5 Apr 2009


JAMII imetakiwa kushirikishwa katika maamuzi yaliyotolewa na Baraza la Madiwani pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kubadili jina la Wilaya ya Missenyi na kuiita Wilaya ya Nkenge ambayo tayari yamekubaliwa na baraza hilo pamoja na chama ili kuona kama kubadilika kuna manufaa kwa jamii.

Ombi hilo limetolewa jana na wajumbe wa kikao cha Kamati cha Ushauri wa Wilaya ya Missenyi (DCC) kilichofanyika katika Kata ya Kassambya ambapo baadhi ya wananchi na viongozi walisema kubadilisha jina la wilaya hiyo hakuna maana yoyote.

Mmoja wa watendaji wa kata za wilaya ya missenyi Joseph Kitakule ambaye ni mtendaji wa Kassambya, alisema wadau wa maendeleo inabidi wapinge vikali suala la kubadilisha jina kwa kuwa litaiingiza halmashauri hiyo kwenye hasara kubwa na watakuwa wamekiuka maamuzi ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa aliyebariki jina hilo.

Alisema kumekuwepo kundi la watu wachache wenye maslahi yao binafsi ambao jina hilo likibadilishwa na wizara husika basi wao watakuwa wamepata faida kubwa na watakuwa wamefanikisha adhma yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Izidor Mtalo, alisema suala hilo wao kama watendaji walilikabidhi Baraza la Madiwani kwa vile ndiyo wenye uwamuzi wa kubadilisha au kutobadilisha.

Alisema hakuna kikao chochote ambacho kinaweza kutengua uamuzi huo kwani likishapitishwa na madiwani linapelekwa katika kikao cha ushauri cha mkoa na baadaye kwa waziri mwenye dhamana.

Akitoa uamuzi wa kubadilisha jina hilo na kuitwa Nkenge, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, William Katunzi, alisema kutokana na mkanganyiko wa majina ya tarafa za Kiziba na Missenyi ambazo zinaunda Jimbo la Nkenge kitendo ambacho kimeibua malalamiko kutoka kwa wakazi wa Kiziba.

“Hawa wakazi wa Kiziba wanahoji kama makao makuu ya wilaya yapo katika tarafa ya Misenyi inakuwaje na jina la wilaya ipewe jina la tarafa na wakati jina la jimbo ni tofauti na wilaya kwa hiyo ndiyo sababu kubwa wanayolalamikia na kutaka jina la wilaya liwe sawa na la jimbo Nkenge,” alisema Katunzi


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.