29 Dec 2010



Sijaamini macho yangu niliposoma habari kuhusu hukumu iliyotolewa na mahakama dhidi ya Mbunge wa Bariadi (CCM) Andrew Chenge a.k.a Mzee wa Vijisenti ambapo licha ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya watu wawili na makosa manne ya barabarani,amehukumiwa faini ya SHILINGI LAKI SABA!And as you would have expected,AMELIPA NA KESI KWISHNEY.

Pengine hakimu aliyetoa hukumu hiyo alikuwa hajatoa zawadi ya Krismas kwa bosi wake mpya,Jaji Mkuu Othman.Au pengine hakimu huyo aliona hukumu hiyo ni fursa nzuri ya kutoa salamu za mwaka mpya kwa Watanzania in form of a prank.Au labda hakimu huyo amezingatia kanuni isiyo rasmi inayotawala sheria za Tanzania kwamba wanaostahili kwenda jela ni walalahoi tu,vigogo wanapokutwa na hatia wanapaswa kunyenyekewa kwa kila hali.Na pale inapobidi kutoa hukumu ya "changa la macho",matokeo yake ndio hukumu kama hii aliyopewa Chenge.

Ungetegemea mtu kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema kukata rufaa dhidi ya hukumu hii ya mzaha.Lakini atapata wapi muda huo wakati yuko bize kuhakikisha majambazi wa Dowans wanalipwa mabilioni yao?Na ungetegemea makundi ya haki za binadamu yashikilie bango hukumu hii lakini you and I know better kuwa generally speaking civil society Tanzania ni imegeuka mradi kwa wajanja (wezi?) kuwaghilibu wafadhili waendelee kumwaga misaada,ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kuongeza idadi ya mahekalu,magari ya kifahari na nyumba ndogo za wenye NGOs hizo.

Ukiwa Mtanzania,unapaswa kuielewa vema Tanzania.No,simaanishi utafute vitabu vya Jiografia,Historia au Elimu ya Uraia kuhusu Tanzania.Ninachomaanisha ni kwamba unapaswa kuishi katika uhalisia na kufahamu kwamba kuna Tanzania ya aina mbili: ile masikini ya kupindukia ya walalahoi,na ile ya wenye ma-Vogue,X8,Hummer,nk.Pia kuna Tanzania ya wezi wa kuku wanaozeekea jela wakati uchunguzi unaendelea,au wanaobambikiwa kesi kwa vile hawamudu kuwahonga polisi mafisadi,na Tanzania ya akina Chenge ambao hata wakigonga na kuua kwa magari yenye bima iliyoisha muda wake wanaishia kupewa faini ya kishkaji la shilingi laki saba!Pia tuna Tanzania ya wanausalama kuhaha huku na kule (huku wakitumia mamilioni ya fedha za walipa kodi) kuandama maisha binafsi ya wanasiasa kama Dokta Wilbroad Slaa,na ile Tanzania ya wanausalama wanaotweta kuhakikisha mmiliki wa Kagoda anaendelea kuwa SIRI KUU.Na tuna Tanzania ambayo ni haramu kuandamana kudai Katiba mpya au kumpongeza mbunge wa chama cha upinzani,na ile ambapo kauli yoyote ya kiongozi wa CCM (hata kama ameitoa ndotoni au akiwa chakari baa)inageuzwa wimbo wa Taifa.

Inachukiza kuona miaka 49 baada ya uhuru wetu,Tanzania inazidi kugeuzwa punching bag na shamba la bibi la mafisadi.Ufisadi unatapakaa kila kona.Na mahakama zetu hazitaki kuachwa nyuma katika mchezo huo mchafu.Ndio maana sikushangazwa na kauli ya kitoto ya Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani kuwa baadhi ya hukumu za majaji zina walakini (na alisubiri astaafu kwanza kisha ndio atoe kilio.Nchi ya rambirambi!).Actually,Jaji Ramadhani alipata fursa adimu ya kuingizwa kwenye vitabu vya historia pale aliposhiriki katika hukumu ya mgombea binafsi.Lakini tungetarajia nini kuyoka kwa wateuliwa ambao utiifu wao uko zaidi kwa aliyewateua kuliko nchi wanayoitumikia?

Nimalize kwa maneno makali.Kuna roho mbili za Watanzania wasio na hatia zilizopelekwa kaburini na Chenge.Kwa lugha nyingine,Chenge alijikabidhi jukumu la Ziraili mtoa roho.Hakimu aliyetoa hukumu hii ya mzaha anafahamu fika kuwa haki haionekani kutendeka japo imetendeka katika hukumu hiyo ya kihuni.Mungu atawalaani washiriki wote katika suala hili.Atawaadhibu ipasavyo kwa kupuuza thamani ya maisha ya marehemu hao wawili.Yawezekana huko waliko wanateseka kusikia thamani ya uhai wao ni shilingi laki saba (inclusive of makosa mengine ya Chenge).Of course,hata kama Chenge angehukumiwa fedha zote za akaunti yake huko Jersey isingetosha kufidia maisha ya marehemu hao,lakini alistahili japo kifungo cha muda mfupi.Lengo la hukumu kali ni kutoa fundisho kwa wazembe na wahalifu.Huruma au mzaha kwa wavunja sheria inachangia sana kukomaza uvunjaji sheria.Ikumbukwe kuwa hukumu hiyo inaweza kutumika katika kesi nyingine kuepisha adhabu kali kwa dereva mwingine atakayegonga na kuua ( hususan kama anatoka Tanzania ya vigogo).

Ee Mola,wewe ni mwenye huruma na mtoa haki ya kweli.Blogu hii inakuomba utoe hukumu mbadala ambayo angalau itaweza kuonyesha kuwa haki sio tu imetendeka bali pia inaonekana imetendeka.Katika Wewe kila jambo linawezekana.Kwa Chenge na hakimu wako,kwa hakika ipo siku mtavuna mlichopanda katika mzaha wenu huu wa mwisho wa mwaka

3 comments:

  1. Well said. Pamoja nakwamba sijasomea field ya sheria, naamini wakati wote Hakimu au Jaji anapotoa hukumu: pamoja nakuhakikisha hapingani na sheria, lakini pia adhabu yake inakusudia kutoa fundisho kwa mtuhumiwa na wengine ili tukio kama hilo lisitokee tena au watu wajifikirie kabla yakutenda. I wonder wakati ajali inatokea Chenge alikua sober au vipi? Je polisi walipima level ya alcohol that night? Kwa mazingira yanavyoonyesha the whole process ilitengenezwa toka mwanzoni. Ivi kweli mtu anayemiliki bajaji anaweza akakimbia asionekane? Yaani gari imeumia vibaya vile alafu dereva wa bajaji amepona nakuweza kukimbia? Kwani mmiliki halali wa bajaji ni nani? Ameshindwa kusaidia polisi ili dereva wake apatikane? Yaani hii inaonyesha the whole process hadi hapa tulipofika ni maigizo. Kuna mtu wakaribu na Chenge alisema Chenge alikwenda mahakamani akijua kabisha how much he is going to pay!!!Lakini kwani tulitegemea jipya kweli kwenye serikali yenye uozo namna hii? Na jaji Ramadhani amegeuka kuwa kichekesho namuomba tu asiongee maana it is better for him to remain quite amasivyo tutafufua uozo aliouangalia na kufanya alipokua kwenye nafasi yake.Ninakusanya data zakutosha kuonyesha ni jinsi gani vyeti/leseni za ku-practice uwakili zilivyotolewa kwa watu fulani fulani bila wao kutimiza masharti (kufanya mtihani etc) huku Jaji Ramadhani akiwa analitambua nakuliangalia hilo. Kwakweli naamini kabisa huyu jaji mkuu mpya amewekwa kwa maslahi fulani. Inawezekana sio udini bali nikulinda maslahi ya watu fulani hivi. Hivi kweli kuanzia J1 mpaka J10 hakuna aliyekua anafaa mpaka tukachagua J11? Yaani hao wote walikua promoted kimakosa kwenye nafasi zao? Mbaya zaidi mtu ambaye ana-less experience na court system ya Tanzania tunamkabidhi majukumu makubwa wakati nchi ikokwenye mgawanyiko mkubwa hasa kwenye mambo ya katiba na mikataba mibovu? Nimejaribu kutafuta any controversial cases alioisikiliza sijapata naona alikua anatoa ushauri tu kwenye level yakimataifa. Au na yeye atahitaji few years zaku-learn usanii wa bongo then ndio aanze kazi? Nachukia ku-prejudge vitu lakini nahisi hali ya hewa sio nzuri kwa miaka inayokuja jinsi mambo yanavyokwenda.Naona drama imeshaanza kwa mwanasheria wa Serikali na Dowans. MORE IS TO COME MY FRIENDS!

    ReplyDelete
  2. JK hawezi kukupatia cheo iwapo wewe siyo fisadi au kuwa kimya kupinga lolote analoagiza....haya madudu yote kiuongozi na utawala lazima yanakuwa na chanzo chake na bila shaka ni yeye JK ndiyo yupo nyuma ya yote haya mafinyufinyu

    ReplyDelete
  3. Hapa fundisho lipo na ni kwamba kama una pesa basi wewe unaweza kuharibu unavyotaka. Kwa tabia ya Tanzania hili ukisoma ripoti ya judge warioba kuhusu corruption utakubaliana na mimi, huyu mhalifu(mfungwa aliyehuru) atakuwa amelipa pesa nyingine nyingi ili kutengenezewa adhabu hii.
    Sasa wale wasomi wa sheria, hivi hawa wafiwa hawawezi kufungua kesi ya madai, kama familia ya mke wa O.J Simpson? na wakalipwa pesa kwani nilishawahi kusoma kuwa hawa wadada walikuwa na majukumu kwenye familia zao.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.