Showing posts with label TAHADHARI. Show all posts
Showing posts with label TAHADHARI. Show all posts

16 Mar 2014

 
Jana nilifahamishwa na rafiki yangu mmoja kwamba ametumiwa barua pepe inayoonyesha kutoka kwa mwanasiasa mmoja wa huko Tanzania. Katika e-mail hiyo, mwanasiasa huyo anaonekana kulalamika kuhusu post 'iliyowekwa' na rafiki yangu huyo japo hakuna post aliyoweka.

Sasa jinsi gani matapeli hao wanavyojaribu kuku-trick uwapatie password yako? Wanakupa link wanayodai ndio yenye post yako huko Facebook, lakini ukiibonyeza inakutaka u-log into akaunti yako ya Facebook. Kimsingi link hiyo sio ya Facebook bali inalenga kunasa password yako.

Mara nyingi hackers (wezi wa password) wanacheza sana na hisia za mlengwa wao. Kwa mfano katika mbinu hii wanafahamu kuwa pindi ukipata e-mail inayokulaumu kwa kosa mbalo hujalifanya unaweza kukurupuka kwa hasira kutaka kumthibitishia huyo anayekutuhumu kwamba hujafanya kitu kama hicho. 

Tahadhari muhimu kuhusu hackers ni kwamba pindi upatapo e-mail za 'kisanii' kama hiyo aliyotumiwa rafiki yangu, IFUTE HARAKA SANA. Usihangaike kuwajibu kwa sababu unapo-reply e-mail kuna information flani kwenye "full header" inayoweza kumpatia hacker taarifa za kukuhujumu.

Basi tafadhali mfahamishe na mwenzako kuhusu utapeli huu mpya.

As always, SHARING IS CARING

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.