15 May 2010

Kwa hakika baadhi ya kauli za Rais wetu Jakaya Kikwete zinachanganya kupita kiasi.Juzijuzi tu alisaini kwa mbwembwe sheria tuliyoambiwa imelenga kudhibiti rushwa katika chaguzi.Tukiweka kando suala la wasaidizi wake kumwingiza mkenge kwa kuchomekea vipengele kinyemela,sambamba na mapungufu lukuki katika utekelezaji wa sheria hiyo (kubwa likiwa uswahiba kati ya CCM ya Kikwete huyohuyo na mafisadi),uamuzi wa kuwa na sheria hiyo ulileta faraja kidogo kwamba angalau mkuu wa nchi sasa anaanza kuikabili rushwa kwa vitendo badala ya maneno na ahadi tupu.

Sasa kabla hata sheria hiyo haijapata nafasi ya kutumika ipasavyo,JK kaja na hadithi mpya.Kwa mujibu wa vyombo vya habari,Rais amewaeleza viongozi wa dini kuwa suala la takrima kwenye chaguzi ni gumu kulidhibiti.Kama huelewi vizuri maana ya takrima basi naomba nikugamishe kuwa hiyo ni jina la kistaarabu (polite name) la rushwa au hongo wanayotoa wagombea kwa kisingizio cha 'ukarimu'.
Kinachonifanya nishindwe kumuelewa JK ni hiki: ina maana wakati anaipigia chapio sheria anayoamini itadhibiti rushwa kwenye chaguzi alikuwa hafahamu kuwa takrima (ambayo ni rushwa) ni ngumu kudhibitiwa? Au tuseme JK haamini kuwa takrima ni rushwa na ndio maana iliharamishwa?Na je kama takrima ni ngumu kudhibitiwa kwahiyo inakuwa halali?Je kiongozi wetu huyu haoni kuwa mkanganyiko anaozua unaweza kupelekea mvurugano baada ya uchaguzi ambapo wagombea watakaoshindwa kutokana na uwezo wao duni kumudu kutoa takrima wakikimbilia mahakamani,watoa rushwa (takrima) watatumia kauli ya JK kuhalalisha kuwa walichofanya ni sehemu ya utamaduni wetu wa ukarimu ("kama alivyobainisha Rais tarehe 14/05/2010)?

Habari kamili kuhusu kauli hiyo ya JK soma HAPA na HAPA.

1 comment:

  1. Huyo ndiyo rais mwenye "personality mbili za uongozi...Kwanza ndiyo mtu wa mwisho kupitisha sheria za nchi na pia ndiye anyeshabikia kuzivunja kwa sababu yeye ndiyo mtu mwenye wazifa wa juu kabisa ktk mahamuzi ya serikali ya Jamhuri ya Tanzania....Angalia Chenge, Mkapa wote wanafurahia taratibu hizo zake kwa sababu ndizo zinawafanya kuwa huru mtaani kufurahia maisha ya uvunjaji sheria bila kuadhibiwa na sheria zilizopo..

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.