
App hiyo ambayo kwa kiasi kikubwa 'imeifunika' app maarufu ya mawasiliano ya meseji, Skype, ilinunuliwa hivi karibuni na kampuni kubwa ya biashara za mtandaoni (e-commerce) Rakuten ya Japan kwa dola milioni 900 imetanua mabawa yake kwa kuwezesha video calls kwa simu za Android na iOS.
Viber ilianza jaribio la video calls katika app yake kwenye desktop lakini sasa imhamishia uwezo huo kwenye app ya simu pia.
Kadhalika, toleo jipya la Viber (Viber 5.0) itamwezesha mtumiaji ku-share contacts kwa kutumia QR Code.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Viber Talmon Marco anasema, "Dhamira yetu haijakamilika...Sasa unaweza kupiga simu kwa video kwa kutumia Viber kwenye PC/Mac yako na kwenye simu katika namna ya kukuridhisha kabisa."
Viber sio app ya kwanza ya meseji kuwezesha video calls. Skype, Line, WeChat, Kakao na lundo la apps nyingine zina feature hiyo pia.
Downloads: Viber kwa Android, iOS, Windows Phones, Blackberry, Nokia, Windows 8 na Viber kwenye desktop yako
Downloads: Viber kwa Android, iOS, Windows Phones, Blackberry, Nokia, Windows 8 na Viber kwenye desktop yako