15 Jan 2008

Hivi msomaji wangu mpendwa ulishaota ndoto ngapi za "ningependa kuwa flani" kabla hujafika hapo ulipo?Kwangu ni 3,moja naendelea kuhangaika nayo,na kwa Mapenzi yake Mola+jitihada zangu,natarajia kuitimiza miezi michache ijayo.Naomba niihifadhi ndoto hiyo kwa sasa.Ndoto yangu kwanza utotoni ilikuwa kuwa daktari.Sehemu ya elimu yangu ya msingi na O'level ilipatikana katika shule zilizokuwa karibu na hospitali flani yenye CV ya kuridhisha (imezaa madaktari wengi kupitia chuo cha udaktari kilichopo hapo).Kutokana na ukaribu kati ya shule na hospitali hiyo,wanafunzi walikuwa wakipendelea kwenda hapo wakati wa mapumziko ya asubuhi na mchana.Taratibu nikajikuta natamani kwamba siku moja nami niwe katika majoho meupe nikiokoa maisha ya binadamu wenzangu.Nadhani kilichonivutia zaidi kuhusu taaluma ya utatibu ni role yao katika maisha ya binadamu (well,at least sio kama wale wazembe "waliochanganya madawa" huko Muhimbili kwa kumpasua mtu kichwa badala ya mguu na vice versa).Ndoto hiyo iliyeyuka kama pande barafu kwenye maji ya moto baada ya kufeli somo la Fizikia (sioni haya kusema nilipata F japo nilikuwa na A ya Kemia).PCB ikawa imegoma hapo (nilikuwa na C ya Baiolojia).Nikapiga mahesabu ya CBG-Kemia,Baiolojia na Jiografia (ambapo "combi" ingekubali kwani nilikuwa nina A,C na B,consecutively).Ndoto ilifutika kabisa baada ya kuwasili shule nilopangiwa kusoma A'level.CBG ilikwepo lakini,kwanza shule ilikuwa haina mwalimu wa Jiografia (hivyo wanafunzi walikuwa wanalazimika kwenda shule jirani kupata mihadhara ya somo hilo).Lakini,to make matter even worse,nikaja kugundua kwamba Kemia ya A'level ni "hadithi tofauti" na ile ya O'level niliyoimudu.Did I mention kwamba niliibuka na D ya kichovu kwenye Hisabati huko O'level?Yeah I did,na Kemia ya A level imejaa "namba" (nadhani Physical Chemistry ndio balaa zaidi).Enewei,nikaamua kukimbilia kwenye HGL-Historia,Jiografia na Lugha ya Mama..Kimombo (ambayo ilikuwa na msingi mzuri wa A,B na A,consecutively huko O'level).Kilichonisaidia kuwa na options mbalimbali ni mchanganyiko wa masomo huko O'level (sayansi,sanaa na biashara) lakini ndoto ya udaktari ndio ikafa kifo cha asili.

Ndoto ya pili ilinijia nilipokuwa jeshi la kujenga taifa (JKT).Did I mention kwamba shule niliyosoma A'level nayo ilikuwa ya mchepuo wa kijeshi?Sorry if I didn't,lakini "jeshi linininoma" kisawasawa kwa miaka miwili ya A'level kijeshi na mmoja wa JKT kijeshi.Let's leave it there.Huko JKT nilikutana na jamaa flani mahiri sana kwa kufokafoka (rapping).Sijui yuko wapi sasa.Yeye alikuwa rafiki na jamaa mmoja ambaye aliwahi kuibuka mshindi wa mashindano ya Yo!Rap Bonanza miaka ileeee...anaitwa Frank Mtui a.k.a Fresh XE (kama sijakosea,maana ni muda mrefu sasa).Urafiki wao ndio uliopelekea jamaa yangu huyo ambaye jina limenitoka kidogo kuwa mahiri kwenye ku-rap.Tofauti na yeye,mie nikagundua mapema kwamba ulimi wangu mzito,hivyo to become a rapper was out of question.Ndoto yangu ikaegemea kwenye u-producer.Baada ya ngarambe na fatiki za kambini,jamaa yangu huyo alikuwa akinisimulia stori mbalimbali kuhusu maprodyuza maarufu wa muziki wakufokafoka,kama vile Dr Dre,Jermaine Dupri,Pete Rock,et cetera (Dre became my most favourite).Baadaye nikakutana na watu wawili waliozidi kuipa uhai ndoto yangu ya uprodyuza,mmoja anaitwa Profesa Ludigo (alikuwa akitajwatajwa sana kwenye bongoflava kadhaa,ila sijui kwa sasa yuko wapi),mwingine anaitwa Sajo (sio wa Daz Nundaz) ambaye aliwa karibu na Saigon wa Diplomatz,moja ya makundi ya awali ya rap huko nyumbani.Mara ya mwisho nilisikia huyu jamaa (Sajo) yuko Wichita.Prof Ludigo ni "kichwa" kwenye music production na Sajo anaijua fani hiyo nje-ndani.Ndoto ya uprodyuza ikapata nguvu za ziada.How I ended not being a producer I,for some time, dreamt of becoming ,only my God and I know...here I am,not "book-worming" a certain medical journal or searching for some new beat producing softwares,but SIASA...yeah,that's what I'm studying.

Let's go to the point.Nimesoma na kusikia habari kwamba "hali ya afya ya Bongoflava sio ya kuridhisha",na kama ni mgonjwa basi yuko chumba cha wagonjwa mahututi.May be hiyo ni kile ambacho kwenye sarufi ya Kiingereza wanaita "hyperbole" au kuzidisha chumvi.Lakini,kwa a producer that never became one (mimi huyo),nadhani mwelekeo wa muziki huo sio wa kuleta matumaini sana.Frankly speaking,baadhi ya nyimbo za bongofleva zinaweza kukupa hisia kwamba mwanamuziki na prodyuza wake waliurekodi wimbo husika wakiwa usingizini.Ladha (flava) duni,ujumbe (message) ni dhaifu au haueleweki,na wakikurupuka na video ndio inakuwa kana kwamba ililengwa kwa ajili ya "youtube" na sio kuonyeshwa kwenye runinga.Of course,kuna exceptions lakini ni chache.

Nadhani tatizo kubwa liko kwa mwanamuziki kuhakikisha anakuwa bora zaidi ya alipotoa single au album iliyompatia umaarufu.Shughuli imekuwa "kujirusha" sana na kuwekeza "chini" (you surely know what I mean.If you dont,namaanisha "ngono").Wengine wakakimbilia kununua vitu vya thamani ambavyo kwa bahati mbaya hawana uwezo wa kuvimudu.Wengine wakajilinganisha na "wazungu wa unga" ambao hutumia fedha kwa kasi wakijua "shamba" lipo pindi "wakichoka" (wakifilisika).Wengine wakawaiga watu wa Mbughuni na Mererani ambao nao,kama "wazungu wa unga" hutumia kwa fujo wakijua "jiwe" bado lipo mgodini.

Hakuna dhambi kula matunda ya jasho lako lakini ni muhimu kuepuka kung'oa kabisa mmea unaotoa matunda hayo.Lakini vijana wengi waliotokea kupata umaarufu kwenye bongofleva wanakabiliwa na tatizo jingine kubwa zaidi ya hilo la kubweteka au kula jasho lao pasipo kufikiria kesho itakuwaje.Hili ni matumizi ya majani haramu yajulikanayo kama bangi.Kuna idadi kubwa ya wasanii wanaoendekeza bangi kupita vipaji vyao.Najua wapo wanaodai wakivuta "weed" ndio wanawezesha verse kushuka kwa kasi ya tsunami,lakini hizo ni crazy excuses.Bangi sio kitu kizuri.Na mbaya zaidi ni kwa wale wanaotengeneza cocktail ya bangi,unga na laga.

Nini kifanyike?Well,nchi ina matatizo makubwa na ya muhimu zaidi kuliko "hali ya afya ya bongoflava".Na kwa vile suala la kulinda au kutelekeza ajira au kipaji ni la mtu binafsi,inaweza kuwa sio rahisi kuwashauri baadhi ya nyota wetu wanaoelekea kufifia.Wanaopenda majibu mepesi kwenye maswali magumu wanahitimisha kwamba "taarabu ilivuma wee baadaye ikafifia,na sasa ni zamu ya bongoflava...".Mie naona chanzo ni kipana zaidi ya suala la kuvuma na kufifia:kubweteka na mafanikio,kuendekeza anasa na kusahau kazi,maprodyuza wanaoigana wanaopelekea msikilizaji kushindwa kutofautisha wimbo wa msanii mpya na wa zamani-sambamba na productions nyingi "zisizokwenda shule" ni mlolongo wa sababu zinazowakwaza vijana hawa.You have been warned....

Talking of Dr Dre,he cautions in Been There Done That, that "...a fool and his dough soon split..." in the 3rd line of the 2nd verse.Here is the video (caution: explicit lyrics).


Na hapa ni Jay-Z katika Girls,Girls,Girls (dedicated kwa "wanaoendekeza vimwana")


And finally,nadhani utakubaliana nami kwamba some flavaz seem to last forever in your ears,kwa mfano hii I Got 5 on It ya Luniz (japo wenyewe "wamepotea")





Au hii soundtrack ya Friday, You Can Do It ya Ice Cube (Caution: explicit lyrics)


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.