12 Jan 2009

KWANZA,SAMAHANI KWA KUPOTEA ANGANI GHAFLA.HIYO NI KUTOKANA NA SABABU ZILIZOKUWA NJE YA UWEZO WANGU.PILI,NIMEKUTANA NA HABARI IFUATAYO KATIKA GAZETI LA MWANANCHI,NA IMEVUTA HISIA ZANGU.ISOME KWANZA KISHA TUIJADILI KIDOGO


WAUMINI wa dini ya kiislam wamepinga oparesheni sangara
inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai kuws
chama hicho na operesheni hiyo, haina manufaa kwa uisalam kwa kuwa imejaa
ukabila, ubinafisi na udini
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye
kongamano la kiisilamu, lililofanyika jana jijini Dar es Salaam, walisema
oparasheni Sangara imekuwa ikimchafua rais Jakaya Kikwete bila sababu licha ya
mambo mengi mazuri, aliyoyafanya kwa taifa.
Shekhe Saidi Mwaipopo aliwataka
waisalamu kutambua kuwa chama hicho, hakina msaada wowote wa maendeleo ya
uislamu kutokana na chama hicho kujaa ukabila udini na ubinafisi.
"Napenda
waislamu muelewe kuwa chama cha Chadema hakina msaada wowote juu ya uislamu na
kimekumbatia udini, ukabila na ubinafisi kutokana na sababu hiyo, tutatembea
nchi nzima kuwaeleza wanachi ukweli wa jambo hili na kuwataka wasikiunge mkono
chama hicho,"alisema Mwaipopo...
ENDELEA


HISIA ZANGU ZA HARAKA NI KWAMBA KUNA KUNDI LA MAFISADI AMBAO KATIKA KUTAPATAPA KWAO WAMEAMUA KUTUMIA TURUFU YA UDINI.KUNA VUGUVUGU LA UDINI LINALOENDELEA KIMYAKIMYA HUKO NYUMBANI.KUNA WATU WANATUMIWA KUTETEA MASLAHI YA MAFISADI,AIDHA WAKATI WANAFAHAMU KUWA WANATUMIWA AU HAWAFAHAMU KABISA.
HIVI INAINGIA AKILINI KWELI KWA WAUMINI WA DINI INAYOSIMAMIA HAKI (UISLAM) KUPINGA HARAKATI ZA KUSIMAMIA HAKI?JE IWAPO OPERESHENI SANGARA ITAZAAA MATUNDA KWA KUFANIKISHA UDHIBITI DHIDI YA MAFISADI,WAISLAMU NCHINI HAWATONUFAIKA?HAPA KUNA MIKONO YA WATU WANAOMWAGA FEDHA ZXAO ZA KIFISADI KWA WALE WALIO TAYARI KUSEMA LOLOTE ALIMRADI MKONO UENDE KINYWANI.
TUSIPOKUWA MAKINI,UFISADI UTAIFIKISHA TANZANIA MAHALA PABAYA ZAIDI YA HAPA TULIPO.

1 comment:

  1. UISLAMU UMEJAA NA KUENEA CCM NA CUF. Angalia tu takwimu vizuri. Leo hii walioteuliwa kupitia mgongo wa raisi, wote waislamu.

    Tukija kwenye matokeo ya uchaguzi 2010, maeneo yote yaliyo na idadi kubwa ya waislamu CUF na CCM walishinda kwa kishindo wakati kura hazikutosha kabisa kwa Chadema. Je hii siyo harufu ya udini kama siyo udini wenyewe!

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube