Showing posts with label KAGAME. Show all posts
Showing posts with label KAGAME. Show all posts

27 Aug 2010

Rais wa Rwanda Paul Kagame amechaguliwa tena kuongoza nchi hiyo baada ya kushinda kwa asilimia 93 katika uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni,lakini kulikuwa na taarifa zilizosambaa kuwa waandishi wa habari na wanasiasa wa vyama vya upinzani wameuawa au kuwekwa jela.Sasa,ripoti iliyovuja (leaked) ya Umoja wa Mataifa inaashiria kuwa jeshi la Rwanda linaweza kuwa limetenda uhalifu wa kivita na kuua makumi ya maelfu ya watu mwishoni mwa miaka ya 90 (late 1990s).

Kagame anaheshimika sana kwa kuleta maendeleo na amani kwa nchi hiyo iliyotiwa kovu na mauaji ya kimbari mwaka 1994 ambapo Wahutu (kabila kubwa nchini humo) waliwaua Watutsi (kabila dogo nchini humo)-na Wahutu wenye msimamo wa wastani- takriban milioni moja.Chini ya Kagame,ambaye ni Mtutsi na kamanda wa zamani wa jeshi,Rwanda sasa ni salama,huku ikitajwa kuwa miongoni mwa zenye rushwakidogo zaidi barani Afrika.Matokeo yake,nchi hiyo imekuwa ikipokea mamilioni ya dola katika misaada ya kimataifa na inaendelea kujijenga.

Lakini,kwa mujibu wa gazeti la New York Times,mmoja wa wapinzani wa Kagame alikutwa amekufa kabla ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 mwezi huu,huku kichwa chake kikikaribia kutenganishwa na kiwiliwili.Na wapinzani wengine "maarufu ambao waliongea hadharani kumpinga Kagame na pengine kuuweka majaribuni umaarufu wa Rais huyo walizuiliwa kushiriki katika uchaguzi",kwa sababu za kiufundi.Kagame amehalalisha hatua kali alizowahi kuchukua huko nyuma,kwa mujibu wa gazeti hilo,akidai kuwa Rwanda bado haijatulia vya kutosha.

Kwa jinsi gani hali nchi humo haijatulia inabainishwa na katika ripoti ya kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za binadamu,iliyopatikana na gazeti la Le Monde la Ufaransa kabla haijachapishwa.Ripoti hiyo inabainisha,kwa mujibu wa gazeti la The Guardian la Uingereza,mwaka 1996 wakati vikosi vya Watutsi vikiwakimbiza Wahutu kuelekea Jamhuri ya Kimekrasia ya Kongo (wakati huo Zaire),na mwaka 1998 katika uvamizi wa kudhibiti waasi wa Kihutu,jeshi la Rwanda na washirika wake liliwazingira mamia ya wanaume,wanawake na watoto na kuwachinja kwa kutumia majembe na mashoka.Nyakati nyingine,"wakimbizi wa Kihutu walichinjwa kwa kutumia sime za bunduki,kuchomwa moto au kupigwa nyundo".Matukio hayo,inaeleza ripoti hiyo,ni sawa na mauami ya kimbari.

Serikali ya Rwanda amepinga madai ya ripoti hiyo,na inadaiwa imetishia kuondoa askari wake katika jeshi la kulinda amani huko Darfur na kwingineko,iwapo ripoti hiyo itawekwa hadharani rasmi.Umoja wa Mataifa unaeleza kuwa ripoti ililyovuja ni rasimu (draft) tu.Inasubiriwa kuonwa kama jumuiya ya kimataifa itasalimu amri kwa shinikizo kutoka serikali ya Kagame kuondoa mpambano na kupunguza makali ya lugha katika chapisho timilifu (final version).

Imetafsiriwa kutoka Jarida la Newsweek

7 May 2009


NADHANI TAFSIRI SAHIHI YA "WORLD'S MOST INFLUENTIAL PEOPLE" INAWEZA KUWA NGUMU KWA LUGHA YETU YA TAIFA.SIJUI TUITE "WATU MAARUFU ZAIDI DUNIANI" AU "WENYE MVUTO ZAIDI" AU...?SINA HAKIKA KAMA INFLUENCE NI UMAARUFU AU MVUTO.ANYWAY,KWA MUJIBU WA ORODHA YA WATU 100 INFLUENTIAL KABISA DUNIANI KWA MWAKA 2009 INAYOANDALIWA KILA MWAKA NA JARIDA LA TIME LA MAREKANI,RAIS PAUL KAGAME AMESHIKA NAFASI YA 13.MARA NYINGI ORODHA HIYO HUPATA PIA UPINZANI NA KEJELI HUSUSAN KUTOKA KWA WAHAFIDHINA WANAOTAFSIRI JARIDA LA TIME NA ORODHA HIYO KUWA NA MRENGO WA KUSHOTO AU KILIBERALI ZAIDI.

"NDANI YA NYUMBA" PAMOJA NA KAGAME,NI MCHANYATO WA WANASIASA KAMA SENETA TED KENNEDY NA WAZIRI MKUU WA UINGEREZA GORDON BROWN,KIONGOZI WA KIYAHUDI MWENYE MSIMAMO MKALI KABISA AVIGDOR LIEBERMAN (Pichani Chini)
NA "MFALME WA UNGA" (COCAINE), JOAQUIN GUZMAN,"PABLO ESCOBAR MPYA" AMBAYE PIA NI MIONGONI MWA WATU MATAJIRI KABISA DUNIANI NA AMBAYE KICHWA CHAKE KIMEWEKWA REHANI YA US$ 5MILLION NA VYOMBO VYA DOLA VYA MAREKANI (Pichani Chini),MCHEZA SINEMA MWENYE MVUTO BRAD PITT,TAPELI LA PONZI BERNIE MADOFF,GWIJI LA "KUSEMA OVYO" RUSH LIMBAUGH,MWANAMUZIKI JOHN LEGEND(Pichani Chini),MWANADADA WA KIZAMBIA DAMISA MOYO (Pichani Chini)
BILA KUMSAHAU RAIS OBAMA NA MKEWE MICHELLE (Pichani chini na Oprah)
NA USUAL SUSPECTS KAMA TOM HANKS,GEORGE CLOONEY,TIGER WOODS NA WENGINEO.

BONYEZA HAPA KUANGALIA ORODHA KAMILI.HONGERA RAIS KAGAME.WANYARWANDA WANA KILA SABABU YA KUJIVUNIA UONGOZI WAKO HASA KWA TAIFA LILILOWEZA KUSIMAMA KIDETE KUTOKA KWENYE MAUAJI YA KIMBARI HADI KUWA HADITHI YA KUPIGIWA MFANO BARANI AFRIKA.ANYWAY,SIE TWAENDELEA KUJIVUNIA AMANI NA UTULIVU WETU UFISADI STYLE!!!

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.