21 Apr 2009


SAKATA la mgodi wa Kiwira kufikishwa bungeni, limeendelea kugubikwa na wingu zito, kutokana na ratiba za bunge kutoonyesha kama serikali itatoa ripoti.

Mgodi wa Kiwira, ambao unamuhusisha Rais wa Serikali ya awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati, Daniel Yona umejaa utata kutokana na madai kuwa kampuni ya Tan Power Resources Limited iliununua kwa Sh70 milioni badala ya thamani yake halisi ya Sh4 bilioni.

Hadi sasa serikali haijatoa ufafanuzi wowote kuhusu utata huo licha ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuahidi katika mkutano wa 13 wa bunge kwamba,ingetoa taarifa bungeni.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja alisema tu kwa kifupi "vuta subira".

Iwapo serikali haitatoa ripoti hiyo katika mkutano unaoendelea itakuwa ni mara ya tatu kupigwa tarehe suala hilo.

Katika mkutano wa 13, wakati mjadala wa mgodi wa Kiwira na Meremeta ukiwa umepamba moto, Pinda alisema serikali ilikuwa ikiandaa taarifa lakini akasema ni bora asulubiwe kuliko kutaja wamiliki wa Meremeta kwa maelezo kuwa inahusu usalama wa taifa.

Lakini, hadi mkutano huo unamalizika hakukuwa na ripoti yoyote ya serikali na hata ulivyokuja mkutano wa 14 hakukuwa na ripoti kama hiyo.

Tayari ratiba ya bunge imetoka na kuonyesha kwamba, hoja nzito inayotarajiwa kutikisa bunge hadi sasa ni ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ambayo imepangwa kuwasilishwa bungeni Aprili

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.