5 Jan 2009

Magazeti mbalimbali ya leo huko nyumbani yameongozwa na habari za uzinduzi wa kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ndiye aliyezindua kampeni hizo na kufanya kila ambacho kwa muda mrefu kimekuwa adimu katika duru za siasa za vyama vingi huko nyumbani.Kwa mujibu wa habari hizo,Mwinyi,maarufu kama Mzee Ruksa,alitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kuzungumzia maslahi ya wana-Mbeya Vijijini katika uchaguzi huo badala ya kuipigia debe CCM pekee.

"Mwinyi...hakuonyesha unazi kwa CCM wala mgombea wake wakati alipozindua kampeni za chama hicho jana katika kata ya Kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini.Badala yake, Mwinyi alisisitiza amani, mshikamano na maendeleo ya wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanabakia na mshikamano wakati wanasiasa watakapoondoka jimboni humo baada ya purukushani za uchaguzi...linaandika gazeti la Mwananchi.

Tanzania Daima linamnukuu Mwinyi akisema kwamba "Vyama vya siasa vishindane kwa sera, visitumie lugha za matusi, kejeli, dharau na uongo wakati wa kampeni, uungwana wenu viongozi wa siasa utawapa matumaini wananchi kuchagua chama au mtu wanayemtaka ili kuhakikisha kuwa maendeleo ya nchi yanakua kwa kasi".

Akionyesha kuthamini zaidi maslahi ya wananchi wa Mbeya vijijini kuliko ya kisiasa,Rais huyo mstaafu aliwausia wapiga kura jimboni humo "kumsikiliza kila mgombea kwa makini na baadaye kila mmoja amchague yule anayeona sera za chama chake zinakidhi matumaini ya wananchi wa Mbeya Vijijini, " na kuhakikisha "kwamba wakati wanasiasa wetu wanapoondoka Mbeya Vijijini baada ya kampeni nyinyi mnabaki kuwa kitu kimoja katika umoja wenu," linaeleza Habari Leo.

MIONGONI MWA MAMBO YANAYOKWAZA MAENDELEO NI KUWEKA MBELE MASLAHI YA KISIASA BADALA YA YALE YA WANANCHI.OF COURSE,VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WANAPASWA KUSIMAMIA MASLAHI YA VYAMA VYAO LAKINI NI MUHIMU KWAO KUTAMBUA KUWA JUKUMU KUU LA VYAMA HIVYO NI KUWAHUDUMIA WANANCHI NA NI WANANCHI HAOHAO WANAOWEZESHA KUWEPO HAI KWA CHAMA IN THE FORM OF WANACHAMA.KWA MANTIKI HIYO,WANANCHI,REGARDLESS YA POLITICAL AFFILIATIONS ZAO,WANA NAFASI NA UMUHIMU WA KIPEKEE KWA VYAMA VYA SIASA HASA IKIZINGATIWA PIA KWAMBA WAO NDIO PIA CHIMBUKO LA UONGOZI KATIKA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.

BAADA YA KUNG'ATUKA KATIKA ACTIVE POLITICS,BABA WA TAIFA ALIJITAHIDI KUCHUKUA NAFASI YA UANASIASA WA KITAIFA BADALA YA KICHAMA AMBAPO MARA KADHAA ALIWEKA MKAZO KATIKA MASUALA YANAYOHUSU TAIFA KWA UPANA BADALA YA YALE YA CHAMA CHAKE CHA CCM PEKEE,LICHA YA KUWA YEYE NDIO ALIKUWA MIONGONI MWA WAASISI WAKUU WA CHAMA HICHO TAWALA.KWA UPANDE MWINGINE,MWINYI NAFASI YA MWINYI BAADA YA KUSTAAFU UENYEKITI WA CCM IMEPEWA ATTENTION NDOGO NA WACHAMBUZI WA SIASA PAMOJA NA MEDIA KWA KUTOFANYA REFERENCE YA NAMNA KIONGOZI HUYO WA ZAMANI ANAVYOJITAHIDI KUFUATA FOOTSTEPS ZA BABA WA TAIFA KATIKA KUTANGULIZA ZAIDI MASLAHI YA WANANCHI NA TAIFA KWA UJUMLA BADALA YA KUENDEKEZA UNAZI WA KISIASA PEKEE.

NI MATUMAINI YA WATANZANIA WOTE WAPENDA MAENDELEO KWAMBA MFANO HUU WA MZEE MWINYI UTAIGWA NA WANASIASA WETU WOTE KAMA KWELI NIA YAO NI KUTUHUDUMIA KUPITIA VYAMA VYAO.LAKINI PIA WANANCHI NAO WANAPASWA KUFUMBUKA MACHO NA KUTAMBUA KWAMBA UNAZI WA KISIASA HAUPASWI KUWA INFRONT OF MASLAHI YAO KAMA WANANCHI,NA KWA MANTIKI HIYO TOFAUTI ZETU ZA KIITIKADI HAZIPASWI KULETA MGAWANYIKO AU KUPELEKEA KUCHAGUA VIONGOZI WABOVU KWA VILE TU WANATOKA KATIKA VYAMA TUNAVYOSHABIKIA.

HONGERA SANA MZEE RUKSA.YOU TRULY HAVE SHOWN THE RIGHT WAY.1 comment:

  1. Ahsante kaka Evarist kwa uchambuzi wako mzuri.
    Wengi walitarajia mzee Ruksa angemnadi yule mgombea wa CCM kwa staili ya Makamba, lakini kwa bahati nzuri mzee wa watu anweza kusoma alama za nyakati. Well done Mzee Ruksa.

    Kaka Evarist, hsante sana kwa kunitembelea na kutoa maoni yako, ki ukweli maoni yako yannifanya nifikirie kuandika zaidi na zaidi.

    Ahsante sana kwa kunitembelea

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.