Maelfu ya waandamanaji wanatarajiwa kuandamana baadae leo jijini London kupinga mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina.Inakadiriwa takriban watu 20,000 watashiriki maandamano hayo yatakayowajumuisha watu maarufu kama Mbunge wa chama cha Respect,George Galloway na mwanamuziki mkongwe Annie Lennox.Picha ya mwanzo inaonyesha akinamama wa Kiislam walioandamana jana jijini Dar kupinga mashambulizi hayo,na picha za chini zinaonyesha hali ilivyo na uharibifu uliosababishwa na makombora ya Israel huko Gaza.




VYANZO:Sky News,Habari Leo ,The Washington Post na The Guardian.