22 Dec 2008

Photo courtesy of MJENGWA

KURA YANGU INAWAANGUKIA WABABAISHAJI WA TRL.CHEKI "MBELEKO" NYINGINE HII KUTOKA KWA SUMATRA:

HATIMAYE Kampuni ya MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imeiruhusu Kampuni ya Reli (TRL) kuanza kutumia mabehewa yake 23 ya mitumba yaliyokodishwa kutoka Kampuni ya Reli ya India. Awali Sumatra waliizuia TRL kutumia mahehewa hayo kwa madai kwamba hayakuwa na obora unaotakiwa.

Hata hivyo, meneja uhusiano wa TRL, Midrahji Meiz alisema jana kuwa Sumatra sasa imewaruhusu kuendelea kutumia mabehewa hayo baada ya vigezo vilivyokuwa vinahitajika kukamilika.

“Tumesharuhusiwa na Sumatra kuanza kutumia mahehewa hayo na hivi sasa utaratibu unafanyika ili yanze kusafirisha abiria... baada ya utaratibu huo kukamilika tutatoa taarifa rasmi,” alisema Meiz na kuongeza: “Suala la usafiri wa treni ni suala la msingi kabisa na ndiyo maana tunajitahidi kuboresha usafiri huo kila wakati ili abiria wasafiri katika mazingira mazuri.”

Mkurugenzi na mdhibiti wa reli wa Sumatra, Alfred Nalitolela alikiri kuwepo kwa suala hilo na kusema kuwa wameamua kuiruhusu TRL indelee kutumia mabehewa hayo kwa kuwa wamekamilisha marekebisho yaliyokuwa yanahitajika.

“Tulibaini kwamba mabehewa hayo hayana ubora unaostahili kwa matumizi ya reli yetu, na moja ya vitu hivyo ni kiungio kati ya behewa moja na jingine, usambazi wa umeme ndani ya mabehewa, belling, spring, breki ya mkononi na magurudumu,” alisema Nalitolela na kuongeza:

“Tulipokwenda India kukagua mabehewa hayo, tuliwaeleza wafanye vitu hivyo lakini wakaleta mabehewa kabla ya kukamilika kwake ndipo ikabidi tuwakataze kuyatumia mpaka wamalize kuyafanyia marekebisho hayo.”

Alifafanua kwamba baada ya hapo walichukuwa moja ya kiungio cha mabehewa na kuyapeleka katika maabara ya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuyafanyia utafiti kama ni vifaa vipya na kuomba maelezo ya kina.

“Unafahamu katika suala hili lile jumba la behewa ndilo linalotakiwa kuwa mtumba, lakini vifaa vyote vinavyofanya mabehewa hayo yafanye kazi vinatakiwa kuwa vipya, ikiwemo usambaji wa nyaya za umeme ndani ya behewa. Na hicho ndicho tunachokikagua na kukiangalia na kuhakikisha kwamba viko salama kila wakati,” alifafanua Nalitolela.
CHANZO:Mwananchi
JE MWENZANGU KURA YAKO INAANGUKIA WAPI?

1 comment:

  1. kwanza nilidhani TRL ni bendi ya muziki kama vile FM Akademia, stono musica, twangwa pepeta n.k lakini nikiwa mawazoni nikadhani labda ni ZE Comedy za bill Cosby, masanja mkandamizaji, joti halafu nikamkumbuka mzee pembe, kisha nikamleta Kingwendu kingwendulile pia nikadhani labd akile kipindi cha jiweke sawa na hesawa pale RTD enzi hizo pengine ni hayao lakini TRL ni zaidi pengine ni kioski tu cha kuuza magimbi pale wavuvi wa nyasa wanapotoka kuvua na njaa zao, labda ni store ya mikeka na pengine ni kijiwe tu cha kupigia mizinga wengine NAACHA mkuu wengine wachangie pia

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.