Showing posts with label CHENGE. Show all posts
Showing posts with label CHENGE. Show all posts

23 Jul 2011


Hili sio ombwe tena bali mkusanyiko wa wababaishaji walioteuliwa na mtu asiyejua kwanini aliwateua,na ndio maana wanaendesha mambo kama kwenye mchezo maarufu wa watoto ujulikanao kama kombolela.Watu wazima ovyoo!Lakini ni wazi wanapata jeuri ya kufanya ubabaishaji huo kwa vile wanafahamu fika kuwa aliyewateua hana jeuri ya japo kuwawajibisha,let alone kuwakemea.

Anyway,hebu soma madudu yao hapa chini:

DPP amkana Hoseah  
Friday, 22 July 2011 20:27

ASEMA HAJAPATA JALADA LA CHENGE, AAMBIWA AKAANGALIE MASJAJA
Nora Damian
SIKU moja baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, kusema kwamba ofisi yake imekamilisha uchunguzi wa madai ya kumiliki Dola za Marekani 1.2 milioni katika Kisiwa cha Jersey, Uingereza yanayomkabili Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), Andrew Chenge na kwamba imekabidhi faili lake kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kwa ajili ya kumfungulia mashtaka, kiongozi wake, Eliezer Feleshi amejitokeza na kusema kwamba hawahi kuliona jalada hilo.

"Niko safarini subiri hadi wiki ijayo… kwanza ashtakiwe kwa kosa gani? Acheni siasa nyie,” alisema DPP alipotakiwa kuthibitisha kama jalada hilo limefika mezani kwake na lini Mwanasheria huyo Mkuu wa zamani wa Serikali atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili... “Aseme ni tarehe gani alileta jalada hilo kwangu?”

Kutokana na majibu hayo ya DPP, Mwananchi lilimtafuta Dk Hoseah kupata ukweli juu ya kauli yake hiyo aliyoitoa juzi huko Arusha na kusisitiza kuwa jalada hilo limepelekwa katika Ofisi ya DPP na kumtaka mkuu huyo wa Mashitaka nchini asiharakishe kusema hajaliona, kwani siyo lazima kila kitu akabidhiwe mikononi... “Kwani kila kitu kinachopelekwa kwake lazima akione? Ameangalia registry (masjala)?. Suala hili nimeshaliongea nanyi vya kutosha hivyo muulizeni zaidi DPP.”

Juzi, Dk Hoseah alisema taasisi yake imekamilisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazomkabili Chenge na kwamba jalada lake limepelekwa kwa DPP kwa hatua zaidi. Alisema Chenge atashtakiwa chini ya Kifungu cha 27 cha Sheria ya Takukuru ya mwaka 2007. Kwa mujibu wa kifungu hicho, mtu akiwa na mali ambazo hazilingani na kipato chake alichokipata akiwa madarakani au baada ya kuondoka ni kosa kisheria.

Chenge anadaiwa kukutwa na kiasi hicho cha fedha mwaka 2008 baada ya uchunguzi wa kashfa ya ununuzi wa rada uliofanywa na Taasisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO). Tuhuma hizo ndizo zilizomfanya alazimike kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu mwaka huo.

Malumbano kati ya Dk Hoseah na Feleshi siyo ya kwanza. Mwaka jana waliwahi kulumbana baada ya mkuu huyo wa Takukuru kusema kuna majalada takriban 50 ya kesi za rushwa ambayo yamekaliwa na DPP.

Pia Dk Hoseah aliwahi kumshutumu DPP mbele ya wabunge wakati wa semina elekezi mapema mwaka huu akidai kwamba amekuwa kikwazo cha kesi kubwa za ufisadi kupelekwa mahakamani kwa kukwamisha majalada.

CHANZO: Mwananchi 

29 Dec 2010Sijaamini macho yangu niliposoma habari kuhusu hukumu iliyotolewa na mahakama dhidi ya Mbunge wa Bariadi (CCM) Andrew Chenge a.k.a Mzee wa Vijisenti ambapo licha ya kutiwa hatiani kwa mauaji ya watu wawili na makosa manne ya barabarani,amehukumiwa faini ya SHILINGI LAKI SABA!And as you would have expected,AMELIPA NA KESI KWISHNEY.

Pengine hakimu aliyetoa hukumu hiyo alikuwa hajatoa zawadi ya Krismas kwa bosi wake mpya,Jaji Mkuu Othman.Au pengine hakimu huyo aliona hukumu hiyo ni fursa nzuri ya kutoa salamu za mwaka mpya kwa Watanzania in form of a prank.Au labda hakimu huyo amezingatia kanuni isiyo rasmi inayotawala sheria za Tanzania kwamba wanaostahili kwenda jela ni walalahoi tu,vigogo wanapokutwa na hatia wanapaswa kunyenyekewa kwa kila hali.Na pale inapobidi kutoa hukumu ya "changa la macho",matokeo yake ndio hukumu kama hii aliyopewa Chenge.

Ungetegemea mtu kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema kukata rufaa dhidi ya hukumu hii ya mzaha.Lakini atapata wapi muda huo wakati yuko bize kuhakikisha majambazi wa Dowans wanalipwa mabilioni yao?Na ungetegemea makundi ya haki za binadamu yashikilie bango hukumu hii lakini you and I know better kuwa generally speaking civil society Tanzania ni imegeuka mradi kwa wajanja (wezi?) kuwaghilibu wafadhili waendelee kumwaga misaada,ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kuongeza idadi ya mahekalu,magari ya kifahari na nyumba ndogo za wenye NGOs hizo.

Ukiwa Mtanzania,unapaswa kuielewa vema Tanzania.No,simaanishi utafute vitabu vya Jiografia,Historia au Elimu ya Uraia kuhusu Tanzania.Ninachomaanisha ni kwamba unapaswa kuishi katika uhalisia na kufahamu kwamba kuna Tanzania ya aina mbili: ile masikini ya kupindukia ya walalahoi,na ile ya wenye ma-Vogue,X8,Hummer,nk.Pia kuna Tanzania ya wezi wa kuku wanaozeekea jela wakati uchunguzi unaendelea,au wanaobambikiwa kesi kwa vile hawamudu kuwahonga polisi mafisadi,na Tanzania ya akina Chenge ambao hata wakigonga na kuua kwa magari yenye bima iliyoisha muda wake wanaishia kupewa faini ya kishkaji la shilingi laki saba!Pia tuna Tanzania ya wanausalama kuhaha huku na kule (huku wakitumia mamilioni ya fedha za walipa kodi) kuandama maisha binafsi ya wanasiasa kama Dokta Wilbroad Slaa,na ile Tanzania ya wanausalama wanaotweta kuhakikisha mmiliki wa Kagoda anaendelea kuwa SIRI KUU.Na tuna Tanzania ambayo ni haramu kuandamana kudai Katiba mpya au kumpongeza mbunge wa chama cha upinzani,na ile ambapo kauli yoyote ya kiongozi wa CCM (hata kama ameitoa ndotoni au akiwa chakari baa)inageuzwa wimbo wa Taifa.

Inachukiza kuona miaka 49 baada ya uhuru wetu,Tanzania inazidi kugeuzwa punching bag na shamba la bibi la mafisadi.Ufisadi unatapakaa kila kona.Na mahakama zetu hazitaki kuachwa nyuma katika mchezo huo mchafu.Ndio maana sikushangazwa na kauli ya kitoto ya Jaji Mkuu mstaafu Agostino Ramadhani kuwa baadhi ya hukumu za majaji zina walakini (na alisubiri astaafu kwanza kisha ndio atoe kilio.Nchi ya rambirambi!).Actually,Jaji Ramadhani alipata fursa adimu ya kuingizwa kwenye vitabu vya historia pale aliposhiriki katika hukumu ya mgombea binafsi.Lakini tungetarajia nini kuyoka kwa wateuliwa ambao utiifu wao uko zaidi kwa aliyewateua kuliko nchi wanayoitumikia?

Nimalize kwa maneno makali.Kuna roho mbili za Watanzania wasio na hatia zilizopelekwa kaburini na Chenge.Kwa lugha nyingine,Chenge alijikabidhi jukumu la Ziraili mtoa roho.Hakimu aliyetoa hukumu hii ya mzaha anafahamu fika kuwa haki haionekani kutendeka japo imetendeka katika hukumu hiyo ya kihuni.Mungu atawalaani washiriki wote katika suala hili.Atawaadhibu ipasavyo kwa kupuuza thamani ya maisha ya marehemu hao wawili.Yawezekana huko waliko wanateseka kusikia thamani ya uhai wao ni shilingi laki saba (inclusive of makosa mengine ya Chenge).Of course,hata kama Chenge angehukumiwa fedha zote za akaunti yake huko Jersey isingetosha kufidia maisha ya marehemu hao,lakini alistahili japo kifungo cha muda mfupi.Lengo la hukumu kali ni kutoa fundisho kwa wazembe na wahalifu.Huruma au mzaha kwa wavunja sheria inachangia sana kukomaza uvunjaji sheria.Ikumbukwe kuwa hukumu hiyo inaweza kutumika katika kesi nyingine kuepisha adhabu kali kwa dereva mwingine atakayegonga na kuua ( hususan kama anatoka Tanzania ya vigogo).

Ee Mola,wewe ni mwenye huruma na mtoa haki ya kweli.Blogu hii inakuomba utoe hukumu mbadala ambayo angalau itaweza kuonyesha kuwa haki sio tu imetendeka bali pia inaonekana imetendeka.Katika Wewe kila jambo linawezekana.Kwa Chenge na hakimu wako,kwa hakika ipo siku mtavuna mlichopanda katika mzaha wenu huu wa mwisho wa mwaka

17 Jun 2009


Ni dua pekee linaloweza kubadili viumbe wa aina hii.Sijui ni kujikomba,sijui uhaba wa tafakari au...!!!Soma kwanza stori hii kisha utafakari

Chenge asimikwa utemi

na Sitta Tumma, Magu

MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge, ambaye amekuwa akiandamwa na kashfa mbalimbali, ametawazwa kuwa mtemi wa kabila la Wasukuma-Bagole, Kanda ya Itilima, wilayani Bariadi.

Chenge alichaguliwa katika sherehe maarufu za kabila hilo, maarufu kama Bolabo, mwishoni mwa wiki, wilayani hapa, ambazo mbali naviongozi wa kimila, Mkuu wa Mkoa, Abbas Kandoro, alikuwa ni miongoni mwa waliohudhuria.

Baadhi ya watu waliokuwepo kwenye sherehe hizo, waliuelezea utemi wa Chenge kwa mtazamo tofauti, huku baadhi wakidai kaupata ili kuweka mambo yake sawa, na wengine wakidai anastahili kupata nafasi hiyo kwa kuwa ni miongoni mwa watu wa kabila hilo.

Mbunge huyo ambaye alilazimika kujiuzulu nafasi yake ya uwaziri alisema, utemi huo ni karama aliyopewa na Mungu na kwamba wajibu huo ni sawa na daraja la kuunganisha jamii ya kabila husika.

"Utemi niliopewa naweza kusema ni karama iliyotoka kwa Mwenyezi Mungu! Kazi hii ya utemi ni nzito kwa sababu ina masuala yake yanayohusiana na mambo ya kimila pamoja na kuunganisha jamii ya kabila husika," alisema Chenge.
Ndio maana wakati mwingine hawa "wazungu" wanapata wakati mgumu kutuelewa.Hivi inaingia akilini kweli kwa mtuhumiwa wa ufisadi wa zaidi ya shilingi bilioni moja,Mzee wa Vijisenti Andrew Chenge,kutunikiwa utemi?Watoto wanaozaliwa leo na kesho na kukuta mtemi wao ni miongoni mwa watu waliochuma utajiri kwa njia za miujiza kabisa (fedha alizonazo haziwezi kuwa zimepatikana kwa njia halali,piga ua) watawaelewa kweli wazazi wao?

Mtemi wa nini?Au wanamaanisha utemi wa kuifanya sheria imwogope?Maana kesi yake ya kuua ni vituko vitupu.Mara iundiwe tume,mara iahirishwe kwa hili na lile!Mtu kasababisha ajali huku gari ikiwa na bima iliyoisha muda wake,mnamuundia tume ya nini?Na kwanini hiyo tume iwe kimya kama haikuundwa vile?

Mtuhumiwa huyu wa ufisadi ameendelea pia kuwa kwenye kamati ya maadili ya CCM.Halafu ukisema CCM chama cha kifisadi kuna waungwana wananuna!

Kaaazi kwelikweli

30 Mar 2009

HAYA NI MAONI YA NDUGU YANGU,BLOGA MWENZANGU DAVID MUSIKA.NAYAWASILISHA KAMA YALIVYO

ajali ngapi zilizowahi kutokea bila kuundiwa tume ya uchunguzi kwani hii ina nini? tena watu walikufa ni wawili tu! kule arusha,Tanga watu wangapi walikufa katika ajali na hatukusikia tume? kuna nini kinataka kufichwa hapa? kwanza kabisa inabidi chenge awe jela kwa kuendesha gari bila bima ya gari kwa miaka 2! ebu fikiria ungekuwa wewe unaedesha bila bima ya gari wacha kupata ajali? nahisi bado tanzania hatuna usawa!mbona yule kijana aliyemuua chacha wangwe hakupewa dhamana? au tuseme hao marehemu ndiyo walioua chenge katika ajili hiyo wangepewa dhamana? jamani lazima tutenda haki kwa kila mtanzania kwa vile ni haki ya mtanzania kuwa na haki katika nchi yake.kumwachia mzee chenge huru ni kuendeleza matabaka ya walionacho na wasio nacho. .

NAAMINI WAPENDA HAKI WOTE WANAUNGA MKONO MTIZAMO WA MR MUSIKA.HAKI SHURTI ITENDEKE PASIPO KUANGALIA MATABAKA.
(Pichani juu ni siku Chenge alipopokelewa kishujaa jimboni kwake baada ya kulazimika kujiuzulu kufuatia tuhuma za kumiliki vijisenti huko Jersey,UK.Unaweza kujiuliza inakuwaje watu wenye akili zao timamu wajazane namna hiyo kumlaki mtuhumiwa wa ufisadi.....jibu la swali hilo linaweza kutoa mwangaza wa namna vita ya ufisadi ilivyo ngumu,hususan kwenye kuondoa mentality ya kuwaenzi white-collar criminals).

29 Mar 2009

(Picha kwa hisani ya KENNEDY)

Gazeti la Majira limepotea mtandaoni kwa muda mrefu sasa,na kwa akina sie tunaotegemea habari za nyumbani kupitia nakala za kielektroniki za magazeti husika mkombozi wetu mkuu amebaki Mr Kennedy.Na ni kwa kupitia tovuti yake ndipo nilikutana na version isiyopendeza ya habari kuhusu ajali iliyomhusisha Mzee wa Vijisenti,Andrew Chenge,na kupelekea vifo vya akinadada wawili.

Gazeti la Majira lilidai kuwa marehemu hao ni "machangudoa waliokuwa wanatokea Maisha Club".Sijui vyanzo (sources) vyao vya habari husika ni vipi lakini mwandishi yeyote mwenye busara angepaswa kujiridhisha kuhusu identity halisi ya marehemu hasa kwa vile tunazungumzia watu waliopoteza maisha.Hivi mwandishi huyo atajisikiaje iwapo baada ya uchunguzi itagundulika kuwa marehemu hao hawakuwa machangudoa?In fact,magazeti kadhaa yameripoti maelezo ya ndugu za marehemu yanayoeleza kwamba mmoja wao alikuwa mfanyabishara na mwingine mfanyakazi wa hoteli jijini Mwanza.

Pengine haikuwa nia ya mwandishi kuwa-describe marehemu hao kama changudoa (labda kutokana na haraka ya kuwahisha habari kwa mhariri) lakini taswira ya haraka iliyopatikana kutoka katika habari hiyo ni ujenzi wa matabaka:kigogo (mzee wa vijisenti) kagonga fukara (changudoa).By the way,hata hata kama hao mabinti wangekuwa machangudoa as suggested by the Majira reporter bado haiondoi haki yao ya kuwa hai muda huu!

Kingine ambacho hakihusiani na uandishi japo kinahusu tukio hilo la kusikitisha ni namna Jeshi la Polisi linavyoonekana "kubabaika" katika kushughulikia ajali hiyo.Kwa mujibu wa vyombo vya habari,Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova,ameunda TUME MAALUM ya kuchunguza ajali hiyo eti kwa "kuzingatia uzito wa tukio hilo".Chenge ni Mtanzania kama mie na wewe,na kama amehusika na ajali basi sheria za uslama barabarani zifanye kazi yake.Sijui ni madereva wangapi walalahoi wanaopata "bahati" kama ya Chenge ya kuundiwa tume!

Kamanda Kova anadai kuwa tume hiyo imeundwa ili "kusiwepo mwanya wowote ,taratibu zote zitafuatwa bila kujali nani na wala nafasi aliyonayo....na kuleta uwazi na utawala bora" (kwa mujibu wa gazeti la Majira) na pia amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema kuwa "hapa bwana hakuna mchezo wala hakuna kuangalia vyeo wala nani ni nani...".Hivi matamshi kama hayo (iwapo kesi itapelekwa mahakamini) hayawezi kutumiwa na wakili wa Chenge kudai "ameonewa kwa vile Kamanda Kova alishadai hawataangalia vyeo-which directly points to Chenge ambaye licha ya kuwa ex-minister,pia ni munge na kigogo wa CCM?"

Kama nilivyoandika jana,tuendelee kuwapa polisi benefit of doubt kwa matarajio kwamba wanafahamu bayana kuwa tukio hilo linaangaliwa na Watanzania wengi kama kipimo cha haki sawa kwa wote (huku wakiwa na kumbukumbu ya kesi ya marehemu Ditto).

28 Mar 2009


Aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge (61), amewekwa chini ya ulinzi katika Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar es Salaam, kwa zaidi ya saa saba baada ya kuhusishwa na ajali ya gari na bajaj ambayo imeua watu wawili. Waliokufa ni wanawake wawili ambao ndugu amejitokeza na kudai kuwa wote ni wageni, waliwasili juzi Dar es Salaam kutoka Mwanza na mmoja alikuwa njiani kwenda Zanzibar kuolewa. Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, ajali hiyo ilitokea saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia jana wakati Chenge akiendesha gari namba T 512 ACE aina ya Toyota Hilux na kuigonga bajaj hiyo namba T 736 AXC iliyokuwa na abiria hao wawili wanawake.

Chanzo hicho kilidai kuwa baada ya ajali hiyo, Chenge alikwenda kwanza nyumbani kwake na kuripoti kituoni hapo saa moja asubuhi jana na kuwekwa chini ya ulinzi na kuhojiwa hadi saa saba mchana, huku nje akisubiriwa na ndugu zake. Gazeti hili lilimshuhudia mbunge huyo wa Bariadi Magharibi akiingizwa kwenye gari la Polisi namba PT 0217 na kwenda eneo la tukio karibu na shule ya msingi ya Oysterbay katika makutano ya barabara za Karume na Haile Selassie, ambako alieleza namna ajali hiyo ilivyotokea.

Wakati mbunge huyo akitolewa katika kituo cha Polisi, kulitokea vurugu baina ya ndugu zake na waandishi wa habari, ndugu hao wakitaka kuzuia Chenge kupigwa picha, hali iliyosababisha kusukumana na kurushiana maneno makali. “Ninyi mmezidi kumwonea huyu kwani ni lazima mumpige picha ndio muuze? Hebu tokeni hapa,“ alisikika mwanamke ambaye alikuwa mstari wa mbele kusukuma waandishi, huku akilia na almanusra wapigane na mmoja wa wapigapicha waliokuwa kazini.

Hata hivyo, vurugu hizo zilimalizika baada ya waandishi kuwazidi nguvu ndugu hao na kung’ang’ania kumpiga picha mbunge huyo ambaye awali alikuwa akifunikwa magazeti na nduguze, lakini aliyatoa na kupisha waandishi wampige picha vizuri. Akiwa katika eneo la tukio, Chenge alimwelezea Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Peter Kivuyo, namna ajali hiyo ilivyotokea na alidai ilitokea baada ya bajaj hiyo kutaka kupita gari jingine kwa kasi.

“Bajaj ile ilikuwa inataka kupita gari jingine lililokuwa likitoka Morogoro Stores, bahati mbaya kukawa na gari lingine linakuja, ile bajaj ikabana upande wangu na mimi nilikuwa katika mwendo wa kati ya kilometa 80 hadi 100 kwa saa,“ alidai Chenge. Alidai kuwa baada ya kuona bajaj ile inakwepa gari la mbele wasigongane uso kwa uso, alirudi upande wa kulia ndipo alipoigonga ubavuni kushoto. "Gari la nyuma lingesimama, dereva wake angeweza kueleza vizuri, ila baada ya ajali nikasikia watu wanaita 'Chenge! Chenge!’ nikajua niko salama, nikashuka,“ alidai.

Aliendelea kudai kuwa aliposhuka, alikuta abiria wawili wanawake wakiwa bado wanapumua ingawa kwa shida, lakini walipofika trafiki hali zao zilizidi kuwa mbaya na katika kipindi hicho chote, dereva wa bajaj alikuwa haonekani. Naye askari wa usalama barabarani aliyefika katika ajali hiyo, Mustafa Salum, alimweleza Kivuyo juu ya tukio hilo, ambapo alisema alipata taarifa za ajali hiyo saa 10.30 alfajiri na alipofika eneo la tukio, alikuta tayari abiria hao wawili wameshafariki dunia. “Niliipeleka miili ya marehemu hospitali ya Mwananyamala, ila kwa mujibu wa watu waliokuwa eneo la tukio, waliowaona marehemu hao wawili katika ukumbi wa Maisha Club,“ alisema.

Naye kaka wa mmoja wa marehemu hao, January Constantine, alisema alipata taarifa za kifo cha dada yake, Beatrice Constantine (34) asubuhi na alikwenda kutambua mwili wake hospitalini, lakini kutokana na alivyopondeka alimtambua kwa alama za mwili. Alisema dada yake ni mfanyabiashara na mkazi wa Mwanza na kwamba aliwasili Dar es Salaam, akiwa na rafiki yake huyo na ilikuwa aondoke jana alfajiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya harusi ya rafiki yake huyo. Gazeti hili lilishuhudia gari la Chenge kwa mbele likiwa na damu, nywele na mabaki ya ubongo ambao unasadikiwa kuwa wa mmoja wa marehemu hao. Polisi pia iliokota kipande cha fuvu la mtu katika eneo la tukio.

Gari hilo lilikuwa na stika ya Bima ambayo ilikatwa Juni 6, 2006 na kumaliza muda wake Juni 6, mwaka juzi. Naye Theopista Nsanzugwanko anaripoti kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleiman Kova, alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema mmiliki wa bajaj hiyo ni Zuwena Nassoro na anatakiwa kuripoti katika kituo chochote cha Polisi huku wakiwa wanamshikilia Chenge Oysterbay ili kuisaidia Polisi. Alisema uchunguzi wa tukio hilo unafanywa chini ya Kivuyo na wataalamu mbalimbali ili kuondoa dhana ya upendeleo kwa kuwa Chenge ni mtu maarufu.

Chenge (62) alijiuzulu uwaziri wa miundombinu Aprili 20 mwaka jana, kutokana na kashfa ya rushwa ya dola milioni moja kutoka kampuni kubwa ya uuzaji vifaa vya kijeshi duniani ya BAE Systems. Alijiuzulu baada ya kudaiwa kupokea rushwa ili kuwezesha ununuzi wa rada ya kijeshi ya pauni milioni 20 za Uingereza na kwamba fedha hizo ziliwekwa katika akaunti yake ya kisiwa cha Jersey.

Baada ya kujiuzulu, alikaririwa akisema pamoja na tuhuma hizo, mapenzi kwa nchi yake na chama chake, ndivyo vilimlazimisha achukue uamuzi huo na kuongeza kuwa fedha zilizokutwa katika akaunti yake hiyo hazina uhusiano wowote na BAE Systems. Tuhuma hizo za rushwa zilichochea kelele pale alipohojiwa na waandishi wa habari na kujibu kuwa fedha anazotuhumiwa nazo ni 'vijisenti (fedha kidogo)'.

CHANZO: HabariLeo

I SMELL DITOPILE-LIKE ADMINISTRATION OF JUSTICE......KWA UBINADAMU WA KAWAIDA TU,GARI LAKO LIKIHUSIKA KATIKA AJALI INAYOPELEKEA HATARI YA MAISHA YA MAJERUHI PRIORITY INAKUWA KWENYE KUOKOA MAISHA YA MAJERUHI HAO (KWA MUJIBU WA HABARI HII MZEE WA VIJISENTI ALIKWENDA ZAKE NYUMBANI HADI SAA 1 ASUBUHI ALIPORIPOTI KITUO CHA POLISI NA KUHOJIWA KWA MASAA 7-(DOES IT REALLY MATTER HOW LONG THE INTERROGATION LASTED WHEN TWO PEOPLE HAD ALREADY LOST THEIR LIVES?).

ANYWAY,LET'S GIVE THE POLICE A BENEFIT OF DOUBT HOPING THAT THIS TIME HAKUTAKUWA NA USANII KAMA KATIKA ISHU YA MAREHEMU DITO.

21 Apr 2008

Bilionea mwenye vijisenti,Andrew Chenge amejiuzulu,na Braza Ditto amefariki.Hizo ndizo habari zinazovuma hapa Dar tangu asubuhi.Hii ya kifo cha Ditto niliisikia jana.Na kama ilivyo kawaida,kila mmoja anasema lake ila kwa vile blogu hii si ya udaku,naomba nisiorodheshe conspirancy theories lukuki zinazovuma hapa jijini.Anyway,kuna picha kadhaa nilizozikamata maeneo mbalimbali.Nyingi zinajieleza zenyewe
KIZA KWENYE PLATFORM YA TAZARAHAPO JUU NI CHOO CHA FIRST CLASS CABIN TAZARA

HAPO JUU NI BUFFET COACH TAZARAHUYO UTINGO KAZI YAKE NI KUSHUKA KWENYE FOLENI NA KUWEKA GOGO ILI LORI LISIGONGE MAGARI YA NYUMA.KWA HAKIKA UDEREVA WA BOGNO UNAHITAJI ZAIDI YA LESENI:SALA NA BAHATI NI MUHIMU PIA KUHAKIKISHA UNAMALIZA SALAMA SIKU YAKO BARABARANI.THE SAME LORRY BELOW.
HAPO JUU NA CHINI NI KIZA KWENYE PLATFORM YA TAZARA.


HAPO CHINI NI ENEO LA MIZIGO TAZARA


HAPO CHINI NI KITUO CHA MAFUTA MTANI.VIKO LUKUKI LAKINI BEI INAZIDI KUPAA.INAWEKEKANA ILE KANUNI YA DEMAND NA SUPPLY HAIFANYI KAZI KWENYE SUALA LA MAFUTA!

BELOW IS A LORRY TO AND FROM HELL

18 Apr 2008

Katika picha hapo chini,treni ikikatiza kwenye railway crossing hapo jana.Almanusura itokee ajali mbaya laitimzalendo mmoja asingemshtua dreva kwamba anaona moshi wa treni kwa mbali.Yaani hakuna namna kwa mwenye gari kufahamu awapo kwenye railway crossing iwapo garimoshi linakuja au la.


Picha ya chini ni kwa ajili ya tafakuru:hivi hayo maisha bora kwa kila Mtanzania yatawezekana vipi kwa mkazi wa nyumba hiyo pichani ilhani akina Chenge wanadai dola milioni moja za ufisadi ni vijisenti?Hii ndio Bongo


Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.