18 Feb 2013


Padri Evarist Mush amepigwa risasi kichwani na kufa papohapo na watu wasiojulikana akiwa njiani anaenda kuendesha misa katika Kanisa la Mt. Theresia liloko katka maeneo ya Betras Zanzibar
33Like ·  · 


I hope hao wababaishaji wetu wa Usalama wanaweza kuwa na mahala pa kuanzia uchunguzi wao. Tatizo ni kwamba wapo mahiri zaidi kutuandama akina sie tusio na madhara yoyote badala ya ku pre-empty uhalifu kama wa magaidi waliomuua Padre Evarist Mushi huko Zanzibar

17 Feb 2013


Padre E. Mushi Paroko wa parokia ya Minara Miwili Zanzibar ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika asubuhi hii. 

Ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ghafla ilitokea gari ndogo na waliokuwamo ndani ya gari ile wakamrushia risasi. 

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano. 

Taarifa hizi zimeripotiwa direct toka Zanzibar


CHANZO: Jamii Forums

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.