5 Jan 2009

ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi Nchini, Meja Jenerali, Robert Mboma, amesema anaamini kitambi alicho nacho kimesababisha kushindwa katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) za ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.

Mboma aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.Alisisitiza kuwa anaamini kilichochangia kutopata kura nyingi zaidi ni kitambi hicho alichokuwa nacho na kwamba hali hiyo itamkomaza kisiasa.

Mboma ambaye aliwashangaza baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kijiji cha Ilembo Mbeya vijijini.Alisema kkuanguka kwake katika jimbo hilo kumetokana na wananchama wa chama hicho kumnyima kura.

Alisema kitendo hicho hakiotamuathiri bali wanamkomaza kisiasa na kwamba endapo kama angeteuliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo angelepeleka maendeleo."Kwa kweli nanawashukuru wananchi mlionipigia kura nilizozipata ingawa hazikuwa ndogo lakini ninasikitika na ninawashukuru ambao hawakunipigia kura na kuniangusha wakati wakijua wazi kuwa mimi ni mzaliwa na hapa na mngenichagua ningewaletea wananchi maendeleo katika jimbo la Mbeya vijijini," alisema.

Aliendelea kusema kuwa sio mbaya hata kama wamemchagua Mchungaji Mwanjali kwa sababu anaimani atawaletea Maendeleo na kurithi yale yote aliyatarajia kuyafanya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Richard Nyaulawa katika kuboresha huduma za jamii hususan maji, umeme na kuboreshea miundombinu...HABARI HII INAENDELEA HAPA.

NILIDHANI WANAJESHI WANASTAHILI KUJIWEKA FIT HATA BAADA YA KUSTAAFU MAJUKUMU YAO.HOW COME MKUU WA MAJESHI AMEJIACHIA KIASI CHA KUWA NA KITAMBI KIKUBWA "KILICHOPELEKEA KUANGUSHWA KWAKE KWENYE KINYANG'ANYIRO HICHO"? BY THE WAY I DONT BUY HIS LAME EXCUSE.NADHANI HAKUFANYA RESEARCH YA KUTOSHA KABLA YA KUJIINGIZA KWENYE COMPETITIVE POLITICS.WATANZANIA WAMEANZA KUTOFAUTISHA KATI YA UMAARUFU WA MTU NA UWEZO WA KUWALETEA MAENDELEO.AND IT'S THE LATTER THAT LED TO MBOMA'S FAILURE TO WIN HIS PARTY'S NOMINATION.

HII DHANA YA KWAMBA ANGEPATA UBUNGE ANGEWEZA KUWALETEA MAENDELEO WANA MBEYA VIJIJINI SIO TU POTOFU BALI PIA MUFILISI.KWANI ILI KULETA MAENDELEO YA WANANCHI WENZIO NI LAZIMA UWE KIONGOZI WAO?ALISHINDWAJE KUWALETEA MAENDELEO ALIPOKUWA KIONGOZI WA KITAIFA (MKUU WA MAJESHI) LAKINI AWEZE ATAPOPATA UBUNGE?NI UKOSEFU WA WASHAURI WAZURI AMBAO WANGEPASWA KUMKUMBUSHA HISTORIA YA MA EX-CDF WENZIE.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.