3 Jan 2009

Maelfu ya waandamanaji wanatarajiwa kuandamana baadae leo jijini London kupinga mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina.Inakadiriwa takriban watu 20,000 watashiriki maandamano hayo yatakayowajumuisha watu maarufu kama Mbunge wa chama cha Respect,George Galloway na mwanamuziki mkongwe Annie Lennox.Picha ya mwanzo inaonyesha akinamama wa Kiislam walioandamana jana jijini Dar kupinga mashambulizi hayo,na picha za chini zinaonyesha hali ilivyo na uharibifu uliosababishwa na makombora ya Israel huko Gaza.
VYANZO:Sky News,Habari Leo ,The Washington Post na The Guardian.

3 comments:

 1. Hali ya huko ni mbaya. Na la kusikitisha ni kuwa "biashara" ya nchi kubwa na "vita baridi" baina yao inaendeleza hali hii. Wana uwezo wa kuzuia maafa haya kwa wahanga wasio na hatia. Wana uwezo wa kuweka mambo sawa, lakini biashara ya silaha na vyakula itakwama. Utu si kitu kwa baadhi ya watu na zaidi ni pesa na utawala. Kujijengea uchumi na nafasi ya kuwa mtawala ndilo linalopewa kipaumbele hata kama ni kwa kumwaga damu. "Hatuwezi kutatua tatizo kwa kutumia njia zilezile zilizotuletea tatizo hilo" Ndicho walichosahau waheshimiwa. Sijui chanzo, na sijui mwisho ni lini, lakini twauhitaji mwisho huo sasa.
  Blessings

  ReplyDelete
 2. Mimi taaluma yangu uadishi wa habari ninashindwa kujua juu ya mashabulizi haya!!! Je nyinyi wanasiasa kitaaluma tufanye nini ili kuthibiti na kuimalisha amani duniani?

  ReplyDelete
 3. Yanapotokea maandamano kama haya, kwamba kinachofanywa na waisrael dhidi ya maadui wao, kuna waungwana waumini wanakwambia biblia ilishatabiri: "...nanyi mtakuwa watu wa kukataliwa na mataifa yote kwa ajili ya Jina langu...".

  Sasa mtu unajiuliza, kukataliwa kwa ajili ya 'Jina langu' ndio huku kuwaua raia wengine (hata kama wana hatia)? Kwa nini Mwizrael akiua inaonekana si kosa kama anapouawa mpalestina?

  Haya ndio mambo ya Taifa la Mungu. Kila wanachofanya kinaungwa na wakristo duniani kote hata kama Waisrael wenyewe hawajawahi kuukubali Ukristo.

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.