11 Oct 2008


Siasa ni mchezo mchafu,hilo halina ubishi.Wapo wanaotumia uzushi,udini,ubabaishaji,haiba na hata ndumba  kufikia malengo yao ya kisiasa.Pamoja na uchafu katika mchezo uitwao siasa,kuna wanasiasa wastaarabu wenye kutumia kanuni na taratibu kufikia malengo yao.Hadi hivi karibuni,John McCain alikuwa mmoja wao.Lakini baada ya kuona kura zinamwendea kombo akaamua kuwasikiliza wapambe wake wanaodhani kuwa njia ya mkato ya kumkabili Barack Obama ni ku-assassinate character yake:muite terrorist,tumia jina lake la kati Hussein,fananisha Obama na Osama,na upuuzi mwingine kama huo.

Wakati McCain anatafakari kama mkakati wa aina hiyo ungeweza kuleta mabadiliko,Sarah Palin akaingia kichwa kichwa na kumhusisha Obama na watu kama Ayers na Rev Wright.Wafuasi wakawa motivated,na wengine wakafikia hatua ya kumuita Obama terrorist.Kwa Palin (na bila shaka McCain),ilionekana kuwa picha inaanza kukamilika.Lakini vitendo hivyo vya kishenzi vikawafanya baadhi ya watu wanaomheshimu McCain kuhoji iwapo amefilisika kisiasa kiasi hicho.Na inaelekea ujumbe umefika kwake kama inavyoonekana kwenye clip ya hapo chini.

Hata hivyo,McCain anakabiliwa na mtihani mgumu pengine zaidi ya kushinda uchaguzi hapo Novemba 4.Kwa upande mmoja,ana-risk kupoteza sapoti ya wale wanaopenda kuona Obama akishambuliwa kwa nguvu zote.Miongoni mwa hao ni wasaidizi wa karibu wa McCain ambapo wamekuwa wakitoa matangazo ya kumchafua Obama.Kwahiyo,akiacha kumuandama Obama itamaanisha kujitenga na wanaomsapoti,na dalili ya hilo ni hapo jana ambapo baadhi ya waliohudhuria mkutano wake waliishia kumzomea (angalia clip hapo chini).Kwa upande mwingine,undecided voters na independents wanataka kusikia McCain atawafanyia nini iwapo atakuwa rais,au kwa lugha nyingine kwanini wampe kura zao na si Obama.Matusi na maneno mengine machafu yatalikimbiza kundi hili ambalo analihitaji mmno ili aweze kushinda uchaguzi huo.

Japo McCain anaweza kuwa na hoja za msingi kuhoji kuhusu background ya Obama,swali linabaki why now kama sio dalili za desperation na panic ya kuelekea kushindwa uchaguzi?Kibaya zaidi,kinachowatatiza wapiga kura wa Marekani ni namna rais ajaye atakavyoweza kurekebisha hali mbaya ya uchumi wa taifa hilo.Kuhoji undani wa Obama muda huu (hasa wakati Obama ana-concentrate katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya uchumi) ni sawa na kuyapuuza matatizo yanayowakabili wapiga kura,na it goes without saying how they would pay him back come November 4.
0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.