2 Jun 2016

Hivi kama umeshawahi kutishiwa kifo huko nyuma, kwa maana ya vyombo vya dola kukutaarifu kuwa maisha yako yapo hatarini, utajisikiaje ukipata barua-pepe kama hiyo niliyoiambatanisha hapo chini?

Naam, huko nyuma, nilishawahi kufahamishwa na vyombo vya usalama hapa Uingereza kuwa kuna mpango wa kunidhuru. Nilielezea kwa kirefu kuhusu tukio hilo la kutisha HAPA. Sasa mambo kama haya yakishakutokea maishani, unajifunza kutochukulia vitu kirahisi, kwa lugha nyingine, 'unakuwa unaishi kwa machale.' Sio kama inazuwia kwa asilimia 100 uwezekano wa mtu kudhuru, lakini angalau inapunguza nafasi za mwenye nia ovu.

Sasa leo naingia kwenye barua-pepe zangu nakutana na 'tishio' hili. Mwanzoni nilishtuka kidogo, maana hiyo barua pepe ina dalili nyingi za kuonyesha ni ya kweli. Nikajiambia kuwa kabla ya kukimbili kuripoti polisi, hebu niangalie anwani ya aliyeituma kwangu. Nikagundua kuwa hiyo https://goo.gl/zj173Y ni email address ya mzee mmoja mstaafu huko Marekani. 

Kisha nika-Google "I have been paid to kill you" nikabaini kuwa ni utapeli maarufu mtandaoni japo ukikumbana nao mara ya kwanza waweza kudhani ni wa kweli. Inaelezwa kuwa ukishatumiwa email ya vitisho kama hiyo, mtumaji anakuonya usiwasiliane na vyombo vya dola, na kukutaka uwasiliane nae ndani ya masaa 24. Ukijibu tu basi vitafuata vitisho zaidi, lakini pia utaambiwa uanze kufanya malipo ili kumwezesha huyo 'muuaji amuuwe mtu mwingine badala ya wewe aliyetumwa kukuuwa.' Yaani matapeli hapo wanakujengea picha uwaone kama wasamaria wema wanaookoa maisha yako.

Kwahiyo, ukipokea email kama hii, IPUUZE. USIIJIBU, maana ukiijibu tu utawapa moyo matapeli hao kukutisha zaidi. Puuza na block address ya aliyeituma (not that itasaidia ku-block, kwa sababu hao matapeli wana maelfu ya email feki). La muhimu hapa sio email bali maudhui ambayo ni UTAPELI. Kuwa makini 

Nimeona niwashirikishe wasomaji wapenda ili kesho na keshokutwa, ukikumbana na utapeli huu, usije uka-panic. Ila kwa hakika, ni vigumu kupuuza vitisho vya matapeli hawa laiti wanachotishia kishawahi kukutokea maishani.

Endelea kutembelea blogu hii kwa habari mbalimbali za teknolojia na makala nyinginezo. 

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.