16 Oct 2008


"Hata ingekuwa Ronald Reagan katika nafasi ya John McCain dhidi ya Obama,ni dhahiri ingekuwa hadithi ileile...McCain ameshindwa."Hii ni tafsiri isiyo rasmi ya kauli ya Charles Krauthammer kwa Brit Hume,baada ya mdahalo wa mwisho kati ya McCain na Barack Obama.Bill Kristol nae ametoa more or less same conclusion.

Kwa mujibu wa kura za maoni za watazamaji wa mjadala huo kwa CNN na CBS (na Frank Luntz's focus group ya undecided voters,Obama ameshinda mjadala huo.Pia wachambuzi wa mdahalo huo wameonekana kukubaliana kuhusu mwonekano wa wagombea hao wakati wa mjadala,ambapo mara kadhaa Obama alikuwa akitabasamu na kucheka huku akiwa more relaxed wakati takriban muda wote McCain alikuwa serious na kama mtu anayekimbizana na muda.

Ni vigumu kufanya utabiri kwenye siasa,ni vigumu zaidi kufanya utabiri kwenye uchaguzi,na ni vigumu mno kufanya utabiri wa uhakika takriban siku 19 kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani.Hata hivyo,kama hakuna Bradley effect katika opinion polls zinazoonyesha Obama akiongoza katika karibu kila poll,na kama hakutatokea tukio kubwa (kwa mfano,God forbid,shambulizi la kigaidi kama la September 11,au kukamatwa kwa Osama bin Laden) Obama anasimama katika nafasi nzuri ya kuwa rais wa kwanza mweusi wa Marekani hapo November 4.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.