27 Sept 2008

Hatimaye mdahalo wa kwanza kati ya wagombea urais wa Marekani kwa vyama vya Democrat na Republican,Barack Obama na John McCain,respectively,umemalizika dakika chache zilizopita,mdahalo huo ulikuwa katika hatihati ya kufanyika kufuatia uamuzi wa McCain kusimamisha kampeni zake na kuomba mdahalo huo usogezwe mbele,kabla ya kubadili uamuzi huo (wa kushiriki mdahalo) mapema jana asubuhi.

Uchambuzi wa haraka haraka unaonyesha mambo kadhaa yaliyojitokeza kwenye mdahalo huo.Baadhi ya wachambuzi wanaona kwamba udhaifu wa Obama ulikuwa kwenye kuunga mkono hoja za McCain takriban mara saba (saying John is right on...) wakati McCain alikazania kuonyesha udhaifu wa Obama akitumia maneno kama "naivety","Obama doesnt seem to undestand",nk takriban mara nane.Kwa kuafikiana na McCain katika mitazamo au hoja zake,Obama anaweza kuonekana kama alikuwa defensive huku mpizani wake akiwa offensive,and that matters in politics.

Hata hivyo,kama ilivyotarajiwa,Obama ameonekana kufanya vizuri kwenye eneo ambalo anaaminika kuwa stronger kuliko McCain:uchumi.Kwa mwenendo wa mdahalo ulivyokuwa,yayumkinika kuhitimisha kuwa Obama alifanya vizuri kwenye nusu ya kwanza (takriban dakika 40 za mwanzo) ambapo hoja kuu ilikuwa uchumi.Kwa upande mwingine,McCain ameonekana kutawala zaidi kwenye nusu ya pili ya mdahalo huo ambayo iliangalia suala la sera za nje za Marekani.Kwa upande mwingine,pamoja na kutoonekana mshindi kwenye eneo hilo la sera za nje (ambalo McCain anachukuliwa kama mwenye uzoefu zaidi) Obama ameonekana kufanya vizuri zaidi kuliko ilivyotarajiwa kwa kusimamia anachokiamini na kutoyumbishwa na kauli za McCain kwamba mgombea huyo wa Republican ni mzoefu zaidi.Wapo wanaoona kwamba Obama ameweza kufanya kile alichotarajiwa kwenye "eneo lake la kujidai" yaani uchumi ilhali McCain ameshindwa kumfunika Obama kwa namna ilivyotarajiwa kwenye eneo la sera za nje.

Kadhalika Obama ameonekana kushindwa kuipigilia msumari ipasavyo hoja kwamba McCain amekuwa mshirika wa Bush katika kipindi cha miaka minane iliyopita.McCain nae kwa upande wake anaonekana ameshindwa kuitumia ipasavyo fursa ya kuonyesha yeye ni mzoefu zaidi katika eneo la sera za nje (kwa mantiki kwamba japo alifanya vizuri,hakufanya vizuri sana kama ilivyotarajiwa).Kwa kigezo cha hali mbaya ya uchumi nchini Marekani,Obama alipaswa kuwa mshindi lakini hilo halijalishi sana kwa vile mada ya mdahalo huo ilikuwa sera za nje,ambalo ni "eneo la kujidai" la McCain ambaye hata hivyo hakupata ushindi mnono kama ilivyotarajiwa.Kwa maana hiyo,kwa kushindwa kutumia vizuri "eneo lake la kujidai" (foreign policy) McCain anajiweka katika nafasi ngumu kwenye mijadala miwili ijayo ambayo inatarajiwa kuwa na mada ambazo ni strong points kwa Obama,kwa mfano uchumi na domestic affairs.

Japo sio hoja ya muhimu,yayumkinika kusema kwamba baadhi ya kauli za McCain kwa Obama zilikuwa kana kwa yuko patronizing.Ni muhimu kuonyesha kwamba wewe ni mjuzi zaidi katika eneo flani kuliko mpinzani wako lakini unapaswa kuwa makini kutoonekana "patronizing."Lakini pengine la muhimu zaidi,and this is my conclusion,Obama ameonekana kuzungumzia zaidi future ya Marekani na hivyo wakala wa mabadiliko (change) wakati McCain,kwa kusisitiza rekodi na uzoefu wake,ameonekana kuwa anapingana na msisitizo wake kwamba nae yuko for change.

BONYEZA HAPA kusikia mdahalo mzima.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.