17 Dec 2008

SOMA HABARI HII KISHA ANGALIA UCHAMBUZI WANGU
MLOLONGO wa matukio ya kufikishwa mahakamani kwa waliokuwa viongozi waandamizi katika Serikali ya Awamu ya Tatu pamoja na watuhumiwa wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), unaonekana kuwatisha viongozi wa Kanisa Katoliki na sasa wameanza kupanga mikakati ya kuliepusha taifa na hali ya machafuko.

Askofu Mkuu Msaidizi wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Methodius Kilaini, juzi aliiambia Tanzania Daima Jumatano katika mahojiano maalumu yaliyofanyika ofisini kwake kuwa, matukio yanayotokea sasa hapa nchini yanatisha kwa sababu yanaweza kuhatarisha amani iliyopo.

Alisema matukio ya kukamatwa kwa baadhi ya Watanzania wakiwa na mabilioni ya fedha zinazoweza kununua vijiji au mkoa, kufikishwa mahakamani kwa viongozi wastaafu wa serikali wakihusishwa na ufisadi na matumuzi mabaya ya madaraka wakiwa watumishi katika ofisi za umma, viongozi wa juu serikali kujiuzulu na matukio mengi ya mauaji ya kikatili, ni mambo yasiyokuwa ya kawaida na ya hatari.

Alisema kwa kutambua hali inayolikabili taifa, Kanisa Katoliki limeamua kuweka mikakati ya kulinusuru taifa na machafuko, itakayoongozwa na sala maalumu ya kuomba amani iendelee kutawala nchini.

“Kutokana na mambo haya mazito kutoka hapa nchini, tuna jukumu la kuhakikisha tunaiombea nchi yetu ili amani iliyopo iimarike kwa vile mlolongo wa matukio haya yasiyo ya kawaida yanaweza kuhatarisha amani iliyopo.

Sisi Kanisa Katoliki tumepiga kelele tumechoka, wenye jukumu la kuongea sana ni viongozi wa vyama vya siasa na mashirika ya kijamii. Sasa tumeamua kuanza na silaha kubwa zaidi ambayo ni sala, tumewaambia waumini wetu waanze utaratibu maalumu uliotolewa na Baraza la Maaskofu (TEC) wa kusali sala maalumu ya kuliombea taifa amani, ambao utafuatwa na waumini wote Wakatoliki,” alisema Askofu Kilaini.

Alisema pamoja na kusali, kanisa lina jukumu la kuishauri serikali juu ya mwenendo wa mambo nchini, pamoja na kukemea maovu, uvunjaji wa maadili, tabia za ushirikina zinazokithiri, mauaji ya kikatili ya mtu mmoja mmoja na ya koo na mambo mengine ya kifisadi yanayofanywa na baadhi ya viongozi ambao ni waumini wa makanisa au misikiti.

Hata hivyo, alisema si wajibu wa kanisa kuwakataa waumini wake wanaohusishwa na matukio ya ufisadi nchini kwa sababu kuwafukuza kundini si kuwasaidia, bali ni wajibu wa kanisa kuwaelimisha na kuwajenga watu katika maadili mema.

“Sisi si polisi au mahakama, kwa hiyo hatuna jukumu la kumtaja mtu binafsi hadharani au kanisani, kama muumini anashiriki katika mamabo ya kifisadi, tunalo jukumu la kumrekebisha au kumkemea, lakini si kumtaja hadharani.

“Lakini ifahamike kuwa yanapotokea matukio makubwa nchini kama haya ya ufisadi na serikali ikachukua hatua au kutochukua hatua, ni lazima kanisa lizungumze.

Hata hivyo hatua iliyokwishachukuliwa na serikali ya kuwafikisha watuhumiwa wa EPA na wengine waliotumia madaraka vibaya mahakamani wakati wakiwa madarakani ni nzuri, ila ieleweke kuwa kanisa halisemi kuwa watuhumiwa wamekwisha, haliwezi kusema hivyo.

“Kanisa linathamini na kutambua hatua za awali zilizokwisha kuchukuliwa na serikali za kuwafikisha watuhumiwa mahakamani, hatujui wapo wangapi, tunavuta subira kusikiliza kazi ya vyombo vya uchunguzi inayoendelea ili kuwafikisha wote mahakamani,” alisema Kilaini.

Akizungumzia mauaji ya albino, alisema kanisa linasikitishwa na hali inayoendelea nchini ya mauaji ya albino, vitendo ambavyo ni vya kikatili na ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyoweza kuvunja umoja wa kitaifa.

Alisema mauaji ya albino yanakera, yanaitia aibu nchi na kuikosesha heshima machoni pa jumuiya ya kimataifa. Kwamba dunia inawashangaa Watanzania wanaishi karne ipi.

Alisisitiza kuwa matukio ya mauaji ya albino yameichafua nchi kiasi cha wageni kuiona Tanzania kama mahali pasipofaa kuishi.

“Wageni nao wanaanza kuogopa kuja kwani albino wakiisha nchini watafuata kundi jingine la watu, na kwa mtiririko huo, baadaye Watanzania wote wataanza kuuana. Serikali inatakiwa ilitangaze suala hili kuwa janga la kitaifa.

“Kama taifa tunapaswa kuchukua hatua madhubuti kupambana na kukomesha mauaji haya kwa vile tunakoelekea ni kubaya, wakimaliza albino, watawataka wenye kipara, baadaye watu weusi au wa kabila fulani, tukifika hapo ni vita ya wenyewe kwa wenyewe.

“Kanisa linaitaka serikali kutumia mbinu zozote, kutoa elimu kwa raia wake ikiwezekana kuanzia kwenye shule za msingi na sekondari juu ya madhara ya mauaji hayo. Kanisa linaiomba serikali iunde idara maalumu ya usalama wa taifa, makachero watumwe vijijini kuangalia kazi inayofanywa na waganga wa kienyeji, wachunguze kazi zao, wanavyopiga ramli na kupata ufumbuzi wa chimbuko na misingi ya mauaji hayo,” alisema Askofu Kilaini.

Akizungumza sababu ya kanisa kuchukua hatua ya kuanzisha mkakati wa kuomba ili kunusuru taifa na hali yoyote ya uvunjifu wa amani, alisema, imetokana na hofu ambayo kanisa limeipata baada ya kuwapo kwa ongezeka kubwa la matukio ya ajabu ambayo kwa kipindi cha miaka mingi hata kabla ya uhuru hayakuwahi kutokea.


KAMA MKATOLIKI,NAKUBALIANA NA KAULI YA KIONGOZI WANGU WA DINI MHASHAMU KILAINI.LAKINI KAMA MCHAMBUZI (MCHANGA) WA STADI ZA SIASA,NAOMBA KUTOAFIKIANA NAE KATIKA MAENEO YAFUATAYO.

KWANZA,KANISA KATOLIKI LINAPASWA KUKUBALI KWAMBA HALIJAFANYA VYA KUTOSHA KUPAMBANA NA MAOVU NDANI YA JAMII.NA KATIKA HILO,SIO KANISA PEKEE LINALOWEZA KUTUPIWA LAWAMA BALI TAKRIBAN MADHEHEBU YOTE HUKO NYUMBANI.TUNAWEZA KWENDA MBALI ZAIDI KWA KUANGALIA BAADHI YA MAMBO YANAYOWEZA KUWA SABABU KUU YA "UOGA" WA BAADHI YA VIONGOZI WA DINI KUKEMEA MAUMI MENGINE KATIKA JAMII.WENGI WETU TUNAFAHAMU "UCHAFU" WA BAADHI YA VIONGOZI HAO,NA JAPO KANISA LIMEKUWA LIKISISITIZA KUFUATA MAFUNDISHO YA VIONGOZI NA SIO MATENDO YAO,UKWELI UNABAKI KWAMBA NI VIGUMU KUTENGANISHA MANENO NA VITENDO VYA MSEMAJI.HIVI INALETA MAANA KWELI.KWA MFANO,MTUMISHI WA MUNGU ANAYEBANJUA AMRI YA SITA (MZINZI) KISHA AKAHUBIRI KUHUSU DHAMBI YA UZINZI?NI DHAHIRI MJUMBE WA YESU ANAPASWA KUISHI KAMA YESU MWENYEWE.YAYUMKINIKA KUSEMA KWAMBA LAITI MITUME WETU WASINGEKUWA WASAFI KATIKA MATENDO YAO,LEO HII TUSINGEKUWA WAUMINI WA DINI ZETU.

TUKIREJEA KWENYE HABARI HIYO HAPO JUU,SIJAMWELEWA VIZURI MHASHAMU KILAINI ANAPOSEMA "matukio yanayotokea sasa hapa nchini yanatisha kwa sababu yanaweza kuhatarisha amani iliyopo".JE ANAMAANISHA KWAMBA AMANI ITAHATARISHWA KUTOKANA NA TUKIO KAMA KUWAFIKISHA WATUHUMIWA WA UFISADI MAHAKAMANI?KWANINI SUALA HILO LISIWE KIGEZO CHA KUREJESHA IMANI YA WANANCHI ILIYOPOTEA KUTOKANA NA HISIA KWAMBA MAFISADI WANALINDWA?AMANI HAIWEZI KUHATARISHWA KWA KUWACHUKULIA HATUA MAFISADI,REGARDLESS YA NAFASI ZAO KATIKA JAMII.KWA NAMNA FLANI KAULI HIYO YA MHASAHAMU KILAINI INASHABIHIANA NA ILE ILIYOWAHI KUTOLEWA NA MKURUGENZI WA TAKUKURU,BW EDWARD HOSEA,KWAMBA WATUHUMIWA WOTE WA EPA WAKISHTAKI NCHI ITAYUMBA.

SITAKI KUINGIA KWA UNDANI KUHUSU DHANA KUWEPO KWA AMANI HUKO NYUMBANI,KWA SABABU DHANA HIYO NI TETE.JE AMANI NI KUTOKUWEPO KWA VITA PEKEE?JE KUNA AMANI KWA VILE WENYE VIPARA,VITAMBO,MAWOWOWO,ETC HAWAWINDWI KAMA MAALBINO?JE KUNA AMANI WAKATI IDADI YA WASIO NA UHAKIKA WA MLO WA KESHO NI KUBWA ZAIDI YA WALE WENYE UHAKIKA HUO?SIKU CHACHE ZIJAZO NITAINGIA KWA UNDANI KUANZISHA MJADALA KUHUSU DHANA YA AMANI NCHINI TANZANIA.LAKINI TUNALOWEZA KUHOJIM KWA SASA NI IWAPO MATUKIO YANAYOZUNGUMZWA NA MHASHAMU KILAINI YANAWEZA KUHATARISHA AMANI (KAMA TUNAKUBALIANA KUWA AMANI HIYO IPO,IN THE FIRST PLACE).

MHASHAMU KILAINI ANASEMA "Kanisa Katoliki limeamua kuweka mikakati ya kulinusuru taifa na machafuko, itakayoongozwa na sala maalumu ya kuomba amani iendelee kutawala nchini".NATAKA KUAMINI KWAMBA MKAKATI HUU WA KANISA UMEKUWEPO KWA MUDA MREFU ILA SASA UNAIMARISHWA.KINYUME CHA HIVYO ITAMAANISHA KWAMBA KANISA LIKO OUT OF TOUCH NA HALIJALI MADHILA YANAYOWAKUMBA WENGI WA WAUMINI WAKE.SI KWELI KWAMBA MATATIZO YANAYOIKABILI TANZANIA YAMEANZA MAJUZI KIASI CHA KANISA KUSHTUKA NA KUJA NA MKAKATI HUO,BALI MATATIZO HAYO YAMEKUWEPO KWA MUDA MREFU SASA.HATA MAUAJI DHIDI YA ALBINO HAYAJAANZA MWAKA HUU KIASI CHA KANISA KUSHTUKA WAKATI HUU TUNAPOELEKEA MWISHONI MWA MWAKA.

LAKINI TWENDE MBELE ZAIDI NA KUJADILI IWAPO MKAKATI HUO WA SALA UNAWEZA KUWA NA MAFANIKIO.TUNAFAHAMU KWAMBA BAADHI YA WATUHUMIWA WA UFISADI NI WAKRISTO WANAOHUDHURIA KANISANI KILA JUMAPILI.TUAMINI PIA KWAMBA MAHUBIRI MENGI HUKO KANISANI YANASISITIZA UPENDO NA KUPINGA VITENDO VYA KIFISADI.SASA KWA VILE VITENDO HIVYO SIO TU VIMEENDELEA BALI VIMESHIKA HATAMU TO ANA EXTENT YA KULIFANYA KANISA KUJA NA MKAKATI MPYA,NI DHAHIRI KWAMBA SALA PEKEE HAZIWEZI KULETA MABADILIKO YA MAANA.HAWA MAFISADI TUNAOJUMUIKA NAO MAKANISANI WANAPASWA KUWEKWA "KITIMOTO" HATA KAMA KUFANYA HIVYO NI KINYUME NA TARATIBU ZA KANISA.VIONGOZI WETU WA DINI WANAPASWA KUWAITA WAUMINI WAO WANAOTUHUMIWA NA UFISADI NA KUWAAMBIA (KATIKA LUGHA YA KIROHO) KWAMBA MATENDO YAO YANAMKERA MUNGU (NA MUNGU TUNAYEMZUNGUMZIA HAPA NI YULE TULIYEAMBIWA WAKATI WA KAMPENI KWAMBA "ANA CHAGUO LAKE KATIKA UCHAGUZI MKUU WA 2005").

NADHANI WENGI WETU BADO TUNA KUMBUKUMBU NAMNA ASKOFU LAIZER WA KKKT ALIVYOTUMIA MIMBARI YAKE KUMSAFISHA LOWASSA (REJEA MAKALA HII KATIKA JARIDA LA RAIA MWEMA).VIONGOZI WENGI WA DINI WAMEKUWA MASHABIKI WA WANASIASA,PENGINE KWA MASLAHI YAO BINAFSI BADALA YA YALE YA WAUMINI WAO AMBAO NDIO WANAOONJA JOTO YA JIWE KILA KUKICHA KUTOKANA NA MADUDU YA BAADHI YA WANASIASA HAO.NAKUMBUKA LECTURE MMOJA PALE MLIMANI (UDSM) WAKATI NASAKA SHAHADA YANGU YA KWANZA AMBAPO MHADHIRI MMOJA,DR MAX MMUYA,ALIELEZA KWAMBA FORCES KUU ZA KUWEZA KUBADILI TABIA,MAAMUZI NA MATENDO YA WANASIASA NA TAASISI ZA DINI NA WAHISANI.VIONGOZI WA DINI WAKTITISHI KUMTENGA KIONGOZI FISADI LAZIMA ATABADILIKA KWANI ANAJUA KESHO KUNA KIFO.WAHISANI WAKITISHIA KUNYIMA MSAADA BASI HATA WATUHUMIWA WA ANBEM WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.KWA KIFUPI,MADHEHEBU YA DINI NCHINI YAMETUANGAUSHA WAUMINI WAKE KATIKA VITA DHIDI YA UFISADI.

TUREJEE KWENYE HABARI HUSIKA.MHASHAMU KILAINI ANASEMA "Sisi Kanisa Katoliki tumepiga kelele tumechokawenye jukumu la kuongea sana ni viongozi wa vyama vya siasa na mashirika ya kijamii. Sasa tumeamua kuanza na silaha kubwa zaidi ambayo ni sala...".HIVI KAMA KANISA LIMECHOKAM KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI LITAWEZA KWELI KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA SHETANI YANAYOLENGWA KUWASAIDIA WAUMINI WAKE WAUFIKIE UZIMA WA MILELE?THIS IS SHEER IRRESPONSIBILITY!KANISA HALIPASWI KUCHOKA,SIO TU KWENYE KUPIGA KELELE DHIDI YA UFISADI BALI PIA KWENYE KILA JAMBO LITAKALOWASAIDIA WAUMINI WAKE KUUONA UFALME WA MBINGU.KUDAI KUWA JUKUMU LA KUPIGA MAKELELE LIMEACHWA KUONGELEWA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA MASHIRIKA YA KIJAMII NI TUSI KWA WAUMINI WA KANISA HILO.KWANI HAKUNA WAKATOLIKI MIONGONI MWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA NA VYAMA VYA KIJAMII?KAMA WAPO,WAPI WATAPATA MWONGOZO WA KIROHO WA KUWAPA UJASIRI WA KUKEMEA MAFISADI KAMA SIO KANISANI?TANGU LINI KANISA LIKACHOKA?HIVI YESU ANGECHOKA KATIKA MISSION YAKE YA KUMKOMBOA MWANADAMU TUNGEKUWA NA AKINA MHASHAMU KILAINI?SALA PEKEE PASIPO KUPIGA KELELE HAZIWEZI KULETA MABADILIKO KWANI HIYO HAINA TOFAUTI NA KWA MWANAFUNZI KUSALI SANA LAKINI BILA KUJISOMEA KISHA AKATEGEMEA KUFAULU MTIHANI.SALA ZIENDANE NA MAKELELE ZAIDI YA KUKEMEA UFISADI.

MHASHAMU KILAINI AMEJITAHIDI KUNYAMBULISHA MAJUKUMU YA KANISA KWA WAKATI HUU (ACTUALLY,KWA MUDA WOTE) NA HAPO NDIPO ANAPOZUA CONTRADICTION KUBWA ZAIDI KWANI MAJUKUMU HAYO HAYATATEKELEZEKA IWAPO KANISA LITAKUWA LIMECHOKA.BY THE WAY,UCHOVU UNAOZUNGUMZIWA HAPA NI ULE UNAOSHABIHIANA NA KUKATA TAMAA AU UVIVU,NA VYOTE HIVYO NI MIZIZI YA DHAMBI.TUTAMUANIJE MHASHAMU KILAINI KWAMBA BAADA YA KUCHOKA KUPIGA MAKELELE KANISA HALITACHOKA PIA KUISHAURI SERIKALI?

MWISHO,NAUNGANA NA MHASHAMU KILAINI JUU YA UMUHIMU WA KUTANGAZA MAUAJI YA ALBINO KUWA NI JANGA LA KITAIFA.NAAFIKIANA NAE PIA KWAMBA SERIKALI INAPASWA KUZI-MOBILIZE TAASISI ZA USALAMA ZIONGEZE NGUVU ZAO KUKABILIANA NA JANGA HILO.KAMA INAFANYWA HIVYO KATIKA KUKABILIANA NA UJAMBAZI AU KUDHIBITI WAKIMBIZI,KWANINI ISIANZISHWE OPERESHENI MAALUMU DHIDI YA MAUAJI YA ALBINO?


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.