? 😝

Naam taifa letu halina uhaba wa viongozi wapumbavu, na ndio maana baadhi yao wamefikia hatua ya kuaminiwa na Rais wetu hadi kupewa dhamana ya kuongoza wizara muhimu. 

Jana nilikutana na clip moja inaeleza kuhusu ujio wa lundo la watalii kutoka CHINA. Yes, China hii hii ambayo kwa sasa ndio kama "makao makuu" ya maambukizi ya virusi vya Corona.


Huku nchi za Magharibi, ambako wana teknolojia za hali ya juu kutambua maradhi mbalimbali ikiwa ni pamoja na maambukizi ya virusi vya Corona, wanafanya udhibiti mkali kwa kila mtu anayetoka China, ikiwa ni pamoja na raia wa nchi hizi za Magharibi. Muda huu ninapoandika makala hii, kuna raia kadhaa wa Uingereza "waliozuiliwa" sehemu mbalimbali kufuatia tishio la maambukizi ya virusi hivyo.

Sasa sijui sie ni kiburi tu au kutojali uhai wa Watanzania wenzetu au ndio huo upumbavu wa kupindukia, bila hofu wala aibu tuna viongozi wanaoruhusu ujio wa lundo la Wachina katika kipindi hiki hatari.

Kibaya zaidi, nimemsikia daktari mmoja anaongelea suala hilo kwa kuwakejeli walioapatwa na taharuki kutokana na ujio wa Wachina hao, akidai kuwa Wachina hao wamefanyiwa vipimo vyote. 

Huu ni zaidi ya upumbavu, kwa sababu pindi jana la virusi hivyo likiingia katika Tanzania yetu itakuwa balaa kubwa. Huu sio ugonjwa wa "watu masikini" kwa sababu moja ya njia za kusambaa kwake ni pamoja na msongamano, kitu kilichozeleka kwenye daladala zetu, maeneo kama Kariakoo, mashuleni na vyuoni, nk. 

Nihitimishe makala hii kwa kukuambatanishia ujumbe huu muhimu pichani


Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.