PENGINE KUNA CHA ZIADA KINACHONIFANYA NISIAMINI MACHO YANGU KUONA JACOB ZUMA NDIO HIVYOOO ANAELEKEA KUKABIDHIWA URAIS WA AFRIKA KUSINI.NCHI ZA MAGHARIBI ZINAFUATILIA KWA KARIBU YANAYOENDELEA HUKO SAUZI,LAKINI HOFU YA WENGI NI KUWA HUENDA ZUMA NI POPULIST FLANI AMBAYE AMEFANIKIWA SANA KUKONGA NYOYO ZA WENGI NCHINI HUMO LAKINI ANAYEWEZA PIA KULIINGIZA TAIFA HILO TAJIRI MATATIZONI.BINAFSI HUWA SINA IMANI YA KUTOSHA NA WANASIASA WANAOSHINDWA KUONYESHA UDILIFU KWENYE NDOA ZAO KISHA UWATARAJIE WAWE WAADILIFU KWA TAIFA.INAELEKEA WASAUZI WAMELIPUUZA HILO.