Showing posts with label ANNE MAKINDA. Show all posts
Showing posts with label ANNE MAKINDA. Show all posts

1 Feb 2012

Katuni kwa hisani ya Said Michael na Global Publishers

25 Jun 2011


Mshairi Muyaka Al Ghassany (1776-1840 ) toka Mombasa aliwahi kusema hivi:

Vita vyako Fahamu
Havimdhuru Karimu
Ila wewe Bahaimu
Jujue Utaumia

Katika hali isiyo ya kawaida Jumuiya ya wa Swahili Tanzania imemjia juu Spika Anne Makinda juu ya kauli yake ya kuwakebehi watu wa Kariakoo ambako wengi wao wana asili ya Kiswahili.

Tamko rasmi la Jumuiya ya waswahili limekuja baada ya kauli ya makinda iliyojaa dharau na kebehi kwa wabunge kuwa wasiwe kama watu wa Kariakoo. Klabu ya Saigon nayo imesema itatoa tamko lao rasmi kesho juu ya haya matamshi machafu na ya dharau ya spika Anna Makinda.

Anne Makinda labda alitakiwa kurudi darasani na akapigwe brash kuhusu umuhimu wa Kariakoo na watu waliowahi kuishi kariakoo na Makinda should know better than most kuwa hicho chama kilichomweka kwenye hicho kiti alichokalia kilizaliwa Kariakoo na na kusema ukweli ni kuwa dharau aliyoitoa Anna Makinda kwa kariakoo itakuwa si kwa wafanya bishara ndogo ndogo walipo pale bali ni pamoja na waswahili wengine kama akina Mwinjuma Mwinyikambi, Kiyate Mshume, Jumbe Tambaza, Sheikh Hassan bin Amir and Sheikh Suleiman Takadir ambao walikuwa ni wakaazi wa Kariakoo.

Labda Makinda angeongea na wenzie wakampeleka maeneo ya makuu 4 yaliyoifanya kariakoo :

1.Kariakoo

2.Gerezani

3.Kisutu

4.Mission Quarter.

Spika Anna angejua watu wa Katiakoo wameshiri vipi kwenye kwenye uhuru wa nchi hii asingeweza kuwatukana wabunge kwa dharau kama alivyofanya leo.

Najua Makinda hawezi kumwomba ZUNGU au wabunge wengine wa Dar lakini sitoshangaa kuwa huyu mama akawa hajui hata hiyo TAA ilikuwa na makao makuu wapi na sacrifice zipi mzee Bin Sudi aliziingia kutoa lile jengo mwaka 1930!

Anna kama ulijuwa hujui basi ujue kuwa jengo hili ndio TANU ilizaliwa na mpaka leo lipo pale mtaa wa kariakoo na Mtaa Mpya ulipoungana

Kama ulikuwa hujui basi upande wa Magharibi wa Kariakoondiko ilikokuwa Mission Quarter (NYUMA YA TBL) na eneo hili lilitengwa maalim kwa ajili ya kuwalinda wahamiaji na waswahili waliokuwa wengi kariakoo na ambao waliishhi kwa amani na utulivu kwa miaka zaidi ya 70 mpaka leo hii ambako Pspika wa Bunge unatoa kauli zenye nia ya kuvunja amani na utulivu baina ya watu wa kariakoo

Kwa kuonyesha kuwa Waswahili wa Kariakoo walikuwa hawana kinyongo ndio maana majina ya mitaa imebaki vile vile kama vile mtaa wa Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda, Muheza , Magila na sasa hivi mmetuletea jina la mpuuzi wenu yule (MAKAMBA) na mkampa mtaa jina ili hali hana lolote la maana linalomsabahisha na Kariakoo (when time will come TUTALIONDOA)

Lakini wana JAMII FORUM msimlaumu sana huyu Anna Makinda kwani naye anafuata nyayo za baba yake Mwalimu Nyerere ambaye alianza kupandikiza mbegu mbaya za kudharau not only waswahili lakini wana kariakoo kwa ujumla.

Watu wengine maarudu ambao walikuwa ni wana Kariakoo walikuwa wakazi wa MISSION QUATER ni babu yangu bwana THOMAS PLANTAN ambaye alikuwa ni rais wa African Association na al Marhum mzee JOHN RUPIA ambaye alikuwa ni tajiri mkubwa sana enzi zile.

Anna Makinda kama hujui basi kwa taarifa yako tuu ni kuwa nyumba ya Al Marhum John Rupia ilikuwa mtaa wa Likoma na Magila, nyumba hii mpaka leo ipo na ndiko African Association ilianzishwa mwaka 1929. Nyumba hii mpaka leo ipo japi si katika hali yake ya zamani.

Lakini pia nataka nikujulishe kuwa Mission Quarter ndiko kulikokuwepo kiwanda cha kuchapisha cha mwafrica wa kwanza ambacho kilikuwa cha mzee wangu MASHADO PLANTAN ambaye alikuwa ni mtu wa kusini na alikuwa anachapisha JAMII FORUM ya enzi hizo ilikuwa ikiitwa ZUHURA ambayo Nyerere alikuwa analitumia sana kupiga debe dhidi ya wakoloni!

Lakini yote hayo Makinda kwako unaona ni upuuzi tuu kwani kariakoo pia ina eneo linaitwa GEREZANI ambako ilikuwa ni nyumbani kwa Omari Londo, Ally Sykes, Zuberi Mtemvu, Mashado Plantan, Muhsin Mende and Dossa Aziz. Hawa walikuwa ni majabali na wazalendo waliokutana na Nyerere baadae. Kwa kuonyesha tuu kuwa sisi si wafuata bendera, ZUBERI MTEMVU, MUHSIN MENDE na MASHADO PLANTAN waliamua kujiondoa TANU na kuanzisha chama kingine cha upinzani kwa jina la TANGNYIKA AFRICAN CONGRESS na hapo ndiko zilianza tofauti kubwa na baba yako Nyerere.

Anna makinda unaposema waBunge wasiwe kama watu wa kariakoo unamaana hutaki wawe INDEPENDENT THINKERS kama akina Mzee Mshume Kiyate, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Idd Faizi, Idd Tosiri, Bantu Kasella Bantu, Abdulwahid Sykes and Dossa Aziz?

Kwa kuendelea kukuambia tuu umuhimu wa kariakoo ni kuwa ile open space inayotazamana na viwanja vya Mnazi Mmoja ilikuwa ni plot ya JOHN RUPIA ambayo aliitoa kama zawadi kwa TANU ili wajenge ile centre. Of course kwa sababu ya serikali yako ilivyokuwa haithamini historia na heritage ili nyumba ilivynjwa wamejenga gorofa pale bila kuzingatia au kuweka kumbukumbu yoyote ile, na huyo baba yenu Nyeree mnaye sema kuwa mnahifadhi ujumbe wake historia kaye nyingi iliyokuwa mle ndani iliishia kutupwa bila mazingatio yoyote yale ya kuhifadhi yaliyokuwa mle.

Sehemu nyingine ambayo leo hii umeitukana ni Soko la kariakoo ambalo Nyerere alikuwa haishi kwenda pale....bila kusahau kuwa hata shirika la masoko kariakoo lilikuwa linatoa SCHOLARSHIP kuwasomesha watu mpaka University of Dar.

Leo Hii spika wa Bunge umeamua kuwatukana :

WASHOMVI ambao walikuwa wanafanya baishara ya samaki

WAZARAMO ambao walikuwa wanafanya baishara ya nazi

WANYAMWEZI (wanawake) ambao walikuwa wanafanya baishara ya tumbaku kavu huku wanaume wakifanya biashara ya viazi ziliskukuwa zinalimwa Kigamboni

WALUGURU walikuwa wanafanya biashara za machungwa na mboga za majani

WAARABU walikukuwa wanafanya biashara ya ngano, mabucha ya nyama, na viungo mbali mbali

WAHINDI walikuwa wanashindana sana na WAARABU kwenye biashara mbali mbali

Je Anna Makinda unajua kama Nyerere aliwahi kufanya kazi soko la kariakoo kama Market Master? Je unajua kama ofisi yake ilikuwa kwenye junction ya mtaa wa Tandamti ( siku hizi mnauita mtaa wa Mshume Kiyate) na mtaa wa Swahili?

Matusi uliyowatukana wana Kariakoo leo ni matusi ambayo umewatukana wa Swahili wa Mwembe Togwa (siku hizi mnapaita Fire), Umewatukana wakari wa Ronald Cameroon Road ( sikuhizi United Nations Road) na wengineo wengi...lakini wansiasa wenye calibre za wewe Anna Makinda ndio hao hao mlioamua kuquestion maamuzi ya mzee Kitwana Kondo alipokuwa meya mwaka 1995 alipoa mua kubadili jina la mtaa wa Tandamti na kuita mtaa wa Mshume Kiyate ...tena mlipiga makelele mkisaidiwa na waandishi wa habari ambao hawaijui historia ya kariakoo kwa kuuliza huyu Mshume Kiyate ni nani? Nyie nyie ndio mlilalamika mitaa mingine ya kariakoo ilipobadilishwa na kupewa majina ya Tatu Binti Mzee, Max Mbwana, Omari Londo halafu leo hii unathubutu kututukana sisi wana Kariakoo!

Onyo kwa Anna Makinda na wanasiasa wenye tabia za kudharau watu wa kariakoo kama Cyrill Chami na wengineo, Wana Kariakoo na Waswahili wa zama hizi hatutonyamaza kwani vyombo vya kulalama tunavyo na haki zetu tunazijua na mkiendelea na dharau zenu basi mjue kuwa pamoja kuwa waswahili hatutonyamaza na kama ikiwezekana tujibu mapigo basi tutaangalia namna bora zaidi za kuwajibu lakini hatutokaa kimya...maana leo mmeanza na waswahili na watu wa kariakoo kesho tunajua mtahamia kwa wa chagga na watu wa Moshi kesho kutwa mtahamia kwa nyakyusa na watu wa Mbeya na Iringa

Tofauti ni kuwa sasa tumelimika na tunaouwezo wa kuona mnapoanza kutuletea dharau bila kujali wakazi na watu wa kariakoo nao ni wapiga kura kama watu wa kwenu

Muyaka al Ghassany pia alisema hivi:
Yu wapi Firauni
Yuwapi wapi Karuni
Na Shadadi Maluuni
Wote wameangamia

Anna Makinda leo umeamua kuwatukana wana Kariakoo, historia ya Kariakoo na wanaotafuta rizki zao Kariakoo na Waswahili wanaoishi pale lakini ukae ukijua kuwa kuna leo na kesho na sisi hili hatutosahau. Mshazowea kututukana lakini at some point someone has to stand up and say no hatukubali. Labda umesahau kuwa kwa waswahili wa Kariakoo kuna 2 extremes ambazo naona ushazowea ile moja tuu

CHANZO: Jamii Forums

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.