30 Jun 2009

Kifo cha mtu maarufu huambatana na kila aina ya tetesi.Na kifo cha Michael Jackson is no exception.Ukisikiliza,kuona au kusoma kuhusu kifo cha mfalme huyo wa Pop,unaweza kumhukumu kirahisi tu kuwa alikuwa mithili ya mfu aliye hai (dead man walking).Baadhi ya vyombo vya habari vinadai Michael alikuwa akibwia madawa lukuki ya kumudu maumivu ya mwili.Mengine yanadai alikuwa amekongoroka kupita kiasi.Gazeti moja limekwenda mbali zaidi na kudai kwamba eti miezi michache iliyopita,ilibainika wazi kuwa Michael alikuwa na miezi si zaidi ya sita ya kuishi.Lakini picha hizi zilizopigwa wakati wa rehersal zake zilizopangwa kufanyika O2 Arena mwezi ujao,zinatoa taswira tofauti kabisa.


0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube