23 Dec 2008PICHA HIZI ZINAONYESHA UHARIBIFU ULIOSABABISHWA NA VURUGU ZINAZOENDELEA NCHINI UGIRIKI KUFUATIA POLISI KUMUUA MTOTO MMOJA.BAADA YA KUANGALIAPICHA HIZO,HEBU SOMA HABARI IFUATAYO KUHUSU VIFO VYA WATOTO WATATU HUKO KILIMANJARO.
WATOTO watatu wa jamii ya wafugaji wa Kimasai, wameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi waliopo kwenye mazoezi ya kulenga shabaha katika Kijiji cha Embukoi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Embukoi, Peter Pekasi, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni, ambapo watoto hao walikuwa wakipita eneo kwenda kusaga nafaka katika mashine iliyo jirani na kijiji hicho.

Mtendaji huyo aliwataja watoto wanaodaiwa kuuawa kuwa ni Lyomo Orkwari (7), Laata Mollel (15) na Samwel Josia(8), wote wakazi wa kijiji hicho cha jamii ya Masai.

Pekasi alisema eneo la tukio limekuwa likitumiwa kwa muda mrefu kama kituo cha kulenga shabaha kwa askari waliopo mafunzoni katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi (CCP) na kuhatarisha maisha yao.

Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Siha, Anarose Nyamubi.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema hana taarifa kamili za tukio hilo na kuongeza kwamba ametuma maafisa wake eneo la tukio.

“Jamani nimepata taarifa hizo muda mfupi kabla hujaja hapa, nimetuma maofisa wangu eneo la tukio, kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote, nitatoa taarifa zaidi baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa askari wangu,” alisema Ng’hoboko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Nyamubi, akizungumza kwa njia ya simu jana, alithibitisha kupata taarifa hizo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani na kwamba ametuma maofisa wake eneo la tukio.NA HAITOSHANGAZA IWAPO HAKUNA ATAKAYEWAJIBIKA KWA VIFO VYA WATOTO HAO WASIO NA HATIA.


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.