25 Dec 2008


HIVI TUNA UHABA MKUBWA SANA WA WATENDAJI NA VIONGOZI WAZURI HADI TUENDELEE KUWANG'ANG'ANIA HATA WALE WALIOKWISHAFANYA MADUDU HUKO NYUMA?KUNA STORI KATIKA GAZETI LA MWANANCHI KUHUSU ALIYEKUWA MKURUGENZI WA MANISPAA YA TEMEKE,JOHN LUBUVA,AMBAYE ALISIMAMISHWA KAZI KUTOKANA NA SAKATA LA UBOMOAJI NYUMBA HUKO TABATA DAMPO.CHA AJABU ETI KWA SASA NI MKURUGENZI WA MANISPAA YA SHINYANGA VIJIJINI.HII SIO TU DHARAU KWA WAKAZI WA MANISPAA HIYO ILIYOLETEWA "MTENDAJI MPYA" BALI PIA NI MUENDELEZO WA HAKA KAMTINDO KA KUNG'ANG'ANIA VIONGOZI WALIOPUNGUKIWA NA SIFA.JE,KUMREJESHA KIONGOZI HUYO MADARAKANI HAKUWEZI KUWA KICHOCHEO KWA VIONGOZI WENGINE KUREJEA MADUDU KAMA YA MWENZAO ALIYEBORONGA,AKAPEWA MAPUMZIKO MAFUPI KISHA AKAREJESHWA MADARAKANI?TANGU LINI ADHABU KWA MAKOSA YA UONGOZI IKAWA KUHAMISHWA KUTOKA TEMEKE NA KUPELEKWA SHINYANGA?HIVI AKILIKOROGA TENA HUKO SHINYANGA ITAKUWAJE?THIS IS NOT ONLY UNFAIR BUT INAKERA NA KUCHUKIZA PIA.

1 comment:

  1. Heshima kwako Kaka. Ndivyo ilivyo sasa nyumbani na kwa hakika inasikitisha saaana. Yaani sijui kama kuna "kamkataba" kuwa kiongozi asitoke nje ya wale uliopewa kwenye list? Tunaona madudu ya ajabu sana yanaendelea kwenye uongozi wetu huko nyumbani na mbaya zaidi hakuna mwenye "gut" za kuuliza kulikoni? Hivi hawa watendaji wakubwa wa serikali wateuliwapo hawastahili kuidhinishwa na chombo chochote kama Bunge? Ni waziri mkuu tu ama?
    Kuna haja ya kuwa na namna ya kuondoa huo uozo kabla haujanukisha sehemu nyingine

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.