24 Aug 2014

 Only men who suffered impotence as a side effect of illness or those evaluated by a specialist could be given the pills on the NHS
Mamia kwa maelfu ya wanaume hapa Uingereza wanatarajiwa kunufaika na uamuzi wa Taasisi ya Huduma za Afya (NHS) kulegeza masharti ya upatikanaji wa vidonge vya kuboresha nguvu za kiume, Viagra.

Hadi mwezi huu, watu pekee walioruhusiwa kupewa Viagra hospitalini ni wale ambao pungufu wa nguvu zao za kiume ulitokana na athari za matibabu ya maradhi mengine (side effects).

Lakini tangu taratibu za usajili na upatikanaji (patent) ya Viagra ilipoisha muda wake mwaka jana, bei ya vidonge hivyo imeshuka kwa asilimia 93 kwa vile makampuni mengine ya madawa yameruhusiwa kutengeneza aina zisizo asili (generic) za vidonge hivyo.

Kutokana na hali hiyo, NHS imeeleza kuwa watu wote wenye matatizo ya nguvu za kiume wanaruhusiwa kupata Viagra. Madaktari wengi wamefurahishwa na uamuzi huo wakiamini kuwa utasaidia kuboresha mahusiano ya kinyumba na hata kuokoa ndoa.

Hadi 'patent' ya Viagra inakwisha muda wake, Viagra ilikuwa ikiuzwa kwa Paundi za Kiingereza 21.27 (Tsh 58,567.39) kwa pakti ya vidonge vinne lakini bei hiyo sasa imeshuka hadi Paundi .1.45 (Tsh 3,992.61)kwa pakti moja ya vidonge vinne.



0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.