13 Sept 2008

Moja ya mambo hatari sana ambayo kwa kiasi kikubwa ni kama yamefumbiwa macho huko nyumbani ni matangazo yaliyotapakaa kwenye magazeti na mitaani kuhusu tiba ya Ukimwi.Waganga wengi wa jadi,wa kweli na "wasanii",wamekuwa wakijitangaza kuwa wanatibu ugonjwa huo hatari.Ni vigumu kupata takwimu sahihi za watu wanaopoteza maisha kwa kufuata tiba hizo badala ya ARVs,lakini yayumkinika kuamini kuwa utapeli wa aina hii inagharimu maisha ya waathirika wengi.Nimekutana na habari ya usanii kama huo uliokuwa ukiendelea nchini Afrika ya Kusini.Kibaya zaidi ni kwamba mtu aliyesimamia shughuli hiyo,Matthias Rath, alikuwa akijigamba kuwa mkombozi wa Afrika na dunia dhidi ya Ukimwi.Simulizi kamili ya video iko HAPA

0 comments:

Post a comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2020

Powered by Blogger.

Nisapoti

Podcast

Chaneli Ya YouTube