9 Oct 2008

Hii haijatulia,labda mizimu ilikuwa na beef na anayetambika.Hebu imagine,mnakwenda mtoni au baharini kufanya tambiko halafu mwenzetu anazama wakati wa shughuli hiyo!Haitashangaza baadhi ya watu wakikimbilia kudai kuwa huenda kuna miiko ilikiukwa ndio maana mwenzenu kazama na si ajabu wengine wakihitimisha kuwa "aah wapi,yule alikuwa kigagula ndio maana kasombwa na mkondo wa maji wakati wa tambiko."Kifo ni kifo,na siku zote kinahuzunisha.Lakini kuna wakati waombolezaji wanashindwa kujizuia kucheka kwenye matukio kama ya mtu anayekufa kwa kutumbukia kwenye pipa la chimpumu wakati anapima alcoholic content au  mtu aliekutwa na mauti huko kijijini baada ya kuanguka juu ya ukuta wakati anamchungulia mrembo aliyekuwa anaoga kwenye bafu lenye uwa wa makuti (kozimani,peeping tom au mpiga chabo).Anyway,Bwana hutoa Bwana hutwaa,Jina Lake Lihimidiwe milele.Zaidi BONYEZA HAPA

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube