



Mtoto wa miaka minne nchini India, Kaleem (pichani) amewachanganya madaktari kufuatia mikono yake kuvimba kupita kiasi na sasa imefikia uzito wa kilo 12. Mtoto huyo kwa sasa anashindwa kutekeleza japo majukumu madogo tu kama kufunga 'kamba' (laces) za viatu vyake baada ya kuzaliwa akiwa na mikono mikubwa mno.
Kaleem anadai amekuwa akibughudhiwa mno na watoto wenzie wanaomcheka kutokana na maumbile hayo ya ajabu. "Napata mguu kuvaa nguo zangu, kufunga vifungo hata kuvaa nguo ya ndani, anasema mtoto huyo ambaye mama yake alibaini maradhi yake tangu akiwa mdogo lakini hakuwa na cha kufanya kutokana na kutokuwa na uwezo wa kifedha. Wazazi wa Kaleem wana kipato kisichozidi Paundi za Kiingereza 15 (takriban Tsh 42,000) kwa mwezi.
Baba yake, Shamim, anahofu mwanae hatoweza kujitegemea maishani, na anajilaumu kwa kushindwa kumhudumia kutokana na uwezo duni wa kifedha. Dr Ratani, mkurugenzi wa kituo cha afya kilichomfanyia uchunguzi mtoto huyo anakiri kuwa maradhi hayo ni ya ajabu na magumu kutibika.
CHANZO: The Mail Online
0 comments:
Post a Comment