8 Jan 2008


Inatia uchungu,inasikitisha na inakasirisha kuona uhuni anaofanya Mwai Kibaki wa kuamua kutangaza baraza la mawaziri ilhali anafahamu fika kwamba hatua hiyo itakwaza jitihada za kutafuta amani zinazoendelea nchini humo.Nadhani Kibaki anakwepa kwa makusudi jitihada hizo kwa vile anafahamu fika zinaweza kuufichua wizi wake wa kura kwa upana zaidi.Kibaki anapaswa kutambua kuwa miongoni mwa wanaotaabika ni watu wa kabila lake,lakini naamini kwamba uchu wake wa madaraka unamfanya asijali kabisa kinachoendelea.Kama ndugu yangu Hashim wa Russia anavyoona,tatizo kubwa kabisa nchini Kenya ni kupotea kwa upendo kunakochochewa na Kibaki kuendeleza tamaa ya madaraka.

Anyway,hebu tujiliwaze kwa clip hii Where is the Love ya Black Eyed Peas

1 comment:

  1. Hi, Evarist!

    Nimefurahi kukutana na wewe. mh!?...Lol Kukutana kupitia tovuti. Na nimefurahi sana kupata mchango wako katika kurekebisha mambo fulani fulani...na ahsante kwa comment yako...
    Inapendeza kuona kaka yetu unabidii ya kusoma! Ongeza bidii zaidi!

    -TK...

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.